Serikali: Siku za Kigogo wa Twitter zinahesabika na hana siku nyingi

super black Boy

Senior Member
Oct 15, 2019
135
169
Nimepita kwenye social media moja nimekuta huyu jamaa anayeitwa Kigogo anatafutwa na waziri Kangi Lugola.

Jamaa amefanya tukio gani hilo la balaa mpaka amemkuna mheshimiwa waziri?

---
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amesema kuwa hivi karibuni Jeshi la Polisi litamtia nguvuni mtu anayejiita kigogo kupitia ukurasa wa Twitter.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 2, 2019 katika mkutano na wanahabari wakati akitoa tathimini ya hali ya usalama hapa nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo amesema kuwa muda si mrefu polisi watamtia nguvuni mtu huyo.

"Kalenda inazo tarehe, utahesabu mwezi mfupi na mrefu, nataka niwaambie kwa kifupi siku za huyo Kigogo zinahesabika na hana siku nyingi", amesema Waziri Lugola.
 
nimepita kwenye social media moja nimekuta huyu jamaa anayeitwa Kigogo anatafutwa na waziri kangi luoga....jamaa amefanya tukio gani hilo isee LA balaa mpaka amemkuna mweheshimiwa waziri??
picha hii ya ushahidi
Screenshot_2019-11-02-16-59-59.jpeg
 
LUOGA/LUGOLA.
KIGOGO mtego aliotegewa ni ule wa Kuumwa kwa Rais na Kifo.
Pale ndipo alitegwa na amejulikana pale.
CANARY TRAP strategy ilifanya kazi na hana muda mrefu...

Ila serikali ya Tanzania bado imelala sana, ingebidi itangaze dau waziwazi kama milioni 250 kwa mtu atakaye fanikisha kufanikisha kutoa habari zitakazoweza kumpata kigogo na hakika hata wiki haitaisha anakamatwa mapema...

Hawa washauri wa serikali sijui huwa wanawaza nini?? vichwa vyao viko tupu 100%, na hakika kuna watu wanamjua kigogo fika, sema hawawezi mchoma katika mamlaka husika burebure, hapa serikali iingie BOT ichote fedha iweke mezani tuone kama huyo kigogo atachukua round...

Mbinu za kutumia wadada zilikuwa za zama hizo miaka ya 80 (kwa hii mbinu ni ngumu kumkamata kigogo maana ni mjanja kwelikweli), miaka ya hivi karibuni ni fedha tu inaongea.

Hawaoni wenzao Marekani wanachofanya kwa magaidi wanatangaza dau kubwa, waarabu uvumilivu unawashida wanaishia kuwachoa magaidi waliotikisa dunia...
 
Watu wana hints nyingi tu zinazoweza pelekea jamaa kupatikana sema ndio hivyo mikono mitupu hailambwi, serikali itangaze tu hapo dau mezani watu wamwage taarifa
kigogo kwa mawazo yangu sio mtu 1 ni kundi la watu (tena wataalamu sana) kuna siku niliona akisema 'walimdukua wakachemka" unaweza pata picha jamaa ni wa moto kiasi gani?

hii kudanganyana sijui mtego wa kuumwa maggu sijui nini ni porojo
 
kigogo kwa mawazo yangu sio mtu 1 ni kundi la watu (tena wataalamu sana) kuna siku niliona akisema 'walimdukua wakachemka" unaweza pata picha jamaa ni wa moto kiasi gani?

hii kudanganyana sijui mtego wa kuumwa maggu sijui nini ni porojo
Unawakumbuka Tanzagiza?? Kigogo ni mtu mmoja sio kikundi cha watu... Serikali iweke dau watu wamwage taarifa...
 
LUOGA/LUGOLA.
KIGOGO mtego aliotegewa ni ule wa Kuumwa kwa Rais na Kifo.
Pale ndipo alitegwa na amejulikana pale.

Sasa kama umeshasema kuwa katika huo Mtego ndiyo alijulikana inakuwaje wanatutangazia kuwa wanamtafuta? Si wakamchukue tu huko aliko ili tuamini kuwa wamemuweza? Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mange Kimambi na huyu Kigogo wanayehangaika nae 24/7 utadhani Yeye ndiyo anakwamisha Maendeleo ya Tanzania wakati ukweli ni kwamba matatizo ya Tanzania yalikuwepo tokea awamu ya Kwanza na yataendelea kuwepo hadi awamu zijazo labda mpaka Kiama kije au Yesu Kristo wa Nazareth aje Kutuchukua kama tulivyoaminishwa Kiimani.
 
Kuna watu walishamzyshia bodyguard wa rais yule bonge mweusi kuwa ndiye Kigogo2014.

Hapa watahisiwa Watu wengi sana ila ukweli utabaki pale pale kwamba kuna tatizo huko huko Ikulu hadi katika Taasisi Nyeti nchini kwani haiwezekani Jamaa akawa na taarifa mbichi na zenye uhakika kabisa.

Kama Kangi anataka Kumpata huyu Mtu aanze huko Ikulu na katika Taasisi ' Nyeti ' kwani atakuwepo huko huko au ni Mstaafu wao lakini anayewajua vyema na ambaye pengine kuna Vifaa ' Maalum ' vya Mawasiliano vilivyopo Ikulu na Kwingineko ambavyo vimewekwa na Yeye anavijua au atakuwa alienda nae Kozi na ameiva vilivyo.

Ukimsoma utagundaua ya kwamba ni Mtu mwenye Jeuri, Kiburi halafu anajiamini mno hali ambayo inanifanya niamini kuwa huyu Jamaa ni ' Jasusi Mbobezi ' na ' Hatari ' sana kuwahi kutokea nchini Tanzania.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom