Kigoma: Afisa bandari aliyetoroka akamatwa na kushtakiwa pamoja na wenzake 4 kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

KIGOMA 28/05/2021
AFISA BANDARI ALIYETOROKA AKAMATWA NA KUSHTAKIWA PAMOJA NA WENZAKE 4 KWA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – CP Salum Hamduni, tunapenda kuujulisha Umma kwamba leo Ijumaa Mei 28, 2021, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, tunamfikisha mahakamani aliyekuwa Mhasibu - Bandari ya Kigoma Bw. Madaraka Robert Madaraka kwa tuhuma za Ufujaji na Ubadhirifu, Kuisababisha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania hasara ya shilingi 619,278,260.52 pamoja na utakatishaji fedha.

Ikumbukwe kuwa mtuhumiwa huyu ndiye anayetuhumiwa kuongoza genge la kufanya ubadhirifu wa fedha katika kituo cha Bandari ya Kigoma wakati akiwa Mhasibu katika kituo hicho.

Uchunguzi wa TAKUKURU Makao Makuu ulibaini kwamba, mtuhumiwa huyu alitoroka kabla ya Ofisi yetu ya TAKUKURU kuanza uchunguzi mwezi Februari mwaka 2020. Hivyo basi tunapenda kuuarifu umma kuwa Ofisi yetu iliendelea kumtafuta mtuhumiwa huyu hadi ilipofanikiwa kumpata na hivi leo atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma kujibu mashtaka yanayomkabili.

Katika shauri hili, Mtuhumiwa Madaraka Robert Madaraka anaunganishwa na washtakiwa wengine 4 katika Shauri la uhujumu Uchumi Namba 05/2020 linaloendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma hivyo kufanya idadi ya washtakiwa katika shauri hilo kuwa watano (5); Washitakiwa wanne (4) wa awali walikuwa ni watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Kigoma ambao kwa sasa tayari wameshafukuzwa kazi kwa mujibu wa Sheria, na mmoja (1) ni Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni ya M/S Ntinyako Company Limited iliyokuwa ikipewa zabuni ya usambazaji wa vifaa vya ujenzi na miundombinu ya maji katika Ofisi ya Bandari Kigoma.

Majina ya washtakiwa wa awali wanne (4) katika kesi hiyo ni;
1. Eliya Stephano Ntinyako – Mkurugenzi wa Kampuni ya Ntinyako Company Limited
2. Morris Charles Mchindiuza - Aliyekuwa Meneja wa Bandari Kigoma
3. Herman Ndiboto Shimbe – Aliyekuwa Afisa Uhasibu TPA Kigoma
4. Lusubilo Anosisye Mwakyusa – Aliyekuwa Afisa Rasilimali watu TPA Kigoma.

Sambamba na kumuunganisha Madaraka Robert Madaraka katika Shauri hili, uchunguzi wa TAKUKURU Makao Makuu bado unaendelea kufanyika dhidi yake kwa tuhuma zingine za uhujumu uchumi na kuisababishia hasara Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Mara baada ya uchunguzi huo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake pamoja wengine walioshirikiana naye.

IMETOLEWA NA STEPHEN MAFIPA
MKUU WA TAKUKURU MKOA WA KIGOMA
 
Kumbe bado wanakamatwa?
Si walishangilia kifo cha JPM kwamba watapata furaha sasa .
 
Maisha haya bana sisi ambao tupo kwenye vimishahara vya laki sita tunatamani tufike huko japo kwenye mishahara ya kuanzia 1.5M na marupurupu na miposho ya kutosha na walioko huko bado hawatosheki na mishahara yao hiyoo.!

KWELI TUMBO HALITOSHIBA HADI SIKU LINAINGIA KABURINI.
 
Majina ya washtakiwa wa awali wanne (4) katika kesi hiyo ni;
1. Eliya Stephano Ntinyako – Mkurugenzi wa Kampuni ya Ntinyako Company Limited
2. Morris Charles Mchindiuza - Aliyekuwa Meneja wa Bandari Kigoma
3. Herman Ndiboto Shimbe – Aliyekuwa Afisa Uhasibu TPA Kigoma
4. Lusubilo Anosisye Mwakyusa – Aliyekuwa Afisa Rasilimali watu TPA Kigoma.

Sambamba na kumuunganisha Madaraka Robert Madaraka katika Shauri hili, uchunguzi wa TAKUKURU Makao Makuu bado unaendelea kufanyika dhidi yake kwa tuhuma zingine za uhujumu uchumi na kuisababishia hasara Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Mara baada ya uchunguzi huo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake pamoja wengine walioshirikiana naye.
Roho ngumu, hii ni kipindi cha Mwendazake, nafikiria tu hali ilivyokuwa kabla na inavyokuwa baada yake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom