Kigogo Wizara ya Miundombinu, Bw. Leopord Mjungi ajiua kwa kujipiga risasi

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
Wandugu wenzangu wa Jambo, naomba kuwasalimia.....

Nimeona hii habari kwenye gazeti la Nipashe la jana na nimeona niweze kuwashirikisha... Kwa wale tuliofanya kazi kwenye sekta ya Miundombinu kama mimi kwa kweli nimeshtushwa sana na tukio hili na limeacha maswali mengi sana katika kichwa changu ukizingatia matatizo tuliyonayo hivi sasa katika sekta hiyo.

Mungu ailaze roho ya ndugu yetu pema peponi, Amina

Article ni hiyo hap chini:

Mkurugenzi Miundombinu ajimaliza kwa risasi
2007-11-18 10:48:23
Na Anna Nkinda wa Jeshi la Polisi


Mkurugenzi wa Kampuni ya Trunk Roads Tanzania, Bw. Leopord Mjungi (53) amejiua kwa kujipiga risasi kifuani.?Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi Ramadhani Mssika alisema kuwa, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, saa tisa alasiri katika kijiji cha Magata Katuranga wilani Muleba Mkoani humo.

Kamanda Mssika alisema, Bw. Mjungi ambaye alikuwa mfanyakazi wa Wizara ya Miundombinu, alikuwa kijijini kwao kuanzia ?Novemba 11 akitokea jijini Dar es Salaam, alijipiga risasi kwa bastola aina ya Browning Cal. No. 9mm Serial No. 245NW70768.

``Alikwenda nyumbani kwa bibi yake aitwaye Regina Kwebunaya (100) kwa ajili ya kumsalimia na baada ya kuwaaga ndugu zake ili aanze safari yake ya kurudi jijini ?Dar es Salaam, ndipo alipoingia chumbani kwake na kujipiga risasi,`` alisema Kamanda Mssika.?

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya polisi kufika eneo la tukio na kufanya uchunguzi, walikuta tiketi ya ndege iliyokuwa inaonyesha kuwa angesafiri siku hiyo ya tukio kwenda Dar es Salaam kupitia Mwanza.

Bw. Mssika alisema kuwa, Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio hilo.

SOURCE: Nipashe
 
Duuhhh

Tumepoteza "MASHINE" muhimu sana pale Wizarani. Amini usiamini aliyemfanya Magufuli ang'ae pale Wizarani ni huyu Mujungi aliyetutoka. Tumepoteza mtu makini sana pale miundombinu.

Pole kwa familia na pole kwa Taifa la Tanzania, Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina
 
Duuhhh

Tumepoteza "MASHINE" muhimu sana pale Wizarani. Amini usiamini aliyemfanya Magufuli ang'ae pale Wizarani ni huyu Mujungi aliyetutoka. Tumepoteza mtu makini sana pale miundombinu.

Pole kwa familia na pole kwa Taifa la Tanzania, Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina

sasa amejiua kwa sababu ipi? au ameuliwa na kutengenezwa mazingira haya?
 
guys natania tuu li chama letu tawala....as hii ni miaka yao ya shetani kila baya lazima liende kwao...
in the other hand its so sad kumpoteza binadamu mwenzetuu Mungu ailaze roho yake pema peponii
Amen
 
Huenda kajiua kwa sababu za kawaida kabisa, huenda ni migogoro ya kifamilia tu. Ukute jamaa alikuwa na matatizo na familia yake (wazazi), maana taarifa zinasema kuwa alijiua baada ya kutoka kuwatembelea wazazi wake kule kijijini. Nadhani tungesubiri majibu ya uchunguzi kabla ya kuendelea na 'conspiracy theories'
 
MKURUGENZI wa Trunk Roads Tanzania, Bw. Leopald Mjungi (53), amejiua kwa kujipiga risasi kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Bw. Abdallah Mssika, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 9.45 alasiri katika kijiji cha Magata, Katuranga, wilayani Muleba mkoani humo.

Kamanda Mssika alisema marehemu ambaye ni mfanyakazi wa Wizara ya Miundombinu, alikuwa kijijini kwao kuanzia Novemba 14 mwaka huu akitokea Dar es Salaam na alijipiga risasi kwa bastola aina ya Browning namba 245NW70768.

“Marehemu alikwenda nyumbani kwa nyanya yake aitwaye Regina Kwebunaya (100), kumsalimia na baada ya kuwaaga ndugu zake, ili aanze safari ya kurudi Dar es Salaam, aliingia chumbani mwake na kujipiga risasi,” alisema Kamanda Mssika.

Aidha, Kamanda alisema baada ya askari kufika eneo la tukio na kufanya upekuzi, walikuta tikiti ya ndege iliyokuwa ikionesha kuwa marehemu alitakiwa kuondoka juzi saa tisa alasiri kurudi Dar es Salaam kupitia Mwanza.

Kamanda Mssika alisema Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha kujiua kwa Bw. Mjungi, kwani hadi sasa sababu za kujiua kwake bado hazijajulikana.

Chanzo: Majira
Novemba 18, 2007
 
Hii kali, inaelekea jamaa alikuwa na mpango wa kujiua kawapunguzia gharama za kumsafirisha ndugu zake
 
Back
Top Bottom