Kigezo kinachotumika kupima ukuaji wa uchumi si sahihi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigezo kinachotumika kupima ukuaji wa uchumi si sahihi.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Byendangwero, Apr 4, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kigezo cha 'gross national product (GDP)," au zao ghafi la taifa (ZGT) kwa kiswahili, kinachotumiwa katika kupima ukuaji wa uchumi kinapotosha ukweli. GDP auZGT ni jumla ya thamani ya bidhaa zote na huduma zote zilizozalishwa katika nchi katika kipindi cha mwaka mmoja, bila ya kujali kama bidhaa hizo au huduma husika ilitolewa na raia au la. Tatizo linalojitokeza ni kwamba mali nyingi zinazozalishwa hapa nchini na makampuni ya nje, sehemu kubwa ya pato linaslotokana na mali hizo linabakia huko huko nje, (mfano mzuri ni wa madini ambayo serikali iliridhia kampuni hizo kubakiza mauzo yao huko nje eti ili kuziwezesha kulipa madeni) sisi tunabakia tukihesabu hewa. Katika kulifafanua hilo nitatoa mfano mdogo; kwa mfano kama mtu anayo nyumba yake, na akaamua kupangisha nyumba hiyo kwa mtu mwingine kwa kodi ya pango ya shs. 6 milioni kwa mwaka. Na mtu huyo akaitumia kwa bihashara ya "lodging" na kupata faida ya shs. 20 milioni kwa mwaka mathlani. Itakuwa ni wende wazimu kwa mtu huyo mwenye nyumba kupita huku na kule akitamba ya kuwa hali yake ni nzuri kwakuwa nyumba yake imeongeza uzalishaji kutoka shs 6 milioni hadi 20 milioni! Lakini sisi kama taifa ndivyo tufanyavyo. Katika hali hiyo haishangazi kuona JK na mtendaji wake mkuu wanashindwa kujua ni sababu zipi zinawafanya watu kuwa masikini wakati takwimu zinaonyesha kuwa uchumi unapaa!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa ilimu hii. Mimi si Mchumi naomba unisaidie ili nami niwe na uelewa.:

  1. Hivi watu/nchi nyingine duniani zinatumia kipimo gani (SI Unit) katika kupima uchumi wao?
  2. Kama GDP siyo kipimo muafaka, basi kuna kipimo gani mubadala ambacho Tanzania inaweza kukitumia ili kupata kipimo sahihi cha uchumi wa Tanzania?
   
Loading...