Kennedy
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 49,015
- 54,297
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, CP Thobias Andengenye anapenda kuwaarifu wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli kesho tarehe 19.09.2020 atapokea ugeni wa kiserikali, wa Rais wa Burundi, Mh. Evariste Ndayishimiye, ambaye atafanya ziara RASMI ya KISERIKALI nchini Tanzania hapa mjini Kigoma.
Mapokezi ya Mh. Rais Evariste Ndayishimiye yatafanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika. Wananchi wote mnaalikwa kufika Uwanja wa Lake Tanganyika saa mbili kamili asubuhi bila kukosa. Wananchi pia mnajulishwa kuwa, baada Mapokezi ya Ugeni huo na salaam kwa Wananchi, Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mgeni wake watafungua Jengo la Mahakama Kuu Kigoma katika eneo la Bangwe saa Tatu Kamili Asubuhi. Wananchi wote mnaalikwa pia kufika katika shughuli hiyo.