Kigogo wa CCM na mtumishi mstaafu wa serikali (W) Mwanga mbaroni kwa kuhujumu uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo wa CCM na mtumishi mstaafu wa serikali (W) Mwanga mbaroni kwa kuhujumu uchumi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MTENGETI, Jun 29, 2012.

 1. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Taasisi ya Kupambana na kuthibiti Rushwa Nchini TAKUKURU imemkamata aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Ndugu Mamboleo Tery na Aliyekuwa Afisa Elimu wilaya ya Mwanga Mama Phoibe Lyatuu kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Tsh 20,000,000/=.

  Mafisadi wote wawili hao walipata dhamana na kukwepa kwenda Kiruru baada ya kila mmoja kudhaminiwa kwa hati ya nyumba yenye thamani ya Tsh 45,000,000.

  Baada ya kupata dhamana Mwenyekiti huyo alitamba kuwa hawezi kuwa mbuzi wa kafara kwani Prof. Maghembe ndie kinara wa wanaoimaliza Wilaya ya Mwanga kwa Ufisadi. Alifanya hayo alituhumiwa nayo ili kuhakikisha Mbunge anapata ubunge. Amewaomba PCCB wamkamate pia Mh. Mbunge kwani ndie mhusika mkuu.

  My Take
  Hao waliokamatwa nadhani ni vidagaa tu kwani kuna mlolongo mrefu na fedha zilizoibwa Mwanga sio hizo tu. Mwanga haina tofauti kabisa na H/Mashauri ya Kishapu.
   
 2. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wenzentu nafuu huku jimbo- Usangu maarufu kwa ubeche jamaa keshastaafu lakini more than 500m kaiba wala hata kesi haipo mahakamani ameishia PCCB tu.
   
Loading...