Wiston Mogha
Senior Member
- Feb 13, 2014
- 149
- 96
Tuna taarifa ya kikao kilichofanyika leo kati ya DC, DAS, DSO, Afisa uchaguzi wilaya na afisa uchaguzi msaidizi wa wilaya kwa watendaji wa mtaa na kata katika manispaa ya kigoma ujiji walioitwa ofisi ya mkuu wa wilaya na kupewa maelekezo kwenda kukata wagombea wa vyama vya upinzani hasa ACT-Wazalendo na kwenda mbali zaidi kuwatisha kuwa mtendaji yeyote atakaethubutu kumtangaza mshindi alietokana na chama cha upinzani na ajira yake itakuwa imefika kikomo.
Kimsingi tunaona wazi kuwa maelekezo hayo yamewafanya watendaji kufanya kazi under pressure na kutotaka kabisa kutoa ushirikiano kwa wagombea wetu wanaopeleka rufaa zao baada ya kuondolewa kisanii kwenye mchakato mzima wa uchaguzi.
Tunajua kuwa watendaji wote walioacha mchakato huu kuwa huru wameambiwa kuwa watafukuzwa kazi.
Kikao hiki kimefanyika leo 06/11/2019 majira ya saa kumi mpaka saa kumi na moja jioni katika ofisi ya DC yenye kachumba kadogo na kuwabananisha watendaji wa kata na mitaa.
•Tunamkumbusha huyu DC na DSO kuwa mkoa wa kigoma una wenyewe na maendeleo ya mji wetu yataletwa na sisi wenyewe, hamuwezi kamwe kutupangia watu wa kutuongoza na kutupeleka kuifikia kigoma Tuitakayo. Tunawataka mfanye majukumu yenu kwa kufuata sheria na taratibu na sio kutuletea vitisho, kadhia wala manyanyaso.
•Na nyie watendaji wa kata na mitaa fateni sheria za uchaguzi msipokee vitisho kwani hapa ni kwenu na maendeleo ya mji huu yataletwa na sisi wenyewe acheni kabisa kupelekwa pelekwa kama mang'ombe...Akili za kuambiwa changanya na zako #Tusilaumiane
*Wiston Mogha*
#KeshoNyingi
06/11/2019