Kigoma: Mwanamume amkata kwa kisu shingoni Mke wake kisa wivu wa Mapenzi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,649
2,000
Mwanamke wa kijiji cha Mahembe Kigoma anusurika kifo baada ya mume wake kumkata kwa kisu shingoni kutokana na wivu wa mapenzi.

Mwanamke mkazi wa Kijiji cha Mahembe, Wilaya ya Kigoma,Bibi SIYAJUI ALMAS, amenusurika kifo baada ya mume wake aitwaye, MAGURU SHABANI, kumkata kwa kisu shingoni kwania ya kumuua kutokana na wivu wa mapenzi.
Akieleza hali ilivyokuwa, majeruhi SIYAJUI ALMAS ambaye amelazwa katika Kituo cha Afya Bitale Wilayani Kigoma, amesema mumewe amechukua uamuzi huo baada ya kutokea kutoelewana baina yao kutokana na shutuma za usaliti wa mapenzi.

Amesema mumuwe alikimbia baada ya kuhisi kuwa amekufa na kwamba kutokana na kupiga kelele majirani na wifi yake walifika kumsaidia.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bitale, Bwana NORBERT NSHEMETSE amesema majeruhi ambaye amepokelewa akiwa amepoteza damu nyingi anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.

Polisi inaendelea kumsaka mume wa majeruhi ambaye ametoroka baada ya tukio.

Chanzo: ITV
 

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,672
2,000
Huo ni ujinga ulio pitiliza!
Huyo apewe fundisho
Amekushinda achana nae
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom