Kigoma: Baadhi ya wakazi wagoma kulipa huduma ya maji wakidai ni ya Mungu

ila Waha bhana ?!

sasa si ung'oe bomba nyumbani kwako usibir Mungu akuketee maji mpaka nyumbani kwako ?

acheni ujinga basi ...
 
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kigoma wameripotiwa kugoma kulipia huduma ya maji kwa kile wanachodai kuwa bidhaa hiyo inaletwa na Mungu.

Akizungumza katika mkutano wa nusu mwaka wa Wakala wa Usabazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kigoma, Meneja wa wakala huo wilayani humo Mhandisi Leo Respicius amesema, tabia hiyo imechangia kupungua kwa mapato yanayotokana na huduma ya maji katika baadhi ya vijiji.

Kufuatia suala hilo, mkuu wa wilaya ya Kigoma, Ester Mahawe ameitaka RUWASA kushirikiana na viongozi wa vijiji wilayani humo, ili kuwaelimisha zaidi Wananchi juu ya umuhimu wa kulipia huduma ya maji.

Baadhi ya vijiji wilayani Kigoma ambapo wakazi wake wengi wametajwa kugoma kulipia huduma ya maji kwa madai kuwa bidhaa hiyo inaletwa na Mungu ni Mkongoro, Kaseke, Nyamoli na Kidahawe.
Waha ni wabishi sana
 
Waha na ubishi pro max,sishangai sana,wengi nimesoma nao.Wanaweza kubishia taarifa ya habari ya redio
 
Back
Top Bottom