Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 229
Habari iliyohusisha familia ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, imeibua utata mkubwa baada ya kuibuka kwa vitisho vilivyosababisha kuzuiwa kuchapwa kwa gazeti la Raia Mwema toleo lililopita Namba 161 katika mazingira ya kutatanisha; huku habari hiyo hiyo ikikanushwa kwenye gazeti jingine hata kabla haijatoka.
Utata huo ulisababisha uongozi wa Imprint iliyopo chini ya kampuni ya Jamana Printers kusitisha ghafla kuendelea kuchapwa kwa gazeti la Raia Mwema ikiwa tayari limeshachapwa nakala 10,000 katika mazingira yaliyoonyesha kuwapo shinikizo zito kutoka kwa kigogo mmoja aliye karibu na mwanasiasa huyo kutaka habari inayomhusu Lowassa iondolewe ndipo gazeti lichapwe.
Raia Mwema ambalo lina makubaliano maalum na wachapaji hao lilistushwa na uamuzi huo wa ghafla wa wachapaji hao hasa baada ya uamuzi huo kuambatana na hali ya woga mkubwa uliotawala wafanyakazi wa kiwanda hicho usiku wa Jumanne ya wiki iliyopita
..kutokana na amri hiyo wachapaji, wafanyakazi wote wa Raia Mwema na watu wengine wote waliokuwamo kiwandani wakati huo waliamriwa kutoka eneo la uchapaji na kupekuliwa kuhakikisha hawabebi hata nakala moja ya gazeti hilo.
Habari zinasema kuwa nakala 10,000 ambazo tayari zilishachapwa ziliharibiwa chini ya uangalizi mkali wa maofisa wa kiwanda hicho ili kuhakikisha kuwa haziingii kwenye soko, na hivyo habari hiyo kusomwa na wananchi.
Hata hivyo, wakati uongozi wa Raia Mwema ukihangaika kutafuta mahali pengine pa kuchapa, ilibainika kwamba kigogo huyo pamoja na Mbunge mmoja walikuwa tayari na nakala ya gazeti hilo na ilidhihirika siku iliyofuata baada ya gazeti la Mtanzania lenye uhusiano wa karibu na kigogo huyo kuchapisha habari iliyokanusha habari hizo kabla hata ya habari husika kuchapishwa
Habari zaidi katika Raia Mwema ya leo.