Kigoda awaalika Wakorea kuwekeza Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigoda awaalika Wakorea kuwekeza Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Aug 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Saturday, 18 August 2012 09:13

  Geofrey Tengeneza- Seoul Korea Kusini.
  Waziri wa Viwanda na Biashara,Dk Abdallah Kigoda ametoa rai kwa wafanya biashara na wawekezaji nchini Korea kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali za uchumi nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na sekta ya utalii ambayo amesema ina fursa nyingi za uwekezaji katika nyanja tofauti kama vile malazi, usafiri na usafirishaji watalii, utalii wa majini (cruise boat) na kadhalika.

  Kuhusu utalii barani Afrika, Dk Kigoda amewaambia wawekezaji hao kuwa, Tanzania ni eneo bora la utalii kwani ni nchi yenye vivutio vizuri na vya aina yake barani Afrika, hivyo akawahimiza kuja kuitembelea na kujionea wenyewe utajiri, uzuri na upekee wa vivutio hivyo vya utalii ukilinganisha na vile vinavyopatikana katika nchi nyingine Afrika na duniani kwa ujumla.

  Waziri Kigoda alitumia fursa hiyo kumpongeza mwanamuziki maarufu wa hapa Korea na mwenye washabiki wengi nchini hapa aliyejulikana kwa jina moja la Choy kwa kazi nzuri ya kuutangaza mlima Kilimanjaro nchini Korea kupitia sanaa ya muziki “Tanzania ina utajiri wa vivutio vingi vya utalii, kwa mfano mlima Kilimanjaro uko Tanzania, narudia kwa msisitizo kuwa uko Tanzania na si nchi nyingine yeyote, na nina mshukuru sana mwanamuziki Choy kwa kuutangaza mlima huo hapa Korea, alisema waziri Kigoda huku akishangiliwa kwa makofi.

  Waziri Kigoda ameyasema hayo hivi karibuni jijini Seoul nchini Korea katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa mkutano wa kibiashara baina ya wafanyabiashara na wawekezaji wa kikorea takribani 100 kutoka katika sekta kadhaa chini hapa na ujumbe wa maofisa wa Serikali ya Tanzania kutoka sekta mbalimbali uliofanyika katika hotel ya Lotte na kuhuduriwa pia na jumuia ya watanzania wanaoishi nchini Korea.

  Alivitaja baadhi ya vivutio ambavyo Tanzania inajivunia kuwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika, Bonde la Ngorongoro ambalo ni maajabu ya nane ya dunia, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ni miongoni mwa maajabu mapya saba ya dunia na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa utalii wa fukwe na maeneo ya Kihistoria.

  Pembezoni mwa mkutano huo kulikuwa pia na maonesho madogo ya utalii wa Tanzania ambapo wawekezaji hao walipatiwa pia vielelezo kadhaa vya utalii sambamba na maelezo yaliyokuwa yakitolewa na maofisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA)

  Katika mkutano huo jumla ya mada nne ziliwasilishwa tatu miongoni mwa hizo kutoka Tanzania ambazo ziliwasilishwa na wawakilishi kutoka Shirika la EPZ (iliyohusu uwekezaji kwa ujumla), Shirika la STAMICO (uwekezaji katika sekta ya madini) na Bodi ya Utalii Tanzania(Utalii wa Tanzania).

  Baada ya uwasilishwaji wa mada wafanyabiashara na wawekezaji hao wa hapa Korea walipata fursa ya kukutana uso kwa uso na maofisa wa taasisi mbalimbali kutoka Tanzania kwa mazungumzo ya namna ya kushirikiana na kuanzisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji nchini Tanzania.

  Mkutano huo wa Kibiashara wa Seoul uliotayarishwa na Mamlaka ya Biashara ya Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na chama cha watanzania wanaoishi na kusoma hapa Korea umefanyika sambamba na maonyesho ya Kimataifa ya Biashara katika mji mwingine wa Yeosu na kuhudhuriwa na waonyeshaji zaidi ya waonyeshaji 30 kutoka katika sekta ya umma na binafsi nchini Tanzania pamoja na kikundi cha ngoma kutoka chuo cha sanaa Bagamoyo (TASUBA)
   
 2. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Hii ni fursa nyingine pekee ya kuhamishia maliasili zetu upande wa mashariki!
   
 3. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  nchi haina umeme , maji + miundo mbinu ya kubahatisha . nani aje
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Hakuna mafanikio yoyote tuliyaona hadi sasa pamoja na kukaribisha wawekezaji mbali mbali nchini ikiwemo dhahabu, tanzanite, uranium, almasi, gas. Tunachoona ni wao kuendelea kufaidika na kuondoka na mabilioni na Watanzania walio wengi wakiendelea kuishi katika ufukara wa kutisha.

  Imefikia wakati wa kusimamisha wawekezaji kungia nchini mpaka ili kutathmini kwa kina mafanikio/hasara tulizozipata kutokana na kuruhusu "wachukuaji" kuingia nchini kwa zaidi ya miaka 12 sasa.
   
Loading...