Kigezo hiki kinafaa kutumika kumpima Rais ajaye...

Kau na Wana JF,
Ni kweli sio tu Vijana ni kwa Watanzania wote, Maendeleo ya Watanzania yataletwa na Watanzania wenyewe
ila tatizo moja kubwa kwetu ni hii system, viongozi wetu wenye dhamana ya kusimamia Sheria ndio wa kwanza kuzivunja, mifano ipo mingi sina haja ya kuyatolea mifano, nenda Hospitali, Polisi, Mahakama etc utaona nina maana gani, kama haumjui mtu au kama hauna noti kwisha kazi yako, haki na sheria zinavunjwa hakuna wa kumuuliza, ukimuuliza Mkuu wa Kaya na majibu yake mepesi mepesi, SIJUI, hajui hata kwa nini Nchi Masikini ?? Shame On it
Nawakilisha

Kikarara nimekupata vizuri. Mfumo ukiwa mbovu,hata ukifanyaje utakuwa unapiga maktaimu. Mfano shilingi inavyoporomokaga thamani yake.. na kushindwa kudhibiti mchakato mzima wa mafuta[petroli,dizeli na ya taa]..
 
Lile jibu la Dokta liliniacha hoi na ndio kigezo cha Ehud Barak kutufanya sample ya irrelevant country. Hebu jiulize mtu atafikiri nini kwa jibu kama lile: Hawa jamaa walikuwa hawana mtu mwenye utashi wala nia ya kugombea urais, kwa hiyo wakamuomba huyu agombee hivyo hivyo tu mpk atakapopatikana mwenye uwezo

Kwa sababu ktk hali ya kawaida, mtu mpk ufikie kugombea uongozi maana yake umeshanalyse matatizo na changamoto zilizopo, ukajipima na kujiaminisha kuwa utazimudu, then ndio unaomba ridhaa ya wenzako ili ukamilishe vision yako. Sasa kama huyu alijibu hajui, kwa nini tumlaani Ehud Barak kwa aliyoyasema kuhusu sisi? Si ni kama tunajiendeaendea tu.

Vigezo kaka nimekubali, lkn naongezea jambo: Waangaliwe tabia zao za utotoni na kupimwa akili kwanza
 
tanzania ni maskini kwa sababu wananchi wake ni wajinga wanaotegemea serikali ifanye kila kitu wakati wao wakikaa kulalamika bila kuchukua hatua zozote serikali hiyo hiyo wanayoitegemea inapowaibia na kuwatupa.....watz ni makondoo na huu ni umaskini tungekua tunachukua hatua na kuacha kulalamika serikali ingenyooka na kufanya kazi na umaskini ungepungua kwa wengi wetu lakini.....
 
Umetuacha dilemma mharakati. Unaposema hatua,basi uzitaje...
 
Lile jibu la Dokta liliniacha hoi na ndio kigezo cha Ehud Barak kutufanya sample ya irrelevant country. Hebu jiulize mtu atafikiri nini kwa jibu kama lile: Hawa jamaa walikuwa hawana mtu mwenye utashi wala nia ya kugombea urais, kwa hiyo wakamuomba huyu agombee hivyo hivyo tu mpk atakapopatikana mwenye uwezo

Kwa sababu ktk hali ya kawaida, mtu mpk ufikie kugombea uongozi maana yake umeshanalyse matatizo na changamoto zilizopo, ukajipima na kujiaminisha kuwa utazimudu, then ndio unaomba ridhaa ya wenzako ili ukamilishe vision yako. Sasa kama huyu alijibu hajui, kwa nini tumlaani Ehud Barak kwa aliyoyasema kuhusu sisi? Si ni kama tunajiendeaendea tu.

Vigezo kaka nimekubali, lkn naongezea jambo: Waangaliwe tabia zao za utotoni na kupimwa akili kwanza

Analysis yako nimeipenda shizukan.. Asante.
 
sijawahi kusikia kama BMW aliwahi kutamka hivyo nukuu nyingi zinaonesha jk ndio mwenye huo usemi. Kuhusu kigezo cha kumpima mgombea urais naungana na wewe kwamba ni vizuri kila mgombea akatueleza watz kinagaubaga yeye anaona sababu zipi zizofanya nchi yetu iwe kama ilivyo.

nilisharekebisha uzi@ chak..
 
nakuunga mkono mkuu mimi mwenyewe sijawahi ona wala kusikia BWM akisema hii kauli ila aliisema Mk.were alipokuwa akihojiwa na BBC mwaka 2006 kipindi cha hard talk. Ndipo wenyeakili tulipoanza kujua kuwa president wetu ni chaka mwitu. Mkapa alikuwa na vision na asingeweza kujibu hivyo. Ameshahojiwa na international media mara kibao hata sasa hajawahi chemka kma mke..re. Ila kigezo kwa president ajaye naunga mkono.

nilirekebisha uzi tayari
 
Tuna mitazamo tofauti na ndio maana tunaishi na tunapambana lakini kutokana na mfumo mbovu hali zetu zinakuwa chini ya matarajio na ndio maana tunaelimishana makosa yaliyotendeka ili tulisahihishe na tusilirudie. Labda ungesaidia sana kutuelimisha tutapambana vp na mfumuko wa bei, kupanda kwa kodi ya mafuta ya taa, kujazana kwa vitu vilivyo chini ya kiwango, elimu duni?

kila mtu anaboresha maisha yake na familia yake.. Ila si lazima Rais ajinadi? Hili akilijibu,na mwingine na mwingine,tunakuwa na uwanja mpana wa kuchagua
 
Wana JF au huu si ''umbumbumbu''?? Kiongozi wa nchi asiyejua chanzo cha matatizo ya nchi yake. Si ujuha huo? Humu JF kwa sasa kuna wanaopigia debe watu ili wateuliwe kugombea..... Hawana mchango labda kwa sababu unaapply ule msemo wa ''...apendaye haoni..,hata chongo ataita kengeza....??
 
muktadha wako ni mzuri.. Shida yake ni kwamba haumjadili mtu, haumtaji mtu.Sidhani kama utachangiwa sana..
 
Back
Top Bottom