Ijabu Issa
Member
- Apr 29, 2008
- 56
- 19
"KULIKONI, Jumatano 4, 2008
Na Gordon Kalulunga, Mbeya
Shehena kubwa ya pembe za ndovu imekamatwa mkoani Iringa ikisafirishwa kutoka mkoani Mbeya kupelekwa Dar es Salaam ili ipelekwe nje ya nchi.
Tukio hilo limetokea mkoani humo usiku wa kuamkia jana wakati wa harakati za kutorosha pembe hizo zilizokuwa zimebebwa kwenye gari kutoka Wilaya ya Mbarali, Mbeya ambako imeelezwa kuwa ndiko yaliko maficho ya nyara nyingi za Serikali zinazoibwa hapa nchini.
Taarifa za uchunguzi zimebaini kwamba nyara hizo ni mali ya kiongozi mmoja mwandamizi wa Chama Cha Mapinduzi ambaye anadaiwa kuifanya biashara hiyo kwa muda mrefu akishirikiana na viongozi kadhaa wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wengine kutoka katika taasisi nyeti za serikali.
Akizungumza kwa njia ya simu na KULIKONI, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi, alikiri kukamatwa kwa nyara hizo usiku wa kuamkia jana baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Kamanda Nyombi alipoombwa taarifa zaidi juu ya kukamatwa kwa watu hao alisema angelizitoa baadaye baada ya kuzihesabu na kujua nani mmiliki wa nyara hizo.
Aidha, habari kutoka serikalini zimesema kuwa kiongozi huyo mwandamizi wa CCM anatumiwa kama chambo na 'wakubwa' na kwamba mtandao wao ni mkubwa.
Kiongozi mmoja kutoka katika Wizara ya Maliasili na Utalii Dar es Salaam aliyekataa kutajwa jina lake gazetini alisema kwamba mtandao huo ni hatari na huenda ndio uliohusika kuwaua maofisa wa wanyamapori katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa pembe hizo za ndovu kabla ya kusafirishwa zilitunzwa eneo la Lujewa, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya ambako imebainika kuwa ndiko mahala pa siri kutunza nyara za serikali kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Imebainika kuwa kati ya wanaoshikiliwa ni mdogo wa kigogo wa CCM mkoani Mbeya ambaye alimpigia kaka yake simu na baadaye kigogo huyo alikwenda mkoani Iringa akiwa na kitita cha zaidi ya milioni 50 akitaka kutoa rushwa kwa watendaji wa Jeshi la Polisi kabla ya suala hilo halijafahamika kwa wanahabari.
Sanjari na hayo, KULIKONI limeelezwa kuwa kuna vibali vya kampuni za uwindaji vilivyotolewa na wizara husikakatika kampuni zenye utata mkubwa katika usajili na utendaji wake.
Kufuatia tukio hilo wadau mbalimbali mkoani hapa walioongea na gazeti hili wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa haraka madarakani wale wote waliotajwa na wanaoendelea kutajwa kuhusika katika kuhujumu maliasili nchini".
Nilikuwa Zanzibar ambako kutokana na matatizo ya umeme hata magazeti hatusomi. Nimeingia Dar leo na kuona gazeti hili la KULIKONI, nikaona vema habari hii ipate busara za wanaJF. Ijabu