Kigoma: Mtoto adai urithi kwa baba yake mahakamani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,867
Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni. Wakati baadhi ya wazazi wakifurahia mafanikio ya watoto wao, hali ni tofauti kwa Mzee Kharid Segeleje (80), aliyefikishwa mahakamani na mwanaye wa kumzaa.

Mzee huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mwamgongo wilayani Kigoma, amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kigoma na mwanawe, Abas Kharid anayetaka akimdai baba yake huyo urithi wake.

Kesi hiyo ya madai namba nane ya mwaka 2021 ilisikilizwa juzi na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kenneth Mutembei.

Mashtaka hayo yamewasilishwa mahakamani hapo baada ya mtoto huyo kukata rufaa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kalinzi ambako baba yake alishinda kesi aliyokuwa anakabiliwa nayo.

Mtoto huyo ameieleza mahakama kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kuona mali za baba na mama yake ambaye ameshafariki hazimnufaishi, hivyo anataka sehemu inayomstahili ili aitumie kama anavyopenda kwani kwa sasa hawezi kufanya hivyo bila ridhaa ya baba yake.

Alifafanua kuwa mali hizo zimekuwa zikimnufaisha mke mwingine wa baba yake aliyemuoa baada ya mama yake kufariki.

Baada kusikiliza maelezo ya kesi hiyo, Hakimu Mutembei ameagiza iendeshwe kwa njia ya maandishi hivyo upande wa mlalamikaji utatakiwa kuwasilisha hoja zake Jumatatu ijayo ambayo ni Juni 28.

Wakati mlalamikaji akipangiwa tarehe hiyo, hakimu huyo ameutaka upande wa utetezi kuwasilisha taarifa zake Julai 5 ili kumpa yeye nafasi ya kutoa hukumu. Hakimu huyo amesema pande zote mbili zitatakiwa kwenda mahakamani hapo Julai 12 ili kupangiwa tarehe ya hukumu.

Mali zilizoorodheshwa katika mgogoro huo kuanzia mahakama ya mwanzo ni nyumba na shamba la michikichi lenye ukubwa wa ekari 20.

Wakili anayemtetea mzee huyo, Thomas Msasa amesema amejitoa kuhakikisha anamsaidia mtuhumiwa kupata haki yake bila gharama yoyote.

Ingawa damu ni nzito, lakini muafaka umeshindwa kupatikana kati ya Mzee Segeleje, hata hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Kalinzi haijamfurahisha Abas aliyeamua kuidai haki hiyo katika mahakama ya juu zaidi.

Iwapo hakuna kitakachobadilika ndani ya wiki mbili, basi nyundo ya mwisho itakayogongwa na Hakimu Mutembei itatoa mwanzo mpya kwa wawili hao au kuwa mwanzo wa rufaa nyingine.
 
Huyo kijana yupo sahihi maana hapo ni kwa wazazi wake... Huyo mzee itabidi nae akakae kwa wazazi wake.

Shida ni moja, inawezekana mama yake alipigana sana kutafuta hizo mali, na pengine ndie alikuwa mmiliki. Sasa amefariki anaona baba kaoa mke mwingine na pengine akiwa na watoto na wanafaidika na mali za mama yake.
Unaweza ona anakosea, lakini akawa sahihi kwa namna nyingine.
 
Mzee ni mtu mzima sana 80's na ameoa mwanamke mwingine baada ya mama wa kijana aliyechuma mali na mzee kufariki. Kwa hio mama mpya anaweza kumlaghai mzee na kujimilikisha mali zote. Kwa hio mzee azigawe mali zake mapema kuepusha migongano basi.
 
Back
Top Bottom