Kigoma: Baadhi ya wakazi wagoma kulipa huduma ya maji wakidai ni ya Mungu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kigoma wameripotiwa kugoma kulipia huduma ya maji kwa kile wanachodai kuwa bidhaa hiyo inaletwa na Mungu.

Akizungumza katika mkutano wa nusu mwaka wa Wakala wa Usabazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kigoma, Meneja wa wakala huo wilayani humo Mhandisi Leo Respicius amesema, tabia hiyo imechangia kupungua kwa mapato yanayotokana na huduma ya maji katika baadhi ya vijiji.

Kufuatia suala hilo, mkuu wa wilaya ya Kigoma, Ester Mahawe ameitaka RUWASA kushirikiana na viongozi wa vijiji wilayani humo, ili kuwaelimisha zaidi Wananchi juu ya umuhimu wa kulipia huduma ya maji.

Baadhi ya vijiji wilayani Kigoma ambapo wakazi wake wengi wametajwa kugoma kulipia huduma ya maji kwa madai kuwa bidhaa hiyo inaletwa na Mungu ni Mkongoro, Kaseke, Nyamoli na Kidahawe.
 
Nafikiri wapo sawa, zaidi ni mamlaka inapaswa iwape elimu na ikiwezekana wawapeleke kwenye water treatment plant na waeleweshwe gharama za kuyatibu na kuwafikishia maji.

Hao watu wanahitaji elimu, na waambiwe wanachangia gharama na sio kulipia huduma
 
Hii nchi haiishi vituko. Sasa wanategemea gharama za kuyatibu zinatoka kwa nan kama wasipolipia wao? Ama wawaache wawe wanavuna ayo maji wenyewe na kuyatreat na kuyasambaza kwa gharama zao wenyewe ?
 
😬😬hata hivyo wasukuma ni wabishi kama wapo huko wamewaambukiza wenzao
Wasukuma kwa ubishi hawawafikii waha na warundi,hivi unamwonaje zito kabww kajamaa ni kabishi hako.

Mi nimewekeza huko wifi yako no Wa huko,huyu maza ni mbishi balaa,na ukioa huko hapo kwako ndo amefika hawarudigi kwao akishatoka huko,utamuulia hapo kwako.
 
Juzi kati nusura nipewe mke, kisa nimesaidia kulipa ada! Yaani huku ukitoa msaada wenzio ni wakarimu wanaweza kukukirimia hata mke wake.

Karibuni sana Nyakitonto kijiji cha kibiashara, kinakua balaa!
 
Wasukuma kwa ubishi hawawafikii waha na warundi,hivi unamwonaje zito kabww kajamaa ni kabishi hako.

Mi nimewekeza huko wifi yako no Wa huko,huyu maza ni mbishi balaa,na ukioa huko hapo kwako ndo amefika hawarudigi kwao akishatoka huko,utamuulia hapo kwako.
😀😀😀😀why hawataki kurudi kwao
 
Back
Top Bottom