Kigogo wa CCM ajiua

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Kigogo wa CCM ajiua

2008-02-25 17:08:55
Na Kiyao Hoza, Polisi Kati


Kiongozi mmoja wa Umoja wa Vijana wa CCM Jijini ameacha msiba mzito kwa wapendwa wake baada ya kujinyonga kwa shuka la kujifunikia hadi kujiua.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Pius Sheka amesema tukio hilo limetokea jana, mishale ya saa 1:30 usiku huko Mwananyamala Kisiwani.

Kamanda Sheka amemtaja kiongozi huyo wa Vijana CCM, ambaye ni Katibu wa Kata ya Mwananyamala kuwa ni Bw. Cyprian Likonoka, 35.

Amesema Bw. Likonoka alijinyonga kwa kutumia shuka alilolitundika katika kenchi, chumbani kwa mdogo wake aliyetajwa kwa jina la Albino Likokola, 25.

Amesema chanzo cha Bw. Likonoka kujinyonga hakijafahamika na polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Akasema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala.

Katika tukio jingine lililotokea katika barabara ya Bagamoyo eneo la Tegeta, karibu na bar iliyofahamika kwa jina la Zero, mwanaume mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki amekufa baada ya kujibamiza kwenye trela moja lililokuwa mbele yake.

Kaimu Kamanda Sheka amesema tukio hilo limetokea leo mishale ya saa 6:45 usiku, wakati mtu huyo, Thomas Makore, akitokea katika bar hiyo huku akiwa amelewa.

Amesema marehemu alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T 174 ASX, alilivaa trela lenye namba za usajili T 680 AGH iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara.

Amesema katika tukio hilo marehemu alijeruhiwa kichwani na kuchubuka usoni, na alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala.

Wakati huohuo, dereva wa gari yenye namba za usajili T 385 AFP aina ya Nissan Patrol, George Masanga, 32, amefariki dunia, baada ya gari yake kuacha njia na kupinduka mara tatu.

Kaimu Kamanda Sheka amesema tukio hilo limetokea leo mishale la 8:30 usiku, katika eneo la mataa ya Magomeni.

Amesema marehemu alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili, na maiti yake imehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo.

Katika tukio jingine, binti mmoja mkazi wa Ukonga Mazizini amenusurika kufa, baada ya jaribio lake la kutaka kujitoa uhai kugonga mwamba.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Masindoki Masindoki, amemtaja binti huyo kuwa ni Queen Insi, 23, aliyefanya jaribio hilo jana mishale ya saa 4:30 usiku.

Amesema binti huyo alibwia sumu ya panya kwa madai kuwa alikuwa na uvimbe tumboni ambao ulikuwa ukimsababishia maumivu makali.

Kamanda Masindoki amesema binti huyo amelazwa katika Hospitali ya Amana na hali yake inaendelea vizuri, akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

SOURCE: Alasiri
 
kah!! mi nkajua kigogo, kigoooogo, kumbe katibu kata, anyway, nature's call, poleni mlofiwa!
 
Nadhani hii yapaswa kuondoka hapa ilipo iende huko kwa udaku.Kiongozi wa Kata naye anaitwa Kigogo ? Upuuzi huu
 
Mwandishi amekurupuka kwa kutumia neno kigogo wakati muhusika kumbe sio kigogo ni mkereketwa tu wa ccm,mwandishi akanushe taarifa yake kwa vyombo vya habari kwa kuta kuupotosha umma.
 
Mwandishi amekurupuka kwa kutumia neno kigogo wakati muhusika kumbe sio kigogo ni mkereketwa tu wa ccm,mwandishi akanushe taarifa yake kwa vyombo vya habari kwa kuta kuupotosha umma.

Aina hii ya waandishi wanakubalika sana na jamaa wapendao kuuza magazeti yao na wanao watumia .Aina hii ya waandishi si wachambuzi hata mara moja ni kukurupuka ni sehemu ya maisha yao .Wako wengi katika Nchi hii na hawa hutumika vibaya kuandika maswala ya taifa na wao kugeuza kama mpira wa miguu .Hawa hawa ndiyo huwagawa Watanzania na kuandika habari za siasa kishabiki bila kujua kwamba impact mbaya nia maafa kwa Taifa .
 
Mwandishi amekurupuka kwa kutumia neno kigogo wakati muhusika kumbe sio kigogo ni mkereketwa tu wa ccm,mwandishi akanushe taarifa yake kwa vyombo vya habari kwa kutaka kuupotosha umma.
 
Naomba kueleweshwa maana ya kigogo. Nadhani headline ingekua "Kigogo wa kata wa CCM ajiua".
Anyway, pole kwa wafiwa.
 
Lunyungu...Kigogo wa CCM yoyote anakuwa Kigogo..umesahau ule Ujumbe kutoka Serikali wa MZee ES?...ES kaulizwa hao viongozi wa serikali aloongea nao kina nani?..kwani hata Kiongozi wa serikali ya Mtaa pia ni kiongozi wa serikali....Mjadala umefungwa na Invisible.
 
aaaargh!
Hii habari iko 'shocking' kupita kiasi, utadhani aliyefariki ni kigogo kweli kumbe ni kajitawi tu. Jamani hii habari ingetafutiwa kichwa cha habari kingine, kama vile 'Kada wa Sisiemu afariki'! Ndio yale yale ya akina Uwazi, Kasheshe, Risasi na Alasiri! Utakuta kichwa cha habari kikuuubwa! "WAZIRI AFUMANIWA", ukija kusoma ndani unakuta wameandika "Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Waziri mkazi wa Kigogo amefumaniwa......."
Poleni sana wanasisiemu.
 
Lunyungu...Kigogo wa CCM yoyote anakuwa Kigogo..umesahau ule Ujumbe kutoka Serikali wa MZee ES?...ES kaulizwa hao viongozi wa serikali aloongea nao kina nani?..kwani hata Kiongozi wa serikali ya Mtaa pia ni kiongozi wa serikali....Mjadala umefungwa na Invisible.

Mkuu Chuma,

Heshima mbele mkuu, ninaamini kuwa wewe ni mtu mzima kama mimi, sikuongea na mtu isipokuwa nilipewa amri, na walionipa ujumbe jana usiku walinifahamisha kuwa wameuona ujumbe na wameridhika na topic,

Serikali sio kigogo, kigogo hawezi kukanusha maana ni jina lisilokuwa na mtu, lakini serikali huwa ni moja na ina jina na by now ingekuwa imeshakanusha kuwa haihusiki na ujumbe wangu, au mimi ningekuwa matatani, maana kama haihusiki na ule ujumbe basi kwangu ni crime against serikali, na ninaweza kuwa prosecuted at anytime,

aliyeuliza swali lako ni kijana mmoja "mwenye akili sana" na majina mengi sana, in private anasema one thing, halafu hapa public anasema another, Invisible sio mjinga au mkurupukaji, ndio maana hana mawazo kama yako na mjumbe wako, na ndio kilicho muhimu sana, maana anaelewa "kama sio" nisingemruka na kuweka hapa, maneno kama yako katika siasa za public kama hizi ni ya kawaida, maana kwa muoga huenda kicheko......, ninaomba niseme kuwa sikuchagua kuwa what I am in life, na kabla ya kuuweka ule ujumbe I had to make a choice ya kuwaogopa watu kama wewe na kunyamaza, au kuwakabili kwa the good of wengi at large nafikiri unaelewa nililochagua, na sina tatizo kuishi na watu kama wewe na masatu, ambao moto ulipowaka hatukuwaona, na hatutakuja kuwaona, mpaka mambo yakiwa shwari tu!

Serikali sio kigogo mkuu, na tutaendelea kukata ishus hapa, pia tukiendelea kulindana our backs kwa wanaohusika, maana kama nilivyosema tutaendelea kumuamini Mungu, na kufunga milango ya magari yetu na funguo.

Ahsante Mkuu Chuma!
 
ES,

Kuna wakati mwingine inatakiwa unyamaze tu, hasa ukiona mtu anaenda personal bila sababu ya msingi.

Asante
 
Kata ni sehemu kubwa, (inatakiwa iwe na shule za msingi, sekondari na mungu akijalia kuwa na chuo chake).Katika anga zake huko Mwananyamala ni kigogo.

Pumzika kwa amani, matumaini yangu hakujiua kwa sababu ya kujihisi!
 
Wandugu, pamoja na ukweli kwamba huyu bwana aliyepoteza maisha si kigogo, kwa maana halisi ya "Ukigogo" hatuna budi kumuomba mwenyezi mungu aipumzishe mahali pema peponi roho ya huyu marehemu. Poleni wafiwa wote kwa msiba huu.
 
Back
Top Bottom