Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Matokeo ya kiti cha ubunge jimbo la kigoma mjini yametoka lakini katika mazingira ya kutatanisha. Mpaka saa 2 asubuhi leo mgombea wa CHADEMA Ali Khalfan Mlei alikuwa akiongoza kwa kura zaidi ya kura 480 dhidi ya mgombea wa CCM Peter Serukamba. Watu wengi walikusanyika nje ya ofisi za mkurugenzi wa manispaa ya kigoma/ujiji kushinikiza msimamizi kutangaza matokeo. Polisi wenye silaha wamezunguka ofisi hizo kulinda usalama.
Muda mfupi uliopita msimamizi ametangaza kuwa mgombea wa CCM ameshinda kwa zaidi ya kura 1,000 dhidi ya mgombea wa CHADEMA. sasa hivi mji wa kigoma ni fujo za hatari FFU wakiwa kwenye magari yao wanapiga mabomu ya machozi na uharibifu unaweza kutokea kwani watu wameingia mitaani kupinga matokeo..............