Kigoda cha Mwenge chaibiwa Arusha

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454

Attachments

  • 5_ace33.JPG
    5_ace33.JPG
    35.4 KB · Views: 513
KATIKA hali isiyo ya kawaida na inayoashiria uzembe katika
ulinzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, juzi kijana mmoja
mkazi wa eneo la Phillips katika Kata ya Sekei jijini Arusha,
Hamad Rashid (32) aliiba kiti (kigoda) cha kukalishia
Mwenge. Kuibwa kwa kiti hicho kumethibitishwa na Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas. Kiti hicho
hutumika kuwekea Mwenge wa Uhuru unapokuwa katika
mbio zake nchi mzima. Tukio la kuibwa na kisha kukamatwa kwa mtuhumiwa
lilitokea juzi saa 11 jioni Sanawari eneo la Mataa. Eneo hilo
ndilo lilipangwa kwa ajili ya mkesha wa Mwenge huo baada
ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya
msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo
katika Jiji la Arusha. Kufuatia tukio hilo, Kamanda Sabas aliyetafutwa kwa njia ya
simu kuzungumzia tukio hilo, alikiri kutokea kwa wizi huo
na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo alishakamatwa na
polisi waliokuwa wakiulinda Mwenge pamoja na kiti hicho. Alisema tukio hilo lilitokea wakati Mwenge huo pamoja na
wakimbizaji wake kitaifa, kimkoa na viongozi wengine
wakiwa katika harakati za kusoma salamu za utii kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya ratiba ya
utangazaji wa ratiba ya mkesha kutolewa. Alisema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,
alionekana kwa muda mrefu akiwa amesogelea gari
lililokuwa limebeba kiti hicho kilichoelezwa na kamanda
kuwa kilikuwa cha akiba. Alisema mara baada ya wizi kijana huyo alikamatwa na
katika mahojiano alisema alikuwa anataka kukiangalia tu na
kwamba haikuwa nia yake kukiiba na kuomba msamaha. Hata hivyo alisema polisi wanaendelea kumhoji ili kubaini
dhamira halisi ya kukichukua kiti hicho. Alisema mara baada
ya upelelezi wa kesi hiyo, mtuhumiwa huyo atafikishwa
mahakamani ili kujibu mashitaka yanayomkabili ya wizi wa
kiti hicho cha Mwenge wa Uhuru. Mwenge huo wa Uhuru uliingia Arusha Juni 3 mwaka huu
ukitokea mkoani Manyara na utakimbizwa katika wilaya
mbalimbali za mkoa wa Arusha kabla ya kukabidhiwa kwa
mkoa wa Mara Juni 11, yaani Jumanne ijayo.
 
Angewaambia ana Bibi/Babu yake Mzee hawezi kuchuchumaa kwenye Tundu la Choo cha Shimo akaona kigoda hicho ni muhimu.PERIOD
 
cHEzea machali wa ARACHUGA?wamalamba mpaka Tunzo.Kama kigoda kimechukuliwa si wakachonge kingine 2 au kilichopo sasa kina nin?kama vip wahusika wawajibike
 
maeneo ya Philips ni chadema stronghold!
huu mwenge upumzishwe makumbusha kwani hata mwaka jana wananchi wa Lindi waliamua kuuzima kwa muda.

namuonea huruma magesa mulongo na kamati yake ya ulinzi na usalama...
 
Mabaki pekee ya Falsafa za Mzee Nyerere yanaanza kupotea Mwenge + Muungano bye byee!!
 
Kwani hawajaenda kuilaza hiyo kimwenge hapo Ngalelo? Wangeambulia majivu tu!

Eti mwenge!
 
Duuh makubwa haya
Teh teh kwi kwi

Mwenge nadhani uwe wa dijitali km tochi
za kuchaji tu ili........
 
Polisi wangeanza kujitoa katika suala la ulinzi wa mwenge na sherehe za mwenge kutokana na majukumu mengine waliyokuwa nayo.

Anayetaka kuendeleza kuukimbiza mwenge atafute njia zake za usalama lakini isiwe polisi, jeshi au askari magereza.
 
Manufaa hauna kwako sisi tunajivunia mwenge wetu, na njaa nyngne mbaya

Wewe binafsi Mwenge unakusaidia nini katika maisha yako ya kila siku??
Kuna lipi ulilofaidika nalo kupitia huu mwenge?
 
Tena sijajua hivi mzee waryoba kauongelea kwenye rasimu manake deal pekee iliyobaki ni kupata nafasi ya kuukimbiza

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Huyo kijana huendaalifanya hivyo kwania ya kutaka kujulikana na kupata umaarufu tu, hakuna chochote cha zaidi, kwa sababu kiti cha akiba huwa hakiwekwi karibu sana na mwenge, ingekuwa shughuli nzito angemudu kunyakua au kubeba kilichokuwa kinatumiwa kuwekea Mwenge
 
Back
Top Bottom