Kigoma - Polisi wafanya tena kufuru ya mauaji ya kinyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigoma - Polisi wafanya tena kufuru ya mauaji ya kinyama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Dec 14, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Frasser Kashai

  Polisi sita mbaroni kwa kumuua mtuhumiwa
  • Wadaiwa kumpiga, kumng'oa rasta zake
  Askari sita wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumtesa na kumuua mtuhumiwa wa mauaji. Kabla ya mauaji ya mtuhumiwa huyo, Tatizo Michael (40), askari hao wanadaiwa kumnyoa nywele, kumpiga kichwani na mabegani kwa kutumia virungu hadi kumuua.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Frasser Kashai, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
  Kashai alisema tukio hilo lilitokea Desemba 3, mwaka huu katika kijiji cha Munyegera wilayani humo. “Tunawashikilia askari sita wanaotuhumiwa na uchunguzi unaendelea…ikibainika kuwa walihusika, watafukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” Kamanda Kashai alisema. Hata hivyo, Kashai alikataa kutaja majina ya askari hao kwa maelezo kuwa uchunguzi bado unaendelea na kwamba utakapokamilika, taarifa rasmi itatolewa kwa umma.

  Akizungumza na NIPASHE nyumbani kwake kijijini Munyegera, baba wa marehemu, Michael Dunduru (80), alidai kushuhudia askari hao wakimkimbiza mwanawe na walipofika eneo la mto Nyanga, walimkamata na kuanza kumpiga.
  Kwa mujibu wa Dunguru, askari hao walitumia virungu kumpiga (marehemu) kichwani, begani na kwenye sehemu za siri. Alidai kuwa kutokana na kipigo hicho, Tatizo alivuja damu puani na mdomoni. Alidai kuwa Desemba 4, mwaka huu, alipokea taarifa kutoka polisi wilayani Kasulu ikieleza kuwa mtoto wake (Tatizo), amefariki dunia. “Baada ya kupata taarifa hizo, nilikwenda hadi kituo cha polisi, nilimkuta mtoto wangu, Tatizo amelazwa chali, amekufa…damu zikawa zimejaa kichwani, shingoni, mdomoni na puani,” alidai.


  Dunguru alidai kwamba aliamriwa na maofisa kadhaa wa polisi mkoani Kigoma kuchukua maiti ya mtoto wake Tatizo, kwa madai kuwa askari wanaotuhimiwa kuhusika na mauaji hayo, wanashikiliwa na jeshi hilo.
  Alidai kukaidi agizo hilo na kuhoji sababu ya kifo cha Tatizo, ambapo polisi walimjibu kwamba kilitokana na kipigo kinachodaiwa kufanywa na askari polisi.
  Dunguru alichukua mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi, lakini akaomba hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongela, alifika kijijini Munyegera Desemba 8, mwaka huu na kusisitiza nia ya serikali kuwachukulia hatua stahiki watuhumiwa wa mauaji hayo.
  Naye Mbunge wa Manyovu (CCM), Albert Tabaliba, alisema mauaji hayo ni ishara za ukosefu wa uungwana na kuongeza: “Kazi ya polisi ni kumkamata mtu akiwa hai, kumpeleka kituoni na kumfungulia mashtaka…si kuua raia, taratibu hizi za kuua raia ni kinyume cha sheria za nchi,” alisema.


  Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, Joshua Monge, alithibitisha kupokea mwili wa marehemu na kuufanyia uchunguzi.
  Monge alisema kifo cha marehemu Tatizo kilitokana na kupigwa kichwani na kusababisha jeraha ambalo lilivuja damu nyingi na (marehemu) alikuwa na michubuko begani.


  Tukio hili limekuja siku chache baada ya askari wengine wanane wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kasulu kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kumtesa, kumpa kipigo na kumuua raia, Festo Andrea, kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha.
  Askari hao wanadaiwa kumpiga kichwani na kwenye mbavu kwa kutumia kitako cha bunduki na kumwekea miti kwenye sehemu zake za haja kubwa.
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  [/QUOTE]"Tunawashikilia askari sita wanaotuhumiwa na uchunguzi unaendelea…ikibainika kuwa walihusika, watafukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake," Kamanda Kashai alisema. Hata hivyo, Kashai alikataa kutaja majina ya askari hao kwa maelezo kuwa uchunguzi bado unaendelea na kwamba utakapokamilika, taarifa rasmi itatolewa kwa umma.[/QUOTE] Hapo kwenye red aache kunipandisha hasira,.zombe na wenzie waliua mchana kweupe wameachiwa na sasa wanadai walipwe mabilioni ya fidia...polisi nyinyi ni wabaya kuliko majambazi
  muachieni samson mwigamba
   
 3. v

  valid statement JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  MJINI SHULE...
  Hao wataamishwa tu vituo va kazi.
  Na kuhamishiwa mikoa mengine.
  Labda kama ndugu wa marehemu wafuatilie haki bin haki.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  @Maandamano@ Isitoshe wale askari walioua juzi juzi ule huko huko Kigoma na kumsokomeza vijiti sehemu za kujisaidia kabla ya kumtoa roho shauri lao limeishia wapi? Kama wangechukuliwa sheria stahili hawa askari wengine wasingerudia kola lilelile.
   
Loading...