Kigogo atuhumiwa kuiba vipuri vya gari la serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo atuhumiwa kuiba vipuri vya gari la serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jamadari, Apr 28, 2010.

 1. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  28th April 2010

  Ofisa mwandamizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), anatuhumiwa kubadili vipuri vya gari la serikali na kuvipachika kwenye gari lake.
  Hatu hiyo imefuatia kigogo mwingine wa wakala huo kudaiwa kutia serikali hasara ya jumla ya sh 2.2 bilioni.
  Tukio hilo limetokea siku chache baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutoa tuhuma za ufisadi kwa wakala huo ikiwa ni pamoja na magari mengi ya serikali kutumiwa kama miradi binafsi kwa kupelekwa gereji binafsi.
  Jalada hilo la kesi linalomhusu kigogo huyo lipo katika kituo cha polisi Buguruni na kwamba gari hilo lipo katika karakana ya Vingunguti.
  Kwa mujibu wa taarifa za jalada hilo ofisa huyo alikamatwa kwa tuhuma za wizi ambazo pia zinahusisha matumizi mabaya ya madaraka na baadaye aliachiwa kwa dhamana.
  Kumbukumbu hizo za kipolisi zimetaja gari hilo la serikali lililoibwa vipuri lilikuwa katika karakana hiyo.
  Miongoni mwa vipuri hivyo vilivyoibwa ni pamoja na kiwashio cha gari maarufu kama 'Stata', 'Propelashafti' na 'wepa'.
  Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtuhumiwa anatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati wowote.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faostine Shilogile, hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. b

  bwanashamba Senior Member

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du hatari tupu jamaa kaiba nini eti vipuri
  vya gari uyo jamaa atakua kabadili vitu vingi sana inabi
  di ilo gari walichunguze vizuri kuanzia matairi mpaka jeki
  yake na wheel spaner
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndogo
  jirani yangu mmoja alibadili vipuri vya cruser ya kampuni mpaka ikawekwa juu ya mawe. mwaka mmoja baadaye gari ikapigwa mnada akainunua mil2! akarudishia vipuri na kuanza kutambaa nayo mtaani! tena mali ya uma......!....wanafaa kunyongwa.
   
Loading...