Kigoma - Polisi anapoonyesha mazingira ya kupokea rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigoma - Polisi anapoonyesha mazingira ya kupokea rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 22, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Picha na Dail Nkoromo blog

  Trafiki ni Tanzania nzima! Askari wa kikosi hicho akimhoji kiaina jambo mwendesha pikipiki mjini Kigoma leo huku akipokea msosi.

  Picha hii hapo Juu inatoa taswira yenye utatanishi kwani mwonekano wa mwendesha pikipiki na askari polisi wakiwa na wasiwasi huku mikono ikiwe na reaction ya kuonyesha kinachoendelea. Uwazi wa tukio hilo unaashiria gharama ya haki nchini Tanzania ilivyongumu kuthibitiwa hasa adui wa haki Rushwa kushamiri kwenye vyombo vya usalama vyenye dhamana ya kulinda sheria ya nchi.
   
 2. k

  kipuri Senior Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  hii nayo ni habari ya siasa!
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hili jambo msilizungumzie linashughulikiwa!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Majukumu ya serikali na taasisi zake si shughuli za siasa?
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Haya yote yako ndani ya chama tawala

  cha mafisadi!
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  12012009184.jpg Hapo hapaandikwi kitu ni geresha tu.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  simulaumu hata kidogo mama wa watu. hana ubavu wa kumteka Dr.Uli; hana chansi ya kusoma zaidi kuongeza maarifa; hana nafasi ya kuhudhuria vikao vya kutunga matukio ya kuonesha silaha kwenye tivi. anaishi kwenye nyumba ambayo shuka hutumika kama ukuta wa kutenganisha chumbani kwake anakolala na sebuleni wanakolala watoto wake.

  dawa ni kuipiga chini ccm tu.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kila yanapoanikwa hadharani mambo haya inamaana kwamba ni kuongeza mafuta kwenye kibatari.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Tunaangalia upande mmoja tu katika utoaji na upokeaji rushwa. Anayeandamwa ni mpokea rushwa, lakini hatumnyoshei kidole mtoa rushwa katika shauri kama hili. Madereva wengi ndo chanzo cha askari kujiingiza kwenye rushwa. Madereva ndio wanaoomba kutoa rushwa ili waachiwe.
   
 10. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  hili lipo mahakamani
   
 11. washwa washwa

  washwa washwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 1,522
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Kwani haiwezekani huyo traffic akawa wlimtuma chakula huyo mwendendesha piki piki
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh teh, we bana. Kuna vibanda vingi tu pale na migahawa sidhani kama dhamira kwa mwonekana huo alikuwa anamtuma kumnunulia chakula yule mama askari. Wote wana wasiwasi, kila mmoja anachunga mwelekeo aliko asionwe, na mpiga picha alikuwa mjanga na pasi shaka alitumai simu, maana camera ya kawaida angeshtukiwa. Siku hizi inabidi kuwa makini sana.
   
 13. N

  Njele JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh, mchana kweupe bila aibu huku wapita njia wanashuhudia na mwendesha bodaboda mwingine akiwa karibu. Mazoea hujenga tabia.
   
 14. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Acheni watoe maana bila Traffic humu barabarani tusingepita na ni ajali tupu, kuna watu wanapokea mlungula km Madaktari? yaani yuko radhi mkeo apoteze maisha bila kumpa kuanzia 50,000 hatamfanyia operation Wanafuatiwa na POLISI kuingia rumande wanashangiliwa na hakuna anayetoka bila kuachia kitu kidogo la sivyo utamaliza hapo wiki na sio 24hrs za kishria hujafika Mahakamani utaambiwa na Karani hakimu anataka kuanzia 50,000 ili upate dhamana kesi yoyte ya janai ukibisha unapanda karandika ni siku 14 kula ugali na zege mpaka remove order ikutoe tena ya 200,000 Nachosema hapo mbona padogo traffic mwacheni apete kiboko ni MBUNGE
   
 15. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hii picha imekaa kama Zanzibar vile! Ambako trafiki ama mmoja mmoja au kikundi, wamegwa maeneo yao ya kupokea rushwa. Mara nyengine wanakaa barabarani kwa zamu.
   
 16. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,309
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Fedha ndiyo inayo fungwa pingu.
   
 17. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Sasa huyu jamaa wa pikipiki anatembea na vyakula ili akishikwa na trafiki ndiyo awape kama rushwa? Huyo trafiki hawezi kuwa na wasiwasi wa kuwekewa sumu au kitu chochote kibaya kwa mtu unaye mgendua!
   
 18. v

  vngenge JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Acheni vyombo vya dola vifanye kazi yake, msiviingilie
   
Loading...