Kigoma: Mahakama yatengua udiwani wa Ezekiel Mshindo kwa sababu za Uraia

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,183
4,185
Uamuzi wa Mahakama hiyo ulitolewa Juni 28, mwaka huu, mbele ya Jaji Athumani Matuma baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili.

“Kama ripoti ya uhamiaji inasema mlalamikaji si raia na ripoti hiyo haijapingwa basi hakuna haja ya kutohalalisha au kuharibu uamuzi wa mlalamikiwa namba mbili na tatu kwa kutangaza kuwa kiti cha udiwani wazi kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu mlalamikaji hana sifa, si raia,” alisema.

Alisema Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa inasema mtu atakuwa na sifa katika uchaguzi huo ikiwa atatimiza vigezo vya kuwa raia wa Tanzania. Mshindo alikuwa Diwani CCM alikuwa akilalamika dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) , Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Ezekiel aliwasilisha maombi katika mahakama hiyo akipinga kuondolewa katika nafasi yake ya udiwani. Alikuwa diwani wa Kata ya Kagera - Nkanda, Kasulu na alishinda nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Inadaiwa Aprili 14, mwaka huu, Katibu Mkuu wa TAMISEMI alimfahamisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu kuwa mmoja wa madiwani katika kata yake moja si raia wa Tanzania na kumweleza kwamba aanze kufanya mchakato wa uchaguzi ili kujaza nafasi hiyo.

Wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, Diwani alikuwa akitetewa na mawakili Fortunatus Muhalila, Ignatus Kagashe na Hamisi Kamilomilo na wajibu maombi walikuwa wakiwakilishwa na Wakili wa Serikali Allan Shija akisaidiana na Emmanuel Ladislaus.

Akiwasilisha hoja za mlalamikaji, Wakili Muhalila alidai kuwa kitendo cha kuitisha uchaguzi mpya kimefanyika isivyo halali kwa kuwa mteja wake alishakuwa diwani.

Alidai malalamiko ya kuwa si raia wa Tanzania ni ya kisiasa na hata mteja wake alipohojiwa na Idara ya Uhamiaji hakukubali hoja ya kwamba si raia pia hakupewa nafasi ya kusikilizwa katika ngazi ya kitaifa ya uhamiaji.

Katika hoja nyingine, Wakili Muhalila alidai ripoti ya Uhamiaji inajichanganya kwa kuwa ilikuwa ikizungumzia Yohana Mshita na mlalamikaji kwa wakati mmoja.

Alidai katika mazingira hayo haionyeshi ni yupi hasa anayezungumziwa kati ya mlalamikaji na Yohana, kwa msingi huo hiyo ripoti haina sifa ya kuwa kielelezo kwa upande wa wanadaiwa kinachoweza kuzingatiwa wakati wa kutoa uamuzi.

Mshindo anadai kupitia wakili wake kuwa jukumu la Mwenyekiti wa Halmashauri kumfahamisha Waziri kuhusu suala hilo lakini si jukumu la waziri kufanya hivyo kama inavyoonekana katika hiyo kesi, anaomba mahakama ione mchakato wote uliofanywa katika shauri hilo ni batili.

Akiwakilisha wajibu maombi, Wakili Shija alidai Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa haiwezi kuachiwa hasa inapotokea mabadiliko ya diwani kupoteza sifa kama ilivyotokea kwa mlalamikaji baada ya kubainika kuwa si raia wa Tanzania wakati wa uchaguzi.

Kuhusu mkanganyiko wa majina ya kata ya Kagera Nkinda na Kagera Nkanda, alidai huko ni kuteleza kwa karamu na haina uhusiano na hoja iliyopo kwamba mlalamikaji si raia wa Tanzania.

Kuhusu hoja mlalamikaji kutopewa nafasi ya kusikilizwa na Idara ya Uhamiaji, wakili huyo alidai alipewa nafasi ya kusikilizwa katika ngazi ya wilaya, kama ilivyoonyeshwa katika ripoti na mlalamikaji alipowasilisha nyaraka za utetezi wa uraia wake.

HT: Nipashe
 

Abel2021

Member
May 8, 2021
41
35
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imetengua udiwani wa Ezekiel Mshindo kwa sababu hana sifa za kushika wadhifa huo kwani si raia wa Tanzania. Mshindo alikuwa Diwani wa Kata ya Kagera - Nkanda wilayani Kasulu, nafasi aliyoshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

HT: Nipashe
Chama gani?
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
18,299
32,112
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imetengua udiwani wa Ezekiel Mshindo kwa sababu hana sifa za kushika wadhifa huo kwani si raia wa Tanzania. Mshindo alikuwa Diwani wa Kata ya Kagera - Nkanda wilayani Kasulu, nafasi aliyoshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

HT: Nipashe
Chama Gani? Wagombea wote wa CCM walikuwa raia na hawakosei.
 

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,730
6,068
Mpaka Mahakama ndiyo ikang'amue kuwa hakuwa Raia, Uhamiaji wanafanya kazi gani?
Mwendazake aliharibu sana idara zote zilikuwa kwenye flight ✈️ mode; wasio na vigezo ikiwemo cha uraia walipenya bila kuhoji achana na kutokupngwa.
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
5,206
10,649
Kigoma unanweza kuta nusu ya wakazi sio raia
Sio kweli,Kigoma,Kagera, Tunduma,Mtambaswala Mtwara,wakazi wa hayo maeneo,wanafanana kila kitu na watu wanchi jirani,
Mijtu iliyozaliwa Kerege bagamoyo,Tandale haya hamuyajuhi,Lugha ya Kiha na Kirundi zinafanana,Kiwembwa Cha zambia na lugha ya wakazi wa Tunduma zinafanana,Kagera,Rwanda,Uganda,ukifika kyaka,au murongo boda,hata upande wa TZ watu wanaongea Kiganda,kinyankore,vitu vya kawaida,sasa unataka mkazi,mzaliwa wa Karagwe aongee kama Mzalamo wa Kerege,manzese?
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
20,141
43,121
Chama gani?
Swali gan hili unauliza Chief? Unauliza Jua linatokea upande gani wa dunia? You want to prove the obvious? Kabisa unauliza elements za interahamwe zinapatikana chama gani?
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom