Kigogo wa jeshi la polisi ashushwa cheo na mwingine atumbuliwa kwa wizi wa magari

LTN USU WA MADOSO

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,194
2,000
mkuu wa jeshi la polisi nchi Ernest mangu amemshusha cheo mkuu wa kituo cha polisi Himo (ocs) mrakibu msaidizi wa polisi (ASP) zuhura suleman kwa kukamatwa na gari la wizi aina ya toyota rv4 lililoibiwa pia amehamishwa kituo kwa ajili ya kusubiri taratibu zingine toka mamlaka ya juu.

pia jeshi la polisi limemfukuza kazi moja kwa moja koplo federika shimila kwa kukamatwa na magari mawili ya wizi yaliyoibiwa dar esaalam jeshi hilo limedai kuwa watuhumiwa hao amekatwa baada ya kunasa mtandao wa majambazi dar na kuwataja kuwa askari hao nao pia wanashirikiana nao.

Chanzo. Mwananchi

======

Mwendelezo wa habari hii, unajadiliwa hapa JamiiForums kwenye hii thread=>Moshi: Vigogo wa Jeshi la Polisi wakamatwa na magari 3 ya wizi Himo
 
MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,160
2,000
HII SIYO SUPRISE KWANI USHIRIKIWA ASKARI KTK UHALIFU NI WA LONG TIME!!!!
 
Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,139
2,000
Natoka nje ya mada kidogo. Kozi za Polisi mwaka huu zimeshapangwa?
 
KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,527
2,000
Hapa inaonekana Jeshi la Polisi sio salama, askari wanashirikiana na mitandao ya ujambazi!!? IGP unatakiwa ufanye kazi ya ziada kusafisha hilo jeshi la sivyo litapoteza mvuto mbele ya wananchi.
 
ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Huyo koplo mamlaka zilizofanya akafukuzwa kazi sidhani kama zimefikiria madhara yatokanayo na kufukuzwa kazi kama suluhu ya kosa lililofanyika.Nimefikiria kwa sauti nikaona ni bora huyo koplo angepandishwa kizimbani na kama kuna uwezekano afungwe kwani akiwa uraiani uwezekano ni mkubwa wa yeye kushirikiana na baadhi ya raia kufanya uhalifu kwa mbinu mbadala.
 
ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Wakubwa wanalindana ama? Koplo anafukuzwa halafu bosi wake anashushwa cheo tu ili aendelee kutengeneza madili mengine!

Mimi mwenyewe nashangaa,hapo hao mapolisi wangetakiwa kufunguliwa mashtaka na sheria ichukue mkondo wake inavyopaswa ili kuwe na usawa,na sio mmoja mnamshusha cheo mwingine mnamfukuza halafu eti ndio mwisho.
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,649
2,000
Huyo koplo mamlaka zilizofanya akafukuzwa kazi sidhani kama zimefikiria madhara yatokanayo na kufukuzwa kazi kama suluhu ya kosa lililofanyika.Nimefikiria kwa sauti nikaona ni bora huyo koplo angepandishwa kizimbani na kama kuna uwezekano afungwe kwani akiwa uraiani uwezekano ni mkubwa wa yeye kushirikiana na baadhi ya raia kufanya uhalifu kwa mbinu mbadala.
Atalianika jeshi la polisi kweupeeee. Ule msemo wa kifo cha wengi harusi unahusika hapa!
 
ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,969
2,000
Atalianika jeshi la polisi kweupeeee. Ule msemo wa kifo cha wengi harusi unahusika hapa!
Ngoja tusubiri,nina uhakika huyo aliyefukuzwa kazi atawaanika wenzake na atabuni mbinu nyingine ya kupata magari mengine,siafiki kabisa suala la kumfukuza askari halafu abaki anaranadaranda mitaani.Hii ni aibu kwa waliofanya maamuzi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom