Akieleza hali ilivyokuwa, majeruhi SIYAJUI ALMAS ambaye amelazwa katika Kituo cha Afya Bitale Wilayani Kigoma, amesema mumewe amechukua uamuzi huo baada ya kutokea kutoelewana baina yao kutokana na shutuma za usaliti wa mapenzi.
Amesema mumuwe alikimbia baada ya kuhisi kuwa amekufa na kwamba kutokana na kupiga kelele majirani na wifi yake walifika kumsaidia.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bitale, Bwana NORBERT NSHEMETSE amesema majeruhi ambaye amepokelewa akiwa amepoteza damu nyingi anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.
Polisi inaendelea kumsaka mume wa majeruhi ambaye ametoroka baada ya tukio.
Chanzo: ITV
My take: Michepuko siyo dili, tutakuja kutoana roho bure!