Kigoma: Ajali ya Hiace yaua watu 7 na kujeruhi 12, ni baada ya kupasuka tairi

Manosa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
4,513
2,000
Imetokea ajali mbaya Kigoma njia ya Uvinza Kijiji cha Mulela.

Mpaka sasa nimeshuhudia maiti saba.

Hiace imepasua tairi na kupinduka

Majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Maweni

Hiace ilikua imetoka Uvinza kwenda kigoma mjini

Kwa mujib wa mashuhud Hiace mbil zilikua zinakimbizana zote za kampun moja baada ya kutoka Mwamila kuelekea Kigoma mjini

Uwokozi unaendelea

Stay tuned


======

Kamanada wa Polisi Mkoani Kigoma Martin Ottieno ameiambia JamiiForums kwamba, Gari ya abiria namba T247 DMG Toyota Hiace inayofanya safari zake kati Kigoma na Uvinza, imepata ajali na kupinduka mara tatu baada ya tairi ya nyuma kupasuka muda wa saa kumi na mbili na robo jioni.

Ajali hii imesababisha vifo vya watu saba kati yao Wanaume ni wanne na Wanawake ni Watatu. Vilevile wapo Majeruhi 12 ambao Wanaume ni 8, Wanawake 2 na Watoto Wawili.

Majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Mkoa ya Maweni.
IMG_20190503_233248_732.jpg
 

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
4,125
2,000
Pole nyingi kwa waathirika wa ajali.

'Na tunawaombea matehemu warudi kwenye majukumu yao salama'.
 

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,303
2,000
Imetokea ajali mbaya Kigoma njia ya Uvinza Kijiji cha Mulela.

Mpaka sasa nimeshuhudia maiti saba.

Hiace imepasua tairi na kupinduka

Majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Maweni

Uwokozi unaendelea
Poleni sana Mkuu. Tafadhali hebu jazia nya kidogo taarifa, Hiance ilikuwa inatoka wapi kwenda wapi?
 

data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
23,470
2,000
Polisi hawapendi mripoti habari hizi...

We umesema 7. Wao watasema 1
 

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
6,467
2,000
Uwokozi- uokoaji!


Poleni sana! Ile njia mbovu sana, serikali nao wamewasahau sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom