Kigoma kujenga vizuizi kuzuia magari kugonga treni

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
KIGOMA.jpg

Kigoma. Katika kudhibiti ajali katika maeneo ambayo barabara imepishana na reli, Serikali imesema itahakikisha inajenga vizuizi katika maeneo hayo ili magari yawe yanasimama wakati treni ikipita.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Juni 8, 2018 na mkuu wa wilaya ya Kigoma, Samson Anga ikiwa zimepita siku mbili tangu kutokea ajali ya basi dogo lililogonga treni eneo la Gungu mkoani Kigoma na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine 35 kujeruhiwa.

“Haiwezekani watu wapoteze maisha kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya madereva. Tumechoka kuona hali hii ikiendelea na lazima tuchukue hatua kuokoa maisha ya binadamu wenzetu," amesema.

Amesema ujenzi wa vivuko utahusisha wakala wa barabara (Tanroads) na Shirika la Reli Tanzania(TRC) ambao wataratibu na kujenga vizuizi hivyo.

Maeneo ambayo reli imepishana na barabara mkoani Kigoma ni Kibirizi, Gungu, Nyamoli, Kazuramimba, Uvinza, Tubira na Malagalasi.

Chanzo: Mwananchi
 

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,376
2,000
Akili za viongozi/watendaji huwa hazifanyi kazi hadi litokee janga, hiyo reli iko hapo tangu mwaka 47, hawakuona haja ya kujenga vizuizi hadi leo baada ya princes Hamida kuigonga tren
 

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
5,392
2,000
Kweli hawakuliona Hilo miaka yote hiyo? "na ajabu utakuta hata Tabora, dodoma na morogoro hakuna vizuizi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom