KIGODA:Tofauti za Takwimu kwenye vitabu vya fedha ni SAHIHI

Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,220
52
Heshima Mbele wana JF

naomba kuwakilisha machache kuhusu tofauti hizi, sikuweza kuchukua zote maana nilikuwa natoa direct toka kwenye speech na mimi si mtaalamu wa maandishi so I was missing some points, kwa alie weza kuchukua yote anaweza kuwalisha.

Wakati michango juu ya bajeti ikiwa inamalizika leo Kigoda ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi jioni hii amewasilisha report ya kamati yake iliyo kaa siku hizi chache kufuatilia tofauti za takwimu zilizojitokeka kati ya vitabu vya bajeti ya fedha na hotuba ya waziri wa fedha bwana Mkullo ni SAHIHI na ni kwa ssb zifuatazo:
 • takwimu zote zilikuwa sahihi isipokuwa hazikutolewa ufafanuzi wa kutosha na kuwa leo hii mchana maelezo yakina kuhusu takwimu hizo zimetolewa kwa kamati hiyo.
 • Fedha za wahisani, za GBS na msahamaha wa IMF huwa zinazotolewa kama fedha za ndani (hapo sikuelewa nini maana ya fedha za ndani)
 • tofauti ta takwimu za waziri na vitabu zilisbbshwa na ile nyongezo iliokuja toka NMB na hazina ambazo na zenyewe zilikuwa zikisibiriwa na zilikuwa si za uhakuka (au zilicheleweshwa????)
 • By the tym bajeti inawasilishwa vitabu vingine vilikuwa tayari na vingine vilikuwa ndvinakamilishwa......... (duh...!! hii kali)
 • na sbb nyingine ni kuwa vitabu hivo vilikuwa vikitolewa kwa nyakati tofauti

haya.... akaja Zitto Kuwakilisha yao juu ya bajeti na report ya kamati kama kiongozi wa upindani

Zitto alisema yafuatayo:
 • Bajeti ta Mkulo ilikuwa na mapungufu/tofauti na ndio maana imeleta marekebisho ikuwa inadhihirisha kuwa kulikuwa na tofauti
 • kambi ya upinzani imeridhika na unyoofu wa serikalikw akuleta nyongeza ya marekebisha (akanyosha mkono kuonyesha kitabu cha bajeti chenye mapungufu na chenye marekebisho)
 • Kambi imegundua kuwa tofauti nhizo nyingi zimetokana nakupata makisio yaliyokuwa hayajawasilishwa nalo
 • kwa maelezo ya waziri wa fedha na kamati ya uchumi na fedhaimeonyesha kuwa kuna utegemezi mkubwa sana toka kwa kambi ya upinzani kitu ambacho wameshauri wawatumie

Mapendekezo toka kambi ya upinzani (niliyoweza kuyadaka)
 • iundwe bajeti comittee ambayo itakuwa inatengeneza bajeti na kushirikisha watu toka sehemu mbali mbali
 • na kamati hito iwe inapitia vitabu hivyo kabla ya kuwasilishwa bungeni
 • maamuzi yawe yanachapishwa yanio kuwa documented badala ya kutolewa na spika kama speech kwa aliji ya kuwa kama rejea
 • Kambi pia ina imani kabisa na watendaji wa serikali kuwataka baadhi ya wabunge kutowalaumu bisa sbb na badala yake kuwashauri na kuwasaidia

MUNGU IBARIKI KAMBI YA UPINZANI..........
MUNGU WABARIKI WATETEZI WA WATANZANIA WANYONGE HAPO BUNGENI........
 
na angekuwa hajaambiwa kama ni tofauti angeleta hayo maelezo sahihi? mkullo anapewa free ride hapa na kamati ya uchumi......alichofanya ni uzembe wa kutoa vitabu ambavyo vina takwimu zisizo sawa bila ya kuwaambia kabla wabunge kuwa wategemee vitabu vyengine ambavyo vinatengenezwa
 
SPEEECH NZIMA YA uPINZANI HII HAPA KAMA NILIVYOWEZA KUIPATA.


TAARIFA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI
MHE.HAMAD RASHID MOHAMED (MB) KUHUSU UTATA WA MAHESABU KATIKA KITABU CHA KWANZA CHA MAPATO YAANI “VOLUME 1 FINANCIAL STATEMENT AND REVENUE ESTIMATES” KWA MWAKA WA FEDHA WA FEDHA 2008/2009:
_____________________
UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,
Leo Asubuhi ulitoa mwongozo ulioombwa na Kambi ya Upinzani kuhusiana na kukiukwa kwa Kanuni ya 96(1) kuhusiana na matakwa ya kanuni hiyo kwamba “Waziri atapeleka kwa Katibu Makadirio ya Matumizi ya kawaida na ya maendeleo ya Serikali ya mwaka wa fedha unaohusika na nakala ya makadirio hayo itapelekwa na kumfikia kila mbunge angalau siku ishirini na moja kabla ya Mkutano ambao utashughulikia makadirio hayo” ulitoa mwongozo kuwa kuna utata katika kipengele hicho na kuagiza Kamati ya Fedha kupitia Kanuni hiyo na kupendekeza marekebisho stahiki.

Mheshimiwa Spika,
Kutokana na hoja zilizotolewa na Kambi ya Upinzani wakati wa majadala kuwa kuna mapungufu katika Takwimu za Kitabu cha Mapato, Serikali imewasilisha marekebisho ya Takwimu hizo.
Na kwa kuwa Takwimu za ziada zilizowasilishwa na Waziri leo asubuhi kwa njia ya “Addendum to Volume 1” kuonekana bado hazioani na Takwimu zilizoko kwenye Kitabu cha Hotuba ya Waziri uliagiza Kitabu hicho pamoja na Addendum kipitiwe na Kamati ya Fedha na Uchumi na baadaye Mwenyekiti wa Kamati husika na Kambi ya Upinzani tuitolee Taarifa ndani ya Bunge lako Tukufu.
Ninaomba kuchukua nafasi hii kutoa Taarifa kwa niaba ya Kambi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Spika,
Moja, Kambi ya Upinzani imefarijika na unyofu wa Serikali wa kukubali kuwa kulikuwa na mapungufu na makosa ya Kitakwimu katika Kitabu cha kwanza cha Makadirio ya Mapato (Volume 1 cha Financial Statement and Revenue Estimates), na hivyo kuwasilisha Bungeni Nyongeza ya Marekebisho hayo,(Addendum to Volume l ).

Mbili, Mheshimiwa Waziri ameieleza Kamati ya Fedha kuwa mapungufu hayo yametokana na serikali kupata makisio ya awali ambayo miongoni mwake hayakuwa yamethibitishwa na vyombo vinavyochangia mapato ya serikali (Kwa mfano, katika Benki Kuu Serikali ilikisia sh 11 Bilioni lakini baade ikathibitika kuwa ni sh 6 Bilioni). Kambi ya Upinzani imeridhika na maelezo hayo isipokuwa kwamba kwa miaka ijayo kazi hiyo iwe imekamilika kabla ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kuwasilishwa Bungeni, ili Bunge kwa niaba ya Wananchi liweze kupitisha jambo lililo na uhakika nalo.

Tatu, Baada ya maelezo ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Kambi ya Upinzani imebaini kwamba utegemezi wa Bajeti ya Maendeleo kwa Wahisani bado ni mkubwa mno kwa kiwango cha asilimia 97.5. Hii maana yake ni kwamba tunafanya uchumi wa kuchumia Tumbo (Stomach economy). Kambi ya Upinzani inasisitiza kwamba vyanzo vya Mapato ilivyovibainisha katika Bajeti mbadala vifuatiliwe kikamilifu ili kupunguza utegemezi huu.

Nne, Kambi ya Upinzani bado inasikitishwa na kitendo cha Serikali ya Muungano kutogawa gawio sahihi kutokana na faida ya Benki Kuu kwenda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mujibu wa Kumbukumbu za IMF, ilikuwa inamiliki asilimia 11.5 ya Hisa za Benki Kuu (BOT). Hivyo kugawa gawio kwa asilimia 4.5 ni kuipunja Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupata gawio sahihi kutokana na mtaji wake wakati Benki Kuu inaanza mwaka 1965 baada ya kuvunjwa kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki (East African Currency Board). Kambi ya Upinzani inaitaka Benki Kuu ya Tanzania igawe gawio kwa SMZ kwa mujibu wa hisa zake.

Mheshimiwa Spika,
Tano, Kambi ya Upinzani inasisitiza kuwa katika miaka ijayo Bunge lizingatie Ibara ya 138 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotaja kuwa hakuna Kodi au tozo yeyote inayoweza kutozwa bila idhini ya Bunge au kwa mujibu wa Sheria ya iliyotungwa na Bunge.

Sita, Kambi ya Upinzani inaona upo muhimu pia kufanya marekebisho ya kifungu cha 96 cha Kanuni ya Bunge Toleo la 2007 ili kulifanya Bunge kujadili na kupitisha mapendekezo ya Mapato na Matumizi kama yanavyowasilishwa na Vitabu vyote vinne vya Bajeti badala ya kupitisha matumizi tu kama ilivyozoeleka.

Saba, Kutokana na kasoro zilizoonekana hivi sasa ambapo Bunge limekuwa likijadili na kupitisha vitabu vya matumizi pekee na hata Kamati ya Fedha na Uchumi kutojadili Vitabu vya Mapato, na kutokana na uzoefu wa Mabunge mengine, Kambi ya Upinzani inapendekeza Bunge kuwa na Kamati ya Bajeti (Budget Committee) ambayo wajumbe wake watakuwa ni wenyeviti wa Kamati zote za kudumu za Bunge. Kamati ya Bajeti ndio itakuwa na jukumu la kupitia makadirio yote ya Mapato na Matumizi ya Serikali.

Nane, Kutokana na uzoefu tuliopata kutoka katika Mabunge mengine, Kambi ya Upinzani inapendekeza kuwa kwa vile Mheshimiwa Spika anatoa Maamuzi mengi ndani ya Bunge wakati umefika sasa wa Maamuzi hayo kuchapishwa rasmi katika umbo la Kitabu kurahisisha rejea ya Wabunge kuhusu mambo yaliyokwisha kuamuliwa ndani ya Bunge na wewe Mheshimiwa Spika, Naibu wako na Wenyeviti.

Mheshimiwa Spika,
Tisa, Kambi ya Upinzani Bungeni imefuatilia kwa karibu michango mbalimbali ya wabunge wakati wa wiki hii ya mjadala wa Bajeti.
Kambi imesikitishwa sana na mchango wa Mbunge mmoja jana aliposema kwamba Watendaji wa Serikali hawana nia njema na CCM na hivyo kumkwamisha Waziri wa Fedha.

Tabia ya sisi wanasiasa kupeleka lawama kwa watendaji kwa makosa ambayo sote twahusika ni tabia mbaya.
Kambi ya Upinzani ina imani kubwa na watendaji wa Serikali na tunawataka wafanye kazi zao bila upendeleo wa kiitikadi. Watendaji wote Serikalini, watanzania wazalendo endeleeni kuchapa kazi na mchukulie mchango wa Mheshimiwa Mbunge kama Waheshimiwa binafsi, Poleni sana.

Kumi, hatimaye naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza Wabunge wote wa Kambi ya Upinzani waliosimamia kidete
kurekebishwa kwa mapungufu haya na kuonyesha umuhimu wa Bunge kujadili Kitabu cha kwanza ili kutimiza matakwa ya Katiba, ibara ya 138.

Mheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani ina imani na watendaji wote wa Serikali hasa tukielewa mazingira wanayofanyia kazi hiyo, natumaini kabisa kwamba mapungufu yaliyotokea, yalifanywa kwa nia ya kumuanguasha Waziri, ila ni hali halisi ya matatizo ya kuwa na vianzio vya uhakika na vya kutosha matumizi yetu. Tunaomba waendelee kujenga uadilifu wao kwa Taifa.

Aidha, namshukuru Mhe. Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Mustapha Mkullo, na Manaibu wake wote wawili na watendaji wao kwa jitihada kubwa waliyafanya kwanza kuuthamini mchango wa Kambi ya Upinzani na kukubali kuufanyia kazi ushauri wetu. Hii ndiyo roho inayotakiwa ya Wabunge kuthamini mchango mzuri upande wowote unakotoka.

Mwisho, kutokana na ushirikiano na unyofu alioonyesha Mheshimiwa Waziri na Manaibu wake, Kambi ya Upinzani, kwa kuzingatia maslahi ya Taifa, inampa nafasi na hivyo kufikiria kupitisha au kutokupitisha Bajeti hii itategemea maelezo ya kuridhisha kuhusiana na maeneo yote tuliyohoji katika hotuba zetu mbalimbali.

Mheshimiwa Spika baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha.

/

...............................................................
Mhe. Hamad Rashid Mohamed (Mb)
KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
20.06.2008
 
Kigoda mkuu ,ila ya Kagoda nayo ipo tatizo ni kubwa sana haswa kuweza kuiscan na mimi sina scana hapa wakuu ila nina kurasa zaidi ya 800 zenye nyaraka zote hapa.Ntajitahidi
 
YA Kagoda itakuja muda sio mrefu kaeni makao wa kuchambua

Tunataka pia watuhumiwa waitwe bungeni kuhojiwa.
Hawa wabunge wako wengi tu...Ila naona sasa ni kama mama Killango peke yake.
WANANCHI WANATAKA HAKI...NA HAKI NI KUWAKAMATA MAFISADI.
Hizo siasa zimepitwa na wakati wapinzani...WANANCHI WANAJUWA NANI NI FISADI NA NYIE MNAREMBA WASIKAMATWE...Sasa naona mnadhani wananchi ni misukule.
 
Tunataka pia watuhumiwa waitwe bungeni kuhojiwa.
Hawa wabunge wako wengi tu...Ila naona sasa ni kama mama Killango peke yake.
WANANCHI WANATAKA HAKI...NA HAKI NI KUWAKAMATA MAFISADI.
Hizo siasa zimepitwa na wakati wapinzani...WANANCHI WANAJUWA NANI NI FISADI NA NYIE MNAREMBA WASIKAMATWE...Sasa naona mnadhani wananchi ni misukule.

Mtuhumiwa unamhoji bungeni! Mpeleke kortini au mahakamani!
 
Alichokifanya Mkulo ni zaidi ya aibu, hastahili kuendelea kuwepo serikalini, afadhali apumzishwe akafanye biashara zake
 
Ndio hivyo tena bajeti imepita kwa kishindo japo kwa masashihisha mbalimbali ,ila waziri kaahidi kuwa atayafanyia kazi mapendekezo ya upinzani na kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuinua uchumi wa taifa .
 
Kigoda amefanya haya ili kuokoa jahazi nakufuta aibu za waziri wao ama alikuwa na nia ya kusimamia issue ? Kama nia ni ussue na anadhani hapakuwa na makosa vitabu 2 tofauti why ?
 
Kwa maelezo ya Mh Kigoda vitabu vy abajeti vipo sahihi isipokuwa waziri wa fedha ( pengine na wataalamu wake wizarani) kashindwa ama ku defend au kuilewa kabisa bajeti yenyewe.

Im giving benefit of doubt Mh Kigoda udhoefu na elimu yake kwenye wizara ya fedha unamuwezasha kujua mambo kwa undani zaidi kuliko kilaza Mkulo.

Its time Mkulo to go....
 
Kwa maelezo ya Mh Kigoda vitabu vy abajeti vipo sahihi isipokuwa waziri wa fedha ( pengine na wataalamu wake wizarani) kashindwa ama ku defend au kuilewa kabisa bajeti yenyewe.

Im giving benefit of doubt Mh Kigoda udhoefu na elimu yake kwenye wizara ya fedha unamuwezasha kujua mambo kwa undani zaidi kuliko kilaza Mkulo.

Its time Mkulo to go....

Maneno yako yanamgusa pabaya JK.Yaani Mkullo aondoke ? Hawezi kuelewa.
 
Lunyungu,

He has to, kaondoka mamvi itakuwa Mkulo..

Masatu,

Hivi Mkullo anaweza kuondoka kabla hajalipia madeni yake binafsi? Inaonekana wanampa muda azipate za kutosha kulipia biashara zake zilizokuwa zinayumba kabla hajapewa ulaji rasmi.
 
Masatu,

Hivi Mkullo anaweza kuondoka kabla hajalipia madeni yake binafsi? Inaonekana wanampa muda azipate za kutosha kulipia biashara zake zilizokuwa zinayumba kabla hajapewa ulaji rasmi.

Umesema mameno mazito haya mkuu .Zipi hizo kama unaweza kutaja chache kati ya nyingi ?
 
Umesema mameno mazito haya mkuu .Zipi hizo kama unaweza kutaja chache kati ya nyingi ?

Nitakupa hints kidogo.. ili ufuatilie kwa kutumia mbinu zako za kijasusi. Kesho asubuhi, ukipita kwenye kila kibanda X cha muuza magazeti (pita pale kabla ya saa tatu asubuhi), na gazeti la tano toka kulia utakalonunua, soma uk wa pili kabla ya ukurasa wa michezo na utakuta dokezo la pili.

......
 
Nitakupa hints kidogo.. ili ufuatilie kwa kutumia mbinu zako za kijasusi. Kesho asubuhi, ukipita kwenye kila kibanda X cha muuza magazeti (pita pale kabla ya saa tatu asubuhi), na gazeti la tano toka kulia utakalonunua, soma uk wa pili kabla ya ukurasa wa michezo na utakuta dokezo la pili.

......
Duh...................!!
 
Nitakupa hints kidogo.. ili ufuatilie kwa kutumia mbinu zako za kijasusi. Kesho asubuhi, ukipita kwenye kila kibanda X cha muuza magazeti (pita pale kabla ya saa tatu asubuhi), na gazeti la tano toka kulia utakalonunua, soma uk wa pili kabla ya ukurasa wa michezo na utakuta dokezo la pili.

......
MwK, i like this one... btw, how many 'russian dolls' did you collect this time around?!;)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom