Kigezo hiki kinafaa kutumika kumpima Rais ajaye...

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,758
736
Rais wa nne wa nchi yetu Jakaya M. Kikwete,aliwahi kunukuliwa akisema hajui kwa nini nchi yake ya Tanzania ni maskini!
 
Na katika awamu hii ya nne,alinukuliwa PM,akitoa kauli hiyo![someone can correct me on this..]
 
Sasa hiki kiwe kigezo nambari wahedi! Badala ya ahadi tele za maji safi, zahanati,umeme,shule,madaraja,n.k. kigezo namba moja kiwe kujibu swali hili... Nchi yetu ni maskini kutokana na :-
1. .........
2. .........
3. .... kisha aanzie hapo. Tutawapima huku tukiwaangalia machoni kama wanatufaa,lakini mpaka tunaingia kwenye chumba cha kura tunakuwa na informed choice ya kiongozi.....
 
Viongozi wenye elimu tunao,uzoefu tunao,vijana tunao... Ripoti za Tume mbalimbali zipo! Lakini bado haijafahamika kwa nini asilimia 89.9 tunaishi chini ya dola 2!
 
Rais wa tatu wa nchi yetu Ben Mkapa,aliwahi kunukuliwa akisema hajui kwa nini nchi yake ya Tanzania ni maskini!

sijawahi kusikia kama BMW aliwahi kutamka hivyo nukuu nyingi zinaonesha jk ndio mwenye huo usemi. Kuhusu kigezo cha kumpima mgombea urais naungana na wewe kwamba ni vizuri kila mgombea akatueleza watz kinagaubaga yeye anaona sababu zipi zizofanya nchi yetu iwe kama ilivyo.
 
nakuunga mkono mkuu mimi mwenyewe sijawahi ona wala kusikia BWM akisema hii kauli ila aliisema Mk.were alipokuwa akihojiwa na BBC mwaka 2006 kipindi cha hard talk. Ndipo wenyeakili tulipoanza kujua kuwa president wetu ni chaka mwitu. Mkapa alikuwa na vision na asingeweza kujibu hivyo. Ameshahojiwa na international media mara kibao hata sasa hajawahi chemka kma mke..re. Ila kigezo kwa president ajaye naunga mkono.
 
Asanteni kwa kuboresha na nafuta kauli yangu..! Tena kwenye hii pg ya kwanza.. Lakini ni kigezo bora cha kumpima mtu! Ingawa sina kumbukumbu ni Rais yupi,ntajaribu kuhakikisha majibu yenu. Thanks
 
nakuunga mkono mkuu mimi mwenyewe sijawahi ona wala kusikia BWM akisema hii kauli ila aliisema Mk.were alipokuwa akihojiwa na BBC mwaka 2006 kipindi cha hard talk. Ndipo wenyeakili tulipoanza kujua kuwa president wetu ni chaka mwitu. Mkapa alikuwa na vision na asingeweza kujibu hivyo. Ameshahojiwa na international media mara kibao hata sasa hajawahi chemka kma mke..re. Ila kigezo kwa president ajaye naunga mkono.

Ingawa aliwahi kupanic kwenye kipindi hichohicho,akaloose temper kwa maswali.. 'now you are getting angry Mr President...' akajibu 'Of course....' anyway turudi kwenye hoja.. Na iwe ajenda kwa wananchi wote maana sijui kama nafasi ya midahalo itapatikana!
 
Hoja yako nzuri ila aliyesema hayo maneno ni JK na si BWM,kweli rais ajaye lazima ajibu swali kwnn tz maskin?
 
siasa siku zote ni mchezo mchafu,kwa hiyo usitegemee kwa maisha yako kubadilika kwa kupitia RAISI,vijana tubadilisha mtazamo wetu...............
 
Tuna mitazamo tofauti na ndio maana tunaishi na tunapambana lakini kutokana na mfumo mbovu hali zetu zinakuwa chini ya matarajio na ndio maana tunaelimishana makosa yaliyotendeka ili tulisahihishe na tusilirudie. Labda ungesaidia sana kutuelimisha tutapambana vp na mfumuko wa bei, kupanda kwa kodi ya mafuta ya taa, kujazana kwa vitu vilivyo chini ya kiwango, elimu duni?
 
Mwenye uchungu na mali za tanzania kama nchi,awe ameshapambana tayar na mafisadi na awapende watanzania na awe na msimamamo dhidi ya mabepari.
 
hivyo si vinaweza kuahidiwa? Kwanza ajue umaskini wa nchi anayogombea Urais,kwanini ni masikini..atueleze..
 
...mkuu hapo kwenye swali la kwanza nadhan itakuwa vizuri akaulizwa kwanza kama anajua tanganyika ni masikin alfu ndo yafuate hayo maswali mengine,kuna watu hapa Tanganyika wana-pesa za kufulu,ukimwambia kuna watu hawajui watakula nini leo anaweza ata akakupiga kofi kwa kutoamini maneno yako,na hao ndo kati ya wagombea wanaojitokeza kila mara kugombea urais.Mfano mtu kama "MZEE WA VIJISENTI" unadhani ukimwambia kwamba kuna watanganyika wanalala na njaa hatawezi kukuelewa,na usi-shangae ata yeye akakuuliza...."bwana mdogo kuna mtu anakosa vijisente ata vya kununulia chakula?!" ...
 
Pamoja mkuu ila naona Kau amelala labda akiamka atatuelimisha/atajibu hayo maswali.

Unajua imefikia hatua mtu anatafuta success kwa gharama yoyote! Watu wako tayari kutoa/kupokea rushwa,kuudhalilisha hata utu wao,na njia nyingine zisizofaa,ili mradi mafanikio yapatikane.. Kama namwelewa vizuri,ndiyo typ ya kau...
 
...mkuu hapo kwenye swali la kwanza nadhan itakuwa vizuri akaulizwa kwanza kama anajua tanganyika ni masikin alfu ndo yafuate hayo maswali mengine,kuna watu hapa Tanganyika wana-pesa za kufulu,ukimwambia kuna watu hawajui watakula nini leo anaweza ata akakupiga kofi kwa kutoamini maneno yako,na hao ndo kati ya wagombea wanaojitokeza kila mara kugombea urais.Mfano mtu kama "MZEE WA VIJISENTI" unadhani ukimwambia kwamba kuna watanganyika wanalala na njaa hatawezi kukuelewa,na usi-shangae ata yeye akakuuliza...."bwana mdogo kuna mtu anakosa vijisente ata vya kununulia chakula?!" ...

aah mkuu... Unadhani hawajui? Wanajua ila wanafunga macho tu! Kwani unafikiri ni vigumu? Si unafunga macho tu?! Tena age ya Chenge ndo kabisa wanajua umaskini.Labda ungeniambia watoto wao. Hawa huenda hata kuchemsha yai akala hajui! Ila wazazi wao wamechunga sana mbuzi na ng'ombe,wametembea pekupeku vichakani na kuangua maembe maporini,si ajabu sukari tu kwenye chai walikuwa wanaisikia kwenye bomba..
 
Back
Top Bottom