Kigoma waharibu miundombinu ya umeme ya gridi ya taifa

Longoshe

Member
Jul 30, 2022
52
66
Wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma hazina huduma ya umeme, baada ya watu wasiojulikana kufanya hujuma katika miundombinu ya umeme kwenye kijiji cha Itumbiko wilayani Kakonko.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Kigoma Mhandisi Jafari Mpina amesema, watu hao wasiojulikana wamekata na kung’oa baadhi ya vipuri pamoja na kuchoma moto miundombinu ya umeme kwa makusudi.

Pia wameacha ujumbe unaosema kuwa, kama hawatapatiwa huduma ya umeme katika eneo la Itumbiko wataendelea kuchoma moto nguzo.

1.jpg
2.jpg
 
Huu wa gridi ya taifa si ndio una mgao kila siku??? Watakauwa wanaona bora wabaki na umeme wao kutoka congo ambao haukatiki katiki ovyo ovyo
Toka lini umeme wa kigoma una toka DRC?wa kwao wanatumia kutokana na mafuta.ungejua umeme wa DRC,hasa mashariki kuna mgao ambao cjawahi kuuona duniani,yaani kwa wiki mnapata umeme kwa siku mbili tu.kwa eneo husika,sasa miundo mbinu toka enzi za mobutu ndio zinazotumika hadi leo.
 
Toka lini umeme wa kigoma una toka DRC?wa kwao wanatumia kutokana na mafuta.ungejua umeme wa DRC,hasa mashariki kuna mgao ambao cjawahi kuuona duniani,yaani kwa wiki mnapata umeme kwa siku mbili tu.kwa eneo husika,sasa miundo mbinu toka enzi za mobutu ndio zinazotumika hadi leo.
Basi inaonesha huo wa mafuta ni bora kuliko hii gridi ya mgao wa taifa
 
Waha wabishi sn..wamefikia kuweka bifu na tanesco kwenye umeme!! Na lazima washinde hili

Ila kuwasha Moto nguzo ni ushamba
 
Watu wa Kigoma akili zao wanazijua wenyewe hapo wasipopelekewa umeme watalaumu nini
TANESCO wajitafakari.

Inawezekana waliwapa ahadi ya umeme muda mrefu na kila mara wanawazungusha kiboya boya kama Watoto au wanafanya upendeleo hasa kwa maeneo yenye watu maarufu kama viongozi

Hii ni kawaida kwenye serikali yetu kuahidi na kutotekeleza.
 
Ili kupatiwa/kufungiwa umeme hadi uanze kutumika kuna hatua zake.Sasa,wanataka muda huohuo wapate umeme?Wanadhani ni kama kukamua mawese?Waache upambaff wao.Wapeleleze,kamata,kipigo kikali,fungia kabatini(mahabusu) hadi siku ya kesi mahakamani waende wanachechemea.Marabook zao!
 
Safi sana hizi ndio mambo za kufanya yani umeme ukatize kijijini kwenu wakafaidi wa mjini wakati nyie mnauangalia tu? wametisha hii ndio inatakiwa viongozi waache ufala na dharau, wangekuwa wanagomea hata TOZO na CHAGUZI FEKI nchi ingekuwa mbali sana hiyo
 
Kigoma kuna mambo ya usiasa siasa sana na hasa kwenye masuala ya maendeleo...si jambo la ajabu umeme kutoka kijiji A ukaruka B na kwenda kuwaka C ukiuliza utasikia diwani wa B ni wa chama fulani....na haishi kwenye umeme tu hata barabara, maji, shule na vituo vya afya vinaenda kwa uchama khaaah....
 
Back
Top Bottom