Kigogo Wizara ya Miundombinu, Bw. Leopord Mjungi ajiua kwa kujipiga risasi

Aliyemtaja kasema na sababu? Naamini alikuwa waziri wakati huo
hakuwa waziri... kilikuwa kipindi ambacho yeye alihamishiwa wizara ya uvuvi

amesema chanzo cha huyu jamaa kujiuwa ni kwasababu wakubwa wao wa kazi waliwalazimisha yeye na mfugale kufanya mambo kinyume na taratibu za kazi na walipokataa

wakawawekea zengwe kazini huyu jamaa kwa hasira kwa kuona ananyanyasika kwa kusimamia haki na ethics za kazi yake aliamua kujimaliza..

wakubwa wapi rejea aliyekuwa raisi kipindi hicho..
aliyekuwa waziri wa wizara ya ujenzi/miundombinu/uchukuzi
na aliyekuwa mkurugenzi wa tanroads

magufuli alisema akiwa anampongeza mgugale kwa kusimama kwenye ethics za kazi yake ambapo ndipo kulipelekea mwenzake kujiuwa kwan alishindwa kuvumilia kunyanyasika na kuonewa na wakubwa kisa tu wamekataa kufanya mambo yasiendana na ethics za kazi zao....
 
Leopord mjungi alikuwa kiranja wangu pale Mazengo/Alliance secondary school bweni la Muungano(1976). Alikuwa kichwa sana alipata division 1 PGM. Alale pema peponi. Walaaniwe wote walosababisha ajiue, japo naye alifanya jambo baya sana kujiua.
 
Wandugu wenzangu wa Jambo, naomba kuwasalimia.....

Nimeona hii habari kwenye gazeti la Nipashe la jana na nimeona niweze kuwashirikisha... Kwa wale tuliofanya kazi kwenye sekta ya Miundombinu kama mimi kwa kweli nimeshtushwa sana na tukio hili na limeacha maswali mengi sana katika kichwa changu ukizingatia matatizo tuliyonayo hivi sasa katika sekta hiyo.

Mungu ailaze roho ya ndugu yetu pema peponi, Amina

Article ni hiyo hap chini:

Mkurugenzi Miundombinu ajimaliza kwa risasi
2007-11-18 10:48:23
Na Anna Nkinda wa Jeshi la Polisi

Mkurugenzi wa Kampuni ya Trunk Roads Tanzania, Bw. Leopord Mjungi (53) amejiua kwa kujipiga risasi kifuani.?Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi Ramadhani Mssika alisema kuwa, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, saa tisa alasiri katika kijiji cha Magata Katuranga wilani Muleba Mkoani humo.

Kamanda Mssika alisema, Bw. Mjungi ambaye alikuwa mfanyakazi wa Wizara ya Miundombinu, alikuwa kijijini kwao kuanzia ?Novemba 11 akitokea jijini Dar es Salaam, alijipiga risasi kwa bastola aina ya Browning Cal. No. 9mm Serial No. 245NW70768.

``Alikwenda nyumbani kwa bibi yake aitwaye Regina Kwebunaya (100) kwa ajili ya kumsalimia na baada ya kuwaaga ndugu zake ili aanze safari yake ya kurudi jijini ?Dar es Salaam, ndipo alipoingia chumbani kwake na kujipiga risasi,`` alisema Kamanda Mssika.?

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya polisi kufika eneo la tukio na kufanya uchunguzi, walikuta tiketi ya ndege iliyokuwa inaonyesha kuwa angesafiri siku hiyo ya tukio kwenda Dar es Salaam kupitia Mwanza.

Bw. Mssika alisema kuwa, Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio hilo.

SOURCE: Nipashe
Inabidi polisi wafanya uchunguzi wa kueleweka kuliko kusema tu kajiua.
Nini hasa sababu ya yeye kujiua?
inakuaje mtu anayejua taka akate tiket kwa lengo la kurudi dar?
Ni nani alikuwa ndani wakati anajiua?
Pia si kawaida kwa mtu anayetaka kujiua kujipiga risasi kifuani mara nyingi ni risasi ya kichwa ndiyo ina uhakika zaidi kuwa mhusika atakufa.
Unless kama alijipiga risasi bahati mbaya.
 
Dah I miss those old good times ministry of works hapa mfugale pale mjungi Kati magufuli kule nyamhanga hapa chamuriho. I'm proud to say I once worked with real people even if it was for a short period
Mbn inasemwa hawa jamaa walikua wazee wa 10% au nawe ulikua mhusika, vp yule mrema aliekua Tanroads mbn hujamtaja
 
Leopord mjungi alikuwa kiranja wangu pale Mazengo/Alliance secondary school bweni la Muungano(1976). Alikuwa kichwa sana alipata division 1 PGM. Alale pema peponi. Walaaniwe wote walosababisha ajiue, japo naye alifanya jambo baya sana kujiua.
Kama 1976 Daahh makadirio ya haraka Umezaliwa around 1957-1960 now unaelekea 60.. Shikamoo Babu..
 
hakuwa waziri... kilikuwa kipindi ambacho yeye alihamishiwa wizara ya uvuvi

amesema chanzo cha huyu jamaa kujiuwa ni kwasababu wakubwa wao wa kazi waliwalazimisha yeye na mfugale kufanya mambo kinyume na taratibu za kazi na walipokataa

wakawawekea zengwe kazini huyu jamaa kwa hasira kwa kuona ananyanyasika kwa kusimamia haki na ethics za kazi yake aliamua kujimaliza..

wakubwa wapi rejea aliyekuwa raisi kipindi hicho... aliyekuwa katibu mkuu wizara ya ujenzi/miundombinu/uchukuzi na
aliyekuwa waziri wa wizara ya ujenzi/miundombinu/uchukuzi
na aliyekuwa mkurugenzi wa tanroads

magufuli alisema akiwa anampongeza mgugale kwa kusimama kwenye ethics za kazi yake ambapo ndipo kulipelekea mwenzake kujiuwa kwan alishindwa kuvumilia kunyanyasika na kuonewa na wakubwa kisa tu wamekataa kufanya mambo yasiendana na ethics za kazi zao....
Ni kipindi waziri wa miundombinu akiwa mtemi Andrea Chenge, na waziri mkuu akiwa laigwanan Ngoyai Lowasa. Eng Mjungi alikataa kuwa bangusilo.
 
Back
Top Bottom