Kigoma: Majambazi watano wakiwa na silaha wavamia nyumba tatu na kumuua mfanyabiashara kwa risasi

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,075
4,111
Jeshi la Polisi la Mkoani Kigoma limethibitisha kuwa, Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamevamia nyumba tatu katika Kijiji cha Nyamidaho wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kumuua kwa kumpiga risasi Mfanyabiashara Daglas Kingunyi, na kupora fedha na bidhaa mbalimbali kwenye maduka mawili katika Kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishana Msaidizi wa Polisi, James Manyama amebainisha kuwa Mfanyabiashara huyo alifariki wakati akipelekwa hospitali na wanaendelea na oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao.

manyama.jpg

Kamishana Msaidizi wa Polisi, James Manyama​
 
Ili u deal na majambaz pande hizo
Police wawe na mixer jwtz
Majambaz huko wana roho mbaya
Unakuta wanatoka Rwanda na Burundi

Ova

Sio Rwanda na Burundi tu hadi Congo, kule bastola ya elfu hamsini unapata, SMG hadi elfu sabini unapata kutoka ng’ambo hasa unategemea nini?

Lakini pia walinzi wa kwanza ni wenyeji wa huko naona nao hawatoi ushirikiano wa kutosha
 
Polisi , JWTZ, usalama, uhamiaji wajitahidi kua na operation za mara kwa mara
 
Ili u deal na majambaz pande hizo
Police wawe na mixer jwtz
Majambaz huko wana roho mbaya
Unakuta wanatoka Rwanda na Burundi

Ova
Siyo tu wanatoka Nchi hizo mara Nyingi ni Makomandooo waliotoroka huko kwao kwa kesi za Kivitaa au wakimbizi ndani ya Kigoma.

Hiii hali ndiyo inafanya Mbuga zote za Mkoa wa Katavi na Kigoma Tembo wanaelekea kuisha maaana jamaaa wanajipigia wanavyotaka ili kupata meno ya tembo ni balaaaaa
 
Isije kuwa ni Red tabara hao.

Ngoja tufatilie maana kale kajamaa kakifanya mission huwa kanakwenda mbele mbele kwenye media kujisifu au kutuma machawa wake kujisifu
 
Ili u deal na majambaz pande hizo
Police wawe na mixer jwtz
Majambaz huko wana roho mbaya
Unakuta wanatoka Rwanda na Burundi

Ova
Hiko kijiji cha nyamidaho ni karibu na burundi...na miaka ya 2013-2015 walikua wanafanya matukio sana huko
 
Sio Rwanda na Burundi tu hadi Congo, kule bastola ya elfu hamsini unapata, SMG hadi elfu sabini unapata kutoka ng’ambo hasa unategemea nini? Lakini pia walinzi wa kwanza ni wenyeji wa huko naona nao hawatoi ushirikiano wa kutosha
Elfu 50 bastora?SMG 70? No no nooo...nakumbuka last time miaka ya early 2000s SMG zilirange kwenye laki 3-4 Burundi kwenyewe au kwenye Camp za wakimbizi.

So hapo kwa bei zako upo wrong.

Bastola ungepata kwa laki 2 mpk 7 inategemeana na aina
 
Hiko kijiji cha nyamidaho ni karibu na burundi...na miaka ya 2013-2015 walikua wanafanya matukio sana huko
Kuna wakati tushatoka kigoma Tulikuwa tunaelekea kagera kufika karibia nyakanazi tulishauriwa tusimame tusiendele na safari, tusubiri escort ya maskari kuvusha magari

Nlikuwa na mzee boss wangu alikuwa mtu wa kutoka papua guinea alikuwa mbishi akasema twende tu Hapo tuko na hardtop Alafu mtu mbili tu akaniambia tuwahi kwenda kabanga mine

tulichokutana nacho kama movie

Mpaka Leo hii mwili wangu una alama za risasi upajani na pemben mwa tumbo

Mijitu huko ina roho katili....

Ova
 
Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa Watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamevamia nyumba tatu katika Kijiji cha Nyamidaho wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kumuua kwa kumpiga risasi Mfanyabiashara Daglas Kingunyi na kupora fedha na bidhaa mbalimbali kwenye maduka mawili katika Kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishana Msaidizi wa Polisi, James Manyama amebainisha kuwa Mfanyabiashara huyo alifariki wakati akipelekwa hospitali na wanaendelea na oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao.

View attachment 2155672
Kamishana Msaidizi wa Polisi, James Manyama​
Hao majambazu wangeiba tu bila kumuua jamaa
 
Kuna wakati tushatoka kigoma Tulikuwa tunaelekea kagera kufika karibia nyakanazi tulishauriwa tusimame tusiendele na safari, tusubiri escort ya maskari kuvusha magari
Nlikuwa na mzee boss wangu alikuwa mtu wa kutoka papa guinea alikuwa mbishi akasema twende tu Hapo tuko na hardtop Alafu mtu mbili tu akaniambia tuwahi kwenda kabanga mine
Mamaeee tulichokutana nacho kama movie
Mpaka Leo hii mwili wangu una alama za risasi upajani na pemben mwa tumbo

Mijitu huko ina roho katili....

Ova
Pole Sana mkuu
Hivi ni kweli GT wahenga wanadai huko kigoma enzi hizo wakiwavamia wanawalazimisha kuimba mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.
 
Pole Sana mkuu
Hivi ni kweli GT wahenga wanadai huko kigoma enzi hizo wakiwavamia wanawalazimisha kuimba mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.
Hahaha hii kitu nlikutana nayo msitu mtungutu (mtukutu) dodoma

Enzi hizo barabara ya makutopora kuelekea aneti kondoa vumbi tu

Tulikuwa kwenye basi nakumbuka jina la basi Ilikuwa supersonic....

Sema mwenyeji wangu alishanipanga khs njia hiyo kuna utekaji so na mm kwa sababu nishakutana na matukio nkajipanga, nlichofanya siti nliyokalia nlipigilia hela Ila mfukoni nlibakiza hela kdg ya kuwazuga

Sasa mzee tulipopita pale izava tumeingia kwenye limsitu nkaona Land rover imetupita ikasimama kwa mbele basi likasimamishwa tukashushwa pigwa sachi

Huku unaulizwa maswali unaenda wapi mm nkajibu kusalimia ndg mfukoni wakanipukutisha 60000 jamaa wako faster na muda sasa wakikuta Huna kitu balaa

Kuna dada mmj alibishana nao alipigwa na kitako cha bundk mdomoni yaani ni noma

Ebwana mwishoww tulimbishwa kupiga vigeregere

Baada ya utekaji kufanyika sana huko ndk kukawekwaga police barrier

Haya mambo ombea tu yasikukute
Sema lazima ujue jinsi ya kukabiliana na situation hizi

Sema tulipigishwa vigeregere

Ova
 
Back
Top Bottom