Kigogo wa jeshi la polisi Nigeria auawa kwa kupigwa risasi

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
6,497
2,000
polisiiii.PNG

Meja Jenerali Hassan Ahmed

Watu wasiojulikana nchini Nigeria wamempiga risasi na kumuua mmoja wa vigogo wa jeshi la nchi hiyo, Meja Jenerali Hassan Ahmed.

Meja Jenerali Ahmed aliuawa usiku wa Alhamisi nje kidogo ya Abuja wakati gari lake liliposhambuliwa kwa risasi, akitokea jijini Lokoja kwenda Abuja, akiwa na familia yake.

Dereva aliyekuwa anaendesha alijeruhiwa na mwanamke mmoja aliyekuwepo kwenye gari hiyo anayetajwa kuwa dada wa meja huyo, Safina Ahmed alitekwa.

Jeshi la nchi hiyo limeyaelezea mauaji hayo ni ‘tukio la kusikitisha’, huku kuuawa kwake kukiongeza hofu ya usalama nchini humo.

Meja Jenerali Ahmed hivi karibuni aliteuliwa na mkuu wa majeshi ya nchi hiyo kuwa Mkurugenzi wa jeshi makao makuu. Haijajulikana mara moja kina nani hasa walio nyuma ya shambulio hilo na lina lengo gani hasa.

Kwa muda sasa nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na matukio ya kiusalama ambapo makundi mbali mbali yenye silaha yamekuwa yakiendesha mauaji na utekaji wakilengwa raia na wanajeshi. Kutokana na vitendo hivyo Mamlaka nchini humo zimekuwa zikitupiwa lawama kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
 
Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
1,919
2,000
Ile nchi siyo salama kabisa. 2019 nilibahatika kufika huko tulienda kwa mkutano. Vituko vitupu. Airport mpaka hotelin kwa escort ya polisi. Hotelin mkutanoni escort, nilikumbuka kwetu bongo. Uhuru haukuwepo
Sindio mnataka na hapa muanzishe vurugu
 
Prince Mhando

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
6,738
2,000
Ile nchi siyo salama kabisa. 2019 nilibahatika kufika huko tulienda kwa mkutano. Vituko vitupu. Airport mpaka hotelin kwa escort ya polisi. Hotelin mkutanoni escort, nilikumbuka kwetu bongo. Uhuru haukuwepo
ata kwetu yamewahi kutukuta hayo...umemsahau yule kigogo wa polisi alie uawa kule mwanza na vibaka...ama yule kigogo wa usalama alieuawa kule Arusha....? machafuko yapo kila sehemu...muda tu ndio huwa tofauti
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,582
2,000
Ile nchi siyo salama kabisa. 2019 nilibahatika kufika huko tulienda kwa mkutano. Vituko vitupu. Airport mpaka hotelin kwa escort ya polisi. Hotelin mkutanoni escort, nilikumbuka kwetu bongo. Uhuru haukuwepo
Ulipata muda wa kununua vitenge vya mama kwa escort ya police?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom