Kigogo wa UVCCM afungwa miaka 36 kwa wizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo wa UVCCM afungwa miaka 36 kwa wizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Jul 26, 2011.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kigogo UVCCM jela miaka 36 [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 25 July 2011 21:10 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Joyce Joliga na Kwirinus Mapunda, Singea
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Ruvuma, imemhukumu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, John Komba, kutumikia kifungo cha miaka 36 jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh 80 milioni.

  Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Baptista Mhelela, alisema jana alipokuwa akisoma hukumu hiyo kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 24 kwamba, Benedict Ngwenya, alitenda kosa hilo la kuiibia Kampuni ya DAE Ltd.

  Kwa mujibu wa Hakimu Mhelela, Mahakama hiyo bila shaka yoyote, imeridhika na ushahidi huo na kwamba imemtia hatiani mshitakiwa Ngwenya ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mpepai katika Wilaya ya Mbinga.

  Alifafanua kwamba mshitakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa 13, lakini kosa moja kati ya hayo ambalo ni la kughushi kwa maandishi alishinda. Alisema ametiwa hatiani kwa makosa mengine 12 yaliyobaki.

  Awali, Mwanasheria wa Serikali, Mwegole Shabani, alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Ngwenya alitenda makosa hayo mwaka 2008 kwa nyakati tofauti akiwa anafanya kazi kama mhasibu katika kampuni hiyo ya DAE LtD.

  Shabani alisema mshitakiwa alizichukua fedha hizo kwa lengo la kwenda kugawa kwenye mitambo inayokoboa kahawa mbichi ambapo hata hivyo, hakuzifikisha sehemu husika.

  Alisema baada ya kutenda kosa hilo, aliacha kazi bila kukabidhi ofisi kwa mwajiri wake, jambo ambalo lilimfanya mwajiri huyo kumtilia shaka na kumtaka mkaguzi wa mahesabu wa ndani kufanya ukaguzi ndipo alipobaini upotevu wa fedha hizo.

  Source: Mwananchi


  Hivi kweli haki imetendeka au kuna kitu hapa!! Maana tumeona akina Liyumba ambao wameiba mabillion wakienda jela miaka 2 tu. Akina Mramba kesi zinabadilika. Sisemi kuwa huyu jamaa hakusitahili kufungwa ila naona miaka 36 kwa wizi wa million 80 ni too much!!

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Katibu wa mbunge john komba-mbinga amehukumiwa kifungo cha miaka 36 jela baada ya kuiba pesa sh 80m akiwa mhasibu wa kampuni ya DAE LTD.pesa hizo zilikua zitumike kununua pembejeo za kilimo wilayani mbinga.AMA KWELI MAGAMBA WOTE MAJIZI.source gazeti mwananchi leo
   
 3. L

  Lua JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa vbaka hawa hukumu inatoka ila kwa mafisadi papa ahaaaaaaa. tena ela ya likizo wanapewa.
   
 4. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  haya bwana magamba
  anyway kuna uchaguzi hapo ni kwenda kumwaga sumu tu
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mwizi wa milion 80 miaka 36 lakini mwizi wa zaidi ya bilion 40 anakula kuku majuu
   
 6. zululima

  zululima Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmhhhhhhh, haya, japo wizi kwa magamba ni minor issue lakini mie bado mgeni mods anani observe.
   
 7. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  washabiki na wakereketwa wa ccm wengi ni wezi, corrupt, mafisadi, wakwepa kodi, majambazi nk nk..........
   
 8. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wapi mama faiza foxy! atajifanya wla hakuiona hii.... Magamba bana!
   
 9. kizomanizo

  kizomanizo Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wakati tukiwa chuo na huyo mtajwa(Ngwenya) alikuwa mtu anayeipenda sana CCM na maovu+mema alikuwa anayasema, hata katika vikao vya UVCCM aliwahi kuzunguza kuhusu watu kutoshabikia pesa. Yu wapi huyo leo hii? Huyu jamaa alikua mtu wa vituko japo 'straight' kwa kufikiri sasa sijui kama angeweza kupiga hela mbuzi kama hiyo(Najua ni milioni 80). Mambo huenda yakibadilika... #Weirdo
   
 10. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu Sheria Zetu zinawalinda MAFISADI PAPA lakini wewe fisad dagaa haaa sheria inakunyongea kati, Jairo live barua inasomwa bungeni Luhanjo toka IKULU anakuambia kasimamishwa kupisha uchunguzi na atalipwa mshahara jamani hilo si liko wazi kuwa mkubwa wake ndio katoa Order angekuwa ni yeye kaaamua haki angekuwa Keko since last week

   
Loading...