Kigoma Ujiji yapokea mfumo wa taarifa za kijiografia(GIS)

Wiston Mogha

Senior Member
Feb 13, 2014
149
96
MADIWANI,WATAALAMU NA WATENDAJI WA KATA KTK MANISPAA YA KIGOMA.UJIJI WAPOKEA MFUMO WA (GIS )KWA FURAHA KUBWA WASEMA NI MKOMBOZI WA UKUSANYAJI MAPATO NA UPATIKANAJI TAARIFA ZA UENDESHAJI KTK KUPANGA MAENDELEO YA MJI.

Madiwani, wataalam na watendaji wa kata zote 19 wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma.Ujiji leo march 11, 2019 wamepokea mfumo wa taarifa za kijiografia(GIS) kwa furaha huku wakisema utasaidia katika uendeshaji wa halmashauri.

Mstahiki meya amesema hayo katika ukumbi wa Lake Tanganyika ambapo mafunzo yamefanyika ya kuwafundisha namna mfumo huo wa GIS utakavyofanya kazi, ambapo mafunzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka TAMISEMI chini ya mradi wa uendelezaji na ukuzaji miji kimkakati(TSCP).

Katika semina hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa kutoka katika vyama vyao ambapo wawakilishi wametoka katika chama ACT-Wazalendo, Chama Cha Mapinduz(CCM), na CHADEMA, Madiwani lakini pia viongozi wa Masoko yaliyopo katika halmashauri na watalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa kiwemo na watendaji wa kata.

Akifungua semina hiyo Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Hussein Ruhava ameshukuru TAMISEMI kwa kuamua kuanza mafunzo hayo kutolewa katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji kati ya halmashauri 8 zinazonufaika na mradi huo wa uendelezaji na ukuzaji wa Miji kimkakati Tanzania(TSCP).

Ameendelea kusema halmashauri ina kila sababu ya kusimamia vyanzo vya mapato kupitia mfumo wa taarifa za kijiografia(GIS) kwa kuwa Manispaa inayejegwa na wakazi wa manispaa wenyewe , wanasiasa na wataalamu waliopo huku akiwataka wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wapokee mfumo huo kwa mikono miwili kutokana na faida yake.

Naye kiongozi wa msafari wa wataalamu kutoka TAMISEMI na World Bank(WB) Eng. Nanai akiongea katika semina hiyo amesema imefika hatua sasa za halmashauri kuendeshwa kisasa kutokana na mfumo wa ukusanyaji taarifa za Kijiografia(GIS).

Ameendelea kusema halmashauri itatakiwa iwe na taarifa za walipa kodi wote kwani tayari mfumo uko tayari kufanya kazi huku akiwataka wanasiasa, wataalamu na viongozi wa masoko na wafanyabiashara kuwa na nia njema na kufikisha ujumbe kwa wananchi suala hilo.

Mtaalamu wa mfumo wa taarifa za kijiografia kutoka TAMISEMI Bi. Grace (kwa jina moja) amesema wamekuja kwa ajili ya kuwezesha halmashauri kutumia taarifa na namna zitakavyokuwa zikichakatwa kuingizwa katika mfumo.

Ameendelea kusema ni wajibu wa kila halmashauri kuajili wataalamu wa (GIS) kutokana na mfumo wa utambuzi wa taarifa za watu wote wakiwemo wakazi, wafanyabiashara na shughuli zinazofanyika katika kila eneo la halmashauri kwa kuzingatia mitaa pamoja na kata zote zilizopo.

Ameendelea kusema katika mfumo huo hauna madhara kwa wananchi bali unafaida katika upatikanaji wa taarifa za kijiografia uendeshaji na usimamizi wa halmashauri maeneo ya Masoko na utambuzi wa makazi lakini pia ikienda sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji wa halmashauri.

Mwenyekiti wafanyabiashara aliyehudhulia mafunzo hayo Ndg. Raymond Ndabyegese Soko la Mwanga amepongeza kwa mfumo huo na kusema utaleta ufanisi katika utendaji kazi mzuri wa halmashauri kuwafikia wananchi katika kutoa huduma mbalimbali huku akiahidi wafanyabiashara kupokea mfumo huo katika hali ya uzuri.

Madiwani wa manispaa na washiriki wa semina hiyo wakichangia mada katika semina hiyo Diwani wa kata ya Kigoma mjini Mhe. Hussein Kalyango na Mhe Kacheche Maulidi wamepongeza TAMISEMI kwa mfumo ambao wamekuja nao kwani utaweza kukuza mapato ya halmashauri na kuondoa migogoro baina ya wafanyabiashara wa halmashauri hiyo.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma.Ujiji mchumi wa halmashauri hiyo Ndugu. Frednandi Filimbi ameishukuru serikali kwa kuja na mfumo ambao utakuwa ni mkombozi katika uendeshaji wa halmashuri na kusema halmashauri kupitia watendaji na wataalamu wameupokea kwa mikono miwili na kuwataka wanasiasa nao kutoa ushirikiano katika maeneo yao ya utawala.

Naibu meya akifunga mafunzo kwa niaba ya mstahiki meya alimesisitiza madiwani na wataalamu kushiriki na kutoa ushirikiano kwa moyo mkubwa kufanikisha mfumo huu kufanya kazi nawakikishia hakuna mtu atakaye kwamisha kutoa takwimu za uongo atutakubali kama madiwani huu mfumo ni mkombozi kwetu manispaa.

Mfumo huu ndio mkombozi kwa wakazi wa manispaa kwa kudhibiti upotevu wa fedha lakini taarifa za Kiuchumi,kielimu,kiafya na kimipango mjini ujenzi na mazingira.
#Changekigoma
#Databasekwanza
#Kazinabata

Hussein kaliyango
Diwani kata ya kigoma
Mkiti Huduma za Jamii
Kigoma Municipal
11 March 2019
7dc062a1-a878-4665-9e60-05ae5edb62ac.jpg
2efd9f2d-5f97-4bce-b5ec-a5b04851391f.jpgSent using Jamii Forums mobile app
 
Ujiji kuna sehemu panaitwa BUZEBAZEBA wazee wa kitaa hicho wakikuelewa kama ukigombea jihesabu mshindi ila wakikukataa dah umeisha aise

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Back
Top Bottom