lendila
JF-Expert Member
- Sep 26, 2012
- 5,806
- 4,370
Kigoda cha Mwalimu Nyerere ni taasisi inayojitangaza kwa watanzania kuwa imekuwa na kazi ya kuenzi fikra za mwalimu Nyerere.
Je, ni kweli kigoda cha mwalimu Nyerere kinamuenzi kwa vitendo? Au kigoda cha mwalimu Nyerere ni wapigaji kama wapigaji wengine?
Kigoga cha Mwalimu Nyerere kimejipambanua wazi wazi mchana kweupe kuwa kinaenzi fikra za mwalimu nyerere. Swali linakuja je, kigoda hakioni jinsi makongamano yenye migongano na mawazo tofati yanayosuguana yamepigwa marufuku nchini?
Moja ya fikra za mwalimu nyerere ni kuwa na nchi yenye mfumo wa vyama vyingi vya siasa. Je, kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachukua hatua gani kwa kuona mfumo wa vyama vyingi vya siasa uko hatarini kuliwa na dola mchana kweupe?
Je, kigoda cha mwalimu Nyerere hakina haja ya katiba bora? Kigoda cha mwalimu Nyerere hakijasoma ripoti ya Jaji Kisanga, Jaji Nyalali, Jaji Warioba na kadhalika?
Kigoda cha mwalimu Nyerere kinamuenzi mwalimu kwa lipi? Kwa fikra? Je, hawasikii watanzania wenye mawazo tofauti wanavyokula matusi mazito kutoka kwa Mkapa?
Naomba kigoda cha mwalimu Nyerere wajitafakari upya na wadumishe kweli fikra za mwalimu Nyerere kwa vitendo ikiwepo fikra ya mwalimu Nyerere ya kuleta mfumo wa vyama vyingi vya kisiasa.
Fikra ya mwalimu ya watu kuwa huru bila kubughudhiwa, kubaguliwa kwa vyama vyao, rangi zao dini zao, makabila yao na kadhalika.
Uhuru wa kutoa na kupokea maoni.
Haya ni maendeleo makubwa kwa mwanadamu kuliko hata majengo barabara,ndege na kadhalika,maendeleo ni watu, maendeleo sio vitu mwalimu Nyerere aliyasema haya mwaka 1972, maendeleo ni pamoja na uhuru wa watu kujieleza, kupingana, kukusanyika na kadhalika.
=======
Kigoda cha Mwalimu Nyerere ni nini? SOMA => Kigoda cha Nyerere na utakatifu wake