ANGALIZO: Habari hii imekanushwa - News Alert: - Felix Mkosamali: Sina mpango wa kuhama chama cha NCCR Mageuzi
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Muhambwe Mkoani Kigoma kupitia chama Cha NCCR-Mageuzi Felix Francis Mkosamali ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa kile alichoeleza kuwa chama hicho kimemezwa na Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) hivyo kupoteza dira.Pia Mkosamali ameongeza kuwa vyama vya upinzani vimepoteza dira baada ya kukumbatia waliokuwa mafisadi wanaohamia kwenye vyama hivyo kutoka CCM.
Sababu nyingine aliyoitoa ndugu Mkosamali ni kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli kwenye vita dhidi ya ufisadi na kupigania na kulinda rasilimali za taifa.
Aidha Mkosamali amesema siku kadhaa zijazo atatangaza atakachojiunga nacho.