Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 56,591
- 30,433
Kigogo CELTEL anaswa na TAKUKURU
Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imemkamata Ofisa Usalama wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Celtel (T) Limited, Bw. Mohamed Gulamali, kwa kushawishi na kupokea rushwa ya sh. milioni tatu.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, ilisema tukio hilo lilitokea Julai 8 mwaka huu saa 10 jioni katika maeneo ya ofisi za Celtel, Kijitonyama, Kinondoni, Dar es Salaam.
Ilisema Juni 30 mwaka huu, taasisi hiyo ilipokea taarifa ya kushawishi hongo kutoka kwa mlalamikaji ambaye jina lake linahifadhiwa, ikidai kuwa mtuhumiwa alitaka mtoa taarifa amwongeze mkataba wa kulinda minara ambao ulikwisha muda wake siku hiyo.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, iwapo mkataba huo ungepitishwa basi ingebidi alipwe kila mwezi sh. milioni 4.5, ili malipo yao yawe yanaharakishwa kila mwezi.
Taarifa ilisema baada ya kupata taarifa hiyo, uchunguzi wa awali ulianza kwa nia ya kuthibitisha tuhuma hiyo na Julai 2 mwaka huu, mazungumzo yalifanyika baina ya mtoa taarifa na mtuhumiwa, Bw. Gulamali.
"Bw. Gulamali alisisitiza nia yake, kuwa bila kutimizwa kwa malipo hayo, mkataba hautasainiwa kwani kampuni zingine zinawania kazi hiyo. Aidha iwapo hongo itapokewa, atakuwa anaharakisha malipo yao kila mwezi," ilisema taarifa.
Iliongeza kuwa siku ya tukio, saa 8.30 mchana, mtoa taarifa alipokea ujumbe ukimtaka apeleke fedha, vinginevyo hatua za awali za mkataba hazitapitishwa na hivyo mkataba huo kufutwa.
"Mtoa taarifa alifika ofisini na uchunguzi uliamua kuweka mtego, ambapo mtuhumiwa alikamatwa saa 10 jioni akipokea hongo ya sh. milioni tatu katika ofisi za Celtel, Kijitonyama.
"Utambuzi wa fedha ulifanyika na mashahidi walioshuhudia walizitambua noti na baadaye mtuhumiwa aliletwa ofisini kwa mahojiano ili kukamilisha uchunguzi," ilisema taarifa na kuongeza kuwa baada ya uchunguzi, hatua zingine za kisheria zitafuata.