KIGOMA: Polisi watatu wakataa rushwa ya milioni tatu

Wakuacha

JF-Expert Member
May 19, 2015
2,041
1,323
Jana katika pita pita zangu nikiwa nimefika tu katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Nikaona ngoja nitembee tembee kidogo nishangae vumbi la Kasulu. Nikapita pale NMB nikachagua lugha kidogo nikajaa mfukoni. Nikasema si mbaya nikatafute japo juice nikaelekezwa sehemu moja pale karibia na sehemu wanauza piki piki pembeni yake kuna sheli ya mafuta najua wenyeji wanapajua hapa kidogo nikatupa macho upande wa pili nikaona vijana wa tatu.

Nikaangalia kwa umakini ni kama kuna kitu ki naendelea pale, nilikunywa juice kwa muda mrefu na wale vijana walikuwa pale kama kuna kitu fulani hivi wanakitafuta, mi nikitazama baada ya kumaliza juice yangu nikajisogeza pale ili nijue nini kinaendelea tyuu kufika pale.

"Nikaulizwa we ndo mwenye hii piki piki nikawajibu hapana, wakaniambia kaa hapa nika kaa, "mi mgeni nikajaribu kuwauliza wakadai wao ni maafisa wa polisi, kumbe yule muuzaji huwa anatoa bima feki aaahh nilipigwa na butwaa anagushi bima aisee, halafu mbaya wanaonunua piki piki huwa hawajui.

Jamaa akawavuta pembeni akawatangazia awape Millioni mbili jamaa akafika mpaka tatu inshu waipotezee lakini walimkomalia na hatimaye waliondoka nae hadi kituoni nikasema aisee kweli polisi wameanza kuwa wazalendo kukataa millioni tatu huku wakiwa watatu tu.

Aisee hawa wanastahili pongezi nilianza kuwaza kwa sauti kumbe unaeza kununua piki piki ukapewa bima feki huku kila ukikutana na trafik unamuambia nyumbani ipo originl hii ni copy yake, lakini nikajiuliza tena au huwa ni mchongo kati ya muuzaji na mnunuzi.
 
Jana katika pita pita zangu nikiwa nimefika tu katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Nikaona ngoja nitembee tembee kidogo nishangae vumbi la Kasulu. Nikapita pale NMB nikachagua lugha kidogo nikajaa mfukoni....nikasema si mbaya nikatafute japo juice nikaelekezwa sehemu moja pale karibia na sehemu wanauza piki piki pembeni yake kuna sheli ya mafuta najua wenyeji wanapajua hapa.....kidogo nikatupa macho upande Wa pili nikaona vijana Wa tatu ..nikaangalia kwa umakini ni kama kuna kitu ki naendelea pale,, Nilikunywa juice kwa muda mrefu na wale vijana walikuwa pale kama kuna kitu Fulani hivi wanakitafuta..mi nikitazama baada ya kumaliza juice yangu nikajisogeza pale ili nijue nini kinaendelea tyuu kufika pale..."""Nikaulizwa we ndo mwenye hii piki piki nikawajibu hapana....wakaniambia kaa hapa nikaa kaa.....""Mi mgeni nikajaribu kuwauliza wakadai wao ni maafisa Wa polisi.. Kumbe yule muuzaji huwa anatoa bima feki aaahh nilipigwa na butwaa ...anagushi bima aiseeee halafu mbaya wanaonunua piki piki huwa hawajui. jamaa akawavuta pembeni akawatangazia awape Millioni mbili jamaa akafika mpaka tatu inshu waipotezee lakini walimkomalia na hatimaye waliondoka nae hadi kituoni nikasema aiseeee Kweli Polisi wameanza kuwa wazalendo kukataa millioni tatu huku wakiwa watatu tu......Aiseee hawa wanastahili pongezi nilianza kuwaza kwa sauti kumbe unaeza kununua piki piki ukapewa bima feki uku kila ukikutana na Trafik unamuambia nyumbani IPO originl hii ni copy yake.. Lakini nikajiuliza tena au huwa ni mchongo kati ya muuzaji na mnunuzi......
Mkuu the less you know the better. Karibu dm upate uhalisia wa Kigoma, uvinza, kasulu, buhigwe, kibondo, kakonko.
 
Mkuu the less you know the better. Karibu dm upate uhalisia wa Kigoma, uvinza, kasulu, buhigwe, kibondo, kakonko.
Ahsante kwa sasa nipo maeneo ya NMB bank....nasikia mshikaji bado ameshikiliwa....
 
We ndio umezubaa mbona kutochukua rushwa mbele Ya watu jambo la kistaarabu tu,sitashangaa baada Ya masaa machache muuza pikipiki alirudi kwenye issue zake baada Ya kurekebisha.
 
hawa hawa mkulu aliyesema wapewe buku tano za kusafisha viatu wamekataa m tatu ...hatari sana...
 
Polisi zenyewe ni hizi za bongo, ukiende kituoni kuandika statement unaambiwa uende stationary ukanunue karatasi ya A4, ukienda kuriport kifo mnaambiwa defender ipo lakini hakuna mafuta.:D
 
Polisi zenyewe ni hizi za bongo, ukiende kituoni kuandika statement unaambiwa uende stationary ukanunue karatasi ya A4, ukienda kuriport kifo mnaambiwa defender ipo lakini hakuna mafuta.:D
Ulienda lin ukaambiwa hivyo.....au nawe ndio unatumia uzoefu wa kusikia yasemwayo tuu
 
Ulienda lin ukaambiwa hivyo.....au nawe ndio unatumia uzoefu wa kusikia yasemwayo tuu
Mkuu niliyashuhudia, nilikuwa home kijijini kwetu kabisa, jamaa alimpiga mke wake mpaka mauti yalimkuta yule mama, watu walikusanyika, ilibidi majukumu yagawanywe wengine waende polisi wilayani ili mwili wa marehemu ukahifadhiwe hospitali na polisi wachukue vipimo vyao. Waliokwenda polisi waliambiwa wajaze mafuta na walifanya hivyo.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom