Kigoma: Mbona ahadi ya Rais kuibadilisha Kigoma kuwa Dubai hatekelezwi?

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,998
6,659
Wananchi wengi wa Mkoa wa Kigoma wamekasirishwa na Ahadi za Rais ambazo wameshaona hazitekelezeki za kubadilisha mkoa wao kuwa kama dubai kushindikana wamesema wanataka angalau barabara kwasababu swala la kuifanya kuwa dubai haliwezekaniki hata wakipewa miaka mia chini ya uongozi dhaifu wa CCM hilo ni ndoto. hata waliposikiliza hotuba ya waziri wa Aridhi prof Anna Tibaijuka hakuongelea suala kama hilo kilicho waudhi zaidi hata mji mpya wa kigamboni umetengewa asilimia chache mno kwenye budget. sasa wanashangaa kilichowaleta wakina Nape na team yake nini? badala ya kupeleka makandarasi.
source ni mimi mwenyewe nipo kigoma
 
Wananchi wengi wa Mkoa wa Kigoma wamekasirishwa na Ahadi za Rais ambazo wameshaona hazitekelezeki za kubadilisha mkoa wao kuwa kama dubai kushindikana wamesema wanataka angalau barabara kwMKIENDA KIGOMA LEO WAAMBIENI WATU WAHUKO KWAMBA MMEFUTA SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA.
KWA SASA NI MFUMO WA KIFISADI NDI MNAOUFUATA.
WAZIRI YEYOTE AKIIBA ANAJIUZURU TU HAKUNA MASHITAKA.
CCM HAINA MSEMAJI KILA MTU HATA AKIWA MSALANI ANAKUWA MSEMAJI WA CHAMA.
SIKU 90 ZA MAFISADI ULITELEZA HAMKUMAANISHA HIVYO ILIKUWA MIAKA 90.
CCM IMEANZISHA KITENGO CHA CHINJACHINJA IKIZIDIWA HOJA.
KATIKA HOTUBA ZENU 90%YA MUDA WENU MUUTUMIE KUWASEMA CHADEMA TU
HAPO MTAPATA KADI NYINGI ZA CHADEMA.
 
Godbless Lema alisema kuwa PM ni mwongo, nami nasema JK ni mwongo kuliko PM.
 
Kikwete alitudaganya sisi watu wa kigoma barabara zinamshinda ndio ataweza kujenga mahekalu ya Dubai
 
Poleni sana huyu msanii jk kawaacha njia panda, ana misemo mingi ya kwenye khanga tu utelekelezaji sifuri zaidi atawaambia ni upepo tu.
 
WanaKigoma tulieni mpaka miguu yenu ijae funza na mtakapotembea kwa shida basi hapo mjisikie mpo Dubai, wakati ahadi inatolewa na Zitto alikuwa mpambe pembeni sasa ni wakati muafaka wa kumuuliza
 
JK msanii zile ahadi alikuwa anaropoka kama amepagawa! Hata sijui alikuwa anafikiria nini? Na hapo anatoka mbele anasema ametekeleza asilimia 80! Wajua wana siasa wanacheza na akili za watanzania vijijini! Too bad! Kweli ahadi zake na kuzurula kule! Hata apewe tena miaka 20 mingine hawezi!tapeli wa siasa
 
Back
Top Bottom