Kigoma: Boti (MV Nzeimana) iliyokuwa inatoka Sibwesa, Kigoma kwenda Ikola Katavi yapigwa dhoruba na kuzama ikiwa na Watu takribani 60, tisa wafariki

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,547
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma amesema boti inayobeba abira katika Ziwa Tanganyika ya MV Nzeimana inayofanya safari zake kati ya Sibweso na Ikola mkoani Katavi imezama

Amesema inasemekana majira ya leo saa kumi na moja na nusu ilianza safari kutoka Sibweso ila ilipofika eneo linaitwa Rasini ilipigwa na dhoruba kali na kupinduka

Kamanda huyo, Martin Ottieno ambaye ameeleza kuwa naelekea eneo la tukio, amesema kuwa inasemekana boti hiyo ilikuwa na watu wapatao 60

Amesema miili ya watu tisa waliofariki imeshaopolewa kwenye maji na kati yao Wanawake ni 7 na Wanaume ni 2 na watu 51 wameokolewa wakiwa hai. Amesema akifikia atatoa taarifa kamili
 
Poleni sana ikola, kwakweli maeneo hayo ni hatari sana, hakuna usafiri wa maana kwakweli

Nimepata taarifa wamefariki wengi zaidi ya hao.
 
Wameona kwenye magari watu wameshtukia sasa wamehamia kwenye vyombo vya majini. Kitu kama hiyo imetokea ziwa Victoria pia.
 
Poleni ndugu zangu ninakigugumizi cha usafiri wa majini hadi Leo Nina miaka zaidi ya 40 sijakanyaga kwa shangazi mitaa hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom