Kigoma: Mkoa pekee haujaunganishwa na umeme na barabara hadi 2020

Kuna lami flani kutoka nyakanazi hadi kibondo.. umbali wake haufiki hata Km 100 lakini hio lami imeanza kujengwa mimi nikiwa naenda kuanza form 5 2011 mpaka leo haijaisha.

Wakati kuna barabara ndefu zaidi ya hio zimejengwa na zimeisha lakini hii haiishi na maraisi wote wamepita na kuweka ahadi za uongo.

Mbaya zaidi mbunge wa jimbo la muhambwe ni naibu waziri wa uchukuzi lakini hakuna anachofanya boya yule.. na sasa hivi akipita basi atakua ameiba maana hakuna anayemtaka .. wakifanya free and fair election hata akisimama na mtoto wa form 2 c bora tumchague mtoto.
 
Nimeshangaa kusikia Kigoma bado hufiki kwa lami kutoka Tabora na hata umeme bado? Mbona tunasikia umeme unapelekwa vijiji vyote ifikapo 2021? Au hatuambiwi ukweli?

kigoma ni nchi inayojitegemea, ni nchi inayokaliwa kimabavu na Tanzania au ni koloni la Tanzania.
 
Umeme upo wa generator sio kutoka national grid.. lugha rahisi hautoki kwenye manguzo makubwa unayo kutana nayo mikoa mingine..

Tafuta zile nguzo kubwa zinazo katiza mapori kama utaziona kigoma.
Nimeshangaa kusikia Kigoma bado hufiki kwa lami kutoka Tabora na hata umeme bado? Mbona tunasikia umeme unapelekwa vijiji vyote ifikapo 2021? Au hatuambiwi ukweli?
 
Mkoa kigoma ni mkoa wenye bahati mbaya sana pamoja na kuwa na bahati ya kutoa vipaji katika kila eneo kutoka soka, mziki hadi wasomi waziri na wanasiasa machachari hapa Tanzania.

Lakini cha ajabu hadi leo Tarehe 23 .o8.2020 mkoa kigoma haujaunganishwa kwa barabara ya lami .. na pia haujaunganishwa na grid ya taifa ya umeme.

Mkoa huu kiuchumi upo eneo zuri sana , na kila mmoja atakubaliana kwamba kuufungua mkoa huu kwa miundo mbinu utachochea ukuaji wa uchumi ukanda wa ziwa na Tanzaniankwa ujumla.

Mwaka 2015 tuliahidiwa kwamba Ujiji itakua Dubai, lakini hadi leo bado ujiji ni ujiji.

Tuna amini serikali itakayo chaguliwa kwa haki na kwa uhuru 2020 itatekeleza ahadi zote za mkoa wa kigoma.

Kama wananchi tunaendelea Kumwomba mola juu ya utekelezaji wa miradi katika marneo haya mawili
1. Umeme
2. Barabara

Kigoma ni nchi yaani zenji gridi ya Taifa ipo lakini Kigoma hakuna
 
BTW huyu ndio Tabutupu ... .... ..

Sasa huu ndio unafiki au kitu gani? Propaganda za kishamba na majungu?
Tafuta nguzo kama hizi mkoani kigoma kama utazikuta? Ukizikuta nakupa zizi zima la mbuzi huku karagwe.
IMG-20200823-WA0014.jpeg
 
Mkoa kigoma ni mkoa wenye bahati mbaya sana pamoja na kuwa na bahati ya kutoa vipaji katika kila eneo kutoka soka, mziki hadi wasomi waziri na wanasiasa machachari hapa Tanzania.

Lakini cha ajabu hadi leo Tarehe 23 .o8.2020 mkoa kigoma haujaunganishwa kwa barabara ya lami .. na pia haujaunganishwa na grid ya taifa ya umeme.

Mkoa huu kiuchumi upo eneo zuri sana , na kila mmoja atakubaliana kwamba kuufungua mkoa huu kwa miundo mbinu utachochea ukuaji wa uchumi ukanda wa ziwa na Tanzaniankwa ujumla.

Mwaka 2015 tuliahidiwa kwamba Ujiji itakua Dubai, lakini hadi leo bado ujiji ni ujiji.

Tuna amini serikali itakayo chaguliwa kwa haki na kwa uhuru 2020 itatekeleza ahadi zote za mkoa wa kigoma.

Kama wananchi tunaendelea Kumwomba mola juu ya utekelezaji wa miradi katika marneo haya mawili
1. Umeme
2. Barabara

Subiri ahadi hewa wakati wa kampeni, baada ya kampeni hautawaona TENA
 
Kwanini watu wa Kigoma hawapaswi kuichagua CCM 2020?

Sababu 5 tu

1. Umasikini: Mkoa wa Kigoma ni moja ya mikoa 5 masikini zaidi nchini Tanzania. Licha ya Utajiri mkubwa katika Kilimo, Uvuvi, Utalii na Biashara ya Kimataifa, Serikali ya CCM imeitenga Kigoma Kwa kuinyima Miradi ya Maendeleo ya Watu. Mfano Kwa miaka 5 Serikali imechelewesha Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Mto Luiche wa Hekta 3000 unaofadhiliwa na Serikali ya Kuwait. CCM inaiweka Kigoma kwenye Umasikini.
2. Bandari ya Kigoma: Uchumi wa Mkoa wa Kigoma ni Bandari ya Kigoma. Serikali ya CCM imeua Bandari ya Kigoma na hivyo kuua Biashara katika Mji wa Kigoma. Wakati Bandari inaendeshwa na Kampuni ya AMI mzigo mwingi wa Kongo ( DRC ) ulikuwa unapita Bandari ya Kigoma. Sasa Bandari haipati mizigo. Juhudi za kuboresha Bandari zimekwamishwa na Serikali ya CCM kwa makusudi. Serikali ya CCM imezuia, Kwa miaka 5 sasa, Mradi mkubwa wenye thamani ya Shs Bilioni 100 kupanua Bandari ya Kigoma. Msaada huu kutoka Serikali ya Japan umezuiwa Kwa makusudi ili kuhamisha Bandari kwenda Karema na kujenga Meli ya mizigo huko Karema. CCM inahujumu Bandari ya Kigoma. Hata Uwanja wa Ndege wa Kigoma ( Gombe/Mahale International Airport ) umehujumiwa na kupelekwa Chato.
3. Reli ya Kisasa: Wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaondoka madarakani mpango wa Ujenzi wa Reli ulikuwa ni kujenga Reli kutoka Dar - Tabora - Uvinza - Musongati ( Burundi ) ili kuifanya Uvinza kuwa Bandari Kavu na Kituo kikubwa cha Mizigo kutoka Nchi za Maziwa Makuu. Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imebadilisha njia na kuamua kupeleka Reli Mwanza. Bandari ya Kigoma inaweza kuhudumia 40% ( kwenda Burundi na DRC ) ya mizigo yote inayoingia Bandari ya Dar es Salaam Wakati Bandari ya Mwanza inahudumia 6% tu ( kwenda Uganda ). CCM imehamisha Mradi wa Reli na kuihujumu Kigoma.
4. Umeme: Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 iliahidi Mradi wa Umeme wa Mto Malagarasi 44MW. Baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia Madarakani imeufuta Mradi huo Kwa kisingizio cha kujenga Bwawa la Rufiji ( Stigler’s Gorge ). Mkoa wa Kigoma haupo Gridi ya Taifa na hivyo kukosa Umeme wa Uhakika Kwa ajili ya Maendeleo ya Viwanda. Hata Mradi wa sekta Binafsi wa Umeme wa Jua ( 5MW ) ambao ungepunguza gharama za kuzalisha Umeme hapa Kigoma Kwa 50% Serikali ya CCM imekataa kuutumia licha ya Mradi huo kumalizika tangu Septemba 2017. Benki ya Maendeleo ya Afrika ilitoa Fedha za Mradi wa Umeme wa Malagarasi lakini Serikali ya CCM ikalazimisha zipelekwe Stigler’s Gorge badala ya Igamba II. Hujuma za CCM dhidi ya Mkoa wa Kigoma hazimithiliki.
5. Barabara: Mkoa wa Kigoma ndio Mkoa Pekee ambao Wilaya zake Kongwe ( Kasulu, Kigoma na Kibondo ) hazijaunganishwa kwa lami. CCM wanaufanya Mkoa wa Kigoma kuwa wa mwisho kwa kila kitu. Barabara ya Uvinza - Malagarasi darajani Ina fedha za ufadhili wa Abu Dhabi Fund lakini Serikali kwa makusudi haifuatilii. Barabara ya Kigoma - Nyakanazi ndio sasa imepata fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ucheleweshaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya CCM ya Awamu 5. Serikali ya Rais Magufuli imemaliza miaka 5 haijajenga hata kipande cha 1km ya barabara katika Mkoa wa Kigoma. CCM haiipendi Kigoma.

Kwa sababu hizi 5 Mtu wa Kigoma anayechagua CCM hana mapenzi na Mkoa wa wake. Kila mwana Kigoma anapaswa kuikataa CCM ili Serikali iamke. Wana Kigoma wamefanya hivyo mara kadhaa na kufanikiwa. Barabara za Mwandiga - Manyovu na Kigoma - Kidahwe, Pia daraja la Mto Malagarasi vimejengwa Wakati Kigoma ilipoamua kuchagua wabunge wa Upinzani na kuwanyima Kura wagombea Urais wa CCM. Wembe ule ule wa 2005, 2010 na 2015 tuugeuze upande wa Pili kwa faida ya Kigoma.

Kigoma bila CCM Inawezekana. Mpende anayekupenda, asiyekupenda achana naye. CCM haipendi Kigoma, wana Kigoma tuachane na CCM.

ZITTO KABWE
MB KIGOMA MJINI
10TH SEP 2020
 
Hakuna lami.. uvinza vs tabora vumbi..

Ujiji vs kibondo vs nyakanazi vumbi..
Wacha unafiki na Upumbavu
Nikipande kidogo tu Kutoka Uvinza mpaka Mpeta 50km
Ndio hazina Lami
Kipande cha Nguruka Ugansa kuna mkandarasi anajenga
Kaliwa Urambo Lami mpaka tabora
 
Km 50 ndio ndogo... nini kimekwamisha kikamilisha..

Zile bil 39 mlizocehezea toch kujenga uwanja wa ndege si zingekua zimekamilisha..

Usikute hata kijijini kwenu hakuna hata barabara ya vumbi kazi kushabikia mambo kwa njaa..
Wacha unafiki na Upumbavu
Nikipande kidogo tu Kutoka Uvinza mpaka Mpeta 50km
Ndio hazina Lami
Kipande cha Nguruka Ugansa kuna mkandarasi anajenga
Kaliwa Urambo Lami mpaka tabora
 
Mkoa kigoma ni mkoa wenye bahati mbaya sana pamoja na kuwa na bahati ya kutoa vipaji katika kila eneo kutoka soka, mziki hadi wasomi waziri na wanasiasa machachari hapa Tanzania.

Lakini cha ajabu hadi leo Tarehe 23 .o8.2020 mkoa kigoma haujaunganishwa kwa barabara ya lami .. na pia haujaunganishwa na grid ya taifa ya umeme.

Mkoa huu kiuchumi upo eneo zuri sana , na kila mmoja atakubaliana kwamba kuufungua mkoa huu kwa miundo mbinu utachochea ukuaji wa uchumi ukanda wa ziwa na Tanzaniankwa ujumla.

Mwaka 2015 tuliahidiwa kwamba Ujiji itakua Dubai, lakini hadi leo bado ujiji ni ujiji.

Tuna amini serikali itakayo chaguliwa kwa haki na kwa uhuru 2020 itatekeleza ahadi zote za mkoa wa kigoma.

Kama wananchi tunaendelea Kumwomba mola juu ya utekelezaji wa miradi katika marneo haya mawili
1. Umeme
2. Barabara

Hotuba ya Zitto 10th Sep 2020

Kwanini watu wa Kigoma hawapaswi kuichagua CCM 2020?

Sababu 5 tu

1. Umasikini: Mkoa wa Kigoma ni moja ya mikoa 5 masikini zaidi nchini Tanzania. Licha ya Utajiri mkubwa katika Kilimo, Uvuvi, Utalii na Biashara ya Kimataifa, Serikali ya CCM imeitenga Kigoma Kwa kuinyima Miradi ya Maendeleo ya Watu. Mfano Kwa miaka 5 Serikali imechelewesha Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Mto Luiche wa Hekta 3000 unaofadhiliwa na Serikali ya Kuwait. CCM inaiweka Kigoma kwenye Umasikini.
2. Bandari ya Kigoma: Uchumi wa Mkoa wa Kigoma ni Bandari ya Kigoma. Serikali ya CCM imeua Bandari ya Kigoma na hivyo kuua Biashara katika Mji wa Kigoma. Wakati Bandari inaendeshwa na Kampuni ya AMI mzigo mwingi wa Kongo ( DRC ) ulikuwa unapita Bandari ya Kigoma. Sasa Bandari haipati mizigo. Juhudi za kuboresha Bandari zimekwamishwa na Serikali ya CCM kwa makusudi. Serikali ya CCM imezuia, Kwa miaka 5 sasa, Mradi mkubwa wenye thamani ya Shs Bilioni 100 kupanua Bandari ya Kigoma. Msaada huu kutoka Serikali ya Japan umezuiwa Kwa makusudi ili kuhamisha Bandari kwenda Karema na kujenga Meli ya mizigo huko Karema. CCM inahujumu Bandari ya Kigoma. Hata Uwanja wa Ndege wa Kigoma ( Gombe/Mahale International Airport ) umehujumiwa na kupelekwa Chato.
3. Reli ya Kisasa: Wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaondoka madarakani mpango wa Ujenzi wa Reli ulikuwa ni kujenga Reli kutoka Dar - Tabora - Uvinza - Musongati ( Burundi ) ili kuifanya Uvinza kuwa Bandari Kavu na Kituo kikubwa cha Mizigo kutoka Nchi za Maziwa Makuu. Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imebadilisha njia na kuamua kupeleka Reli Mwanza. Bandari ya Kigoma inaweza kuhudumia 40% ( kwenda Burundi na DRC ) ya mizigo yote inayoingia Bandari ya Dar es Salaam Wakati Bandari ya Mwanza inahudumia 6% tu ( kwenda Uganda ). CCM imehamisha Mradi wa Reli na kuihujumu Kigoma.
4. Umeme: Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 iliahidi Mradi wa Umeme wa Mto Malagarasi 44MW. Baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia Madarakani imeufuta Mradi huo Kwa kisingizio cha kujenga Bwawa la Rufiji ( Stigler’s Gorge ). Mkoa wa Kigoma haupo Gridi ya Taifa na hivyo kukosa Umeme wa Uhakika Kwa ajili ya Maendeleo ya Viwanda. Hata Mradi wa sekta Binafsi wa Umeme wa Jua ( 5MW ) ambao ungepunguza gharama za kuzalisha Umeme hapa Kigoma Kwa 50% Serikali ya CCM imekataa kuutumia licha ya Mradi huo kumalizika tangu Septemba 2017. Benki ya Maendeleo ya Afrika ilitoa Fedha za Mradi wa Umeme wa Malagarasi lakini Serikali ya CCM ikalazimisha zipelekwe Stigler’s Gorge badala ya Igamba II. Hujuma za CCM dhidi ya Mkoa wa Kigoma hazimithiliki.
5. Barabara: Mkoa wa Kigoma ndio Mkoa Pekee ambao Wilaya zake Kongwe ( Kasulu, Kigoma na Kibondo ) hazijaunganishwa kwa lami. CCM wanaufanya Mkoa wa Kigoma kuwa wa mwisho kwa kila kitu. Barabara ya Uvinza - Malagarasi darajani Ina fedha za ufadhili wa Abu Dhabi Fund lakini Serikali kwa makusudi haifuatilii. Barabara ya Kigoma - Nyakanazi ndio sasa imepata fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ucheleweshaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya CCM ya Awamu 5. Serikali ya Rais Magufuli imemaliza miaka 5 haijajenga hata kipande cha 1km ya barabara katika Mkoa wa Kigoma. CCM haiipendi Kigoma.

Kwa sababu hizi 5 Mtu wa Kigoma anayechagua CCM hana mapenzi na Mkoa wa wake. Kila mwana Kigoma anapaswa kuikataa CCM ili Serikali iamke. Wana Kigoma wamefanya hivyo mara kadhaa na kufanikiwa. Barabara za Mwandiga - Manyovu na Kigoma - Kidahwe, Pia daraja la Mto Malagarasi vimejengwa Wakati Kigoma ilipoamua kuchagua wabunge wa Upinzani na kuwanyima Kura wagombea Urais wa CCM. Wembe ule ule wa 2005, 2010 na 2015 tuugeuze upande wa Pili kwa faida ya Kigoma.

Kigoma bila CCM Inawezekana. Mpende anayekupenda, asiyekupenda achana naye. CCM haipendi Kigoma, wana Kigoma tuachane na CCM.

Wakandarasi wako kazini. Usiogope under Magufuli everything is possible . Songea tumeunganishwa na Grid ya Taifa iliyowashinda awamu zote. Kipindi cha Magufuli nchi nzima itakuwa imeungwa na grid ya taifa. Na barabara zote za mikoa zitakuwa lami. Kwa barabara ya Katavi Kigoma mkandarasi yuko kazini, Kigoma Nyakanazi mkandarasi yuko kazini, Kigoma Tabora yuko kazini. So tumpe kura rais Magufuli. Baba mpenda maendeleo.
 
Kadanganye wasio jielewa..

Back
Top Bottom