Kigezo cha uzoefu kiondolewe kuwezesha ajira kwa vijana


Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,092
Likes
4,037
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,092 4,037 280
Kwenye suala la ajira kuna umuhimu wa uzoefu, lakini pia kuna haja ya kuwapo kwa nafasi za watu wasio na uzoefu, kwa sababu ni vigumu mtu anayetoka chuoni kuwa na uzoefu wa kazi wakati hajawahi kuajiriwa.

Vijana wengi waliohitimu elimu ya juu wanapitia kipindi kigumu katika maisha yao kutokana na changamoto za ukosefu wa ajira nchini, hivyo ni vyema tatizo hili likatazamwa kwa jicho la ziada.

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Rais John Magufuli aliahidi kupambana ili kuhakikisha Watanzania wengi wanapata ajira kwani alikerwa na kigezo cha uzoefu ili mtu apate ajira.

Kiongozi huyo akasema, wapo vijana wengi wanaohangaika kutafuta ajira baada ya kuhitimu kwa kuwa ajira nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu wa kufanya kazi.

“Vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wanapata shida kupata ajira kutokana na waajiri kuhitaji uzoefu, sasa mwanafunzi ambaye amemaliza chuo leo atapata wapi uzoefu wakati hajaajiriwa?” alihoji na kuongeza:

“Tena wanataka uzoefu wa hadi miaka mitano wakati mwingine, huo uzoefu wataupata wapi? nataka kama kuna uwezekano haya mambo ya uzoefu yafutwe kabisa.”

Rais alisema hayo kwa uchungu kwani anatambua serikali imejitahidi kuweka fursa ya kuwawezesha vijana wengi nchini kupata elimu, pia kuwezesha sekta binafsi kutoa elimu kupitia shule na vyuo binafsi.

Lakini bahati mbaya vijana wengi waliomaliza elimu ya juu bado ni tegemezi kutokana na ukweli kwamba hakuna ajira za moja kwa moja na sababu kama hizi za vigezo vya uzoefu ndipo tatizo linaongezeka kwao.

Niseme tu kwamba kuanzishwa kwa shule za kata wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kulipanua wigo kwa wanafunzi wengi nchini kujiunga na elimu ya sekondari kwa gharama nafuu.

Hatua hiyo pia ilisababisha ongezeko kubwa la wanafunzi wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu na hivyo kuanzishwa kwa vyuo vikuu vingi vya serikali na binafsi.

Sasa maisha ya wasomi baada ya kuhitimu elimu yao ndio kama hayo ya kuhangaika huku na kule kutafuta ajira, huku kigezo cha uzoefu wa kazi kikiwakwamisha baadhi yao.

Matokeo yake ni kwa wengine kujikuta wakilazimika kujihusisha na kazi tofauti na zile walizosomea, na sidhani kwamba katika mazingira hayo wanaweza kufanya kazi hizo mpya kwa weledi.

Wakati wale wasiotaka kufanya kazi tofauti na elimu yao wamekuwa wakilaumiwa kuwa wanachagua kazi wakisisitizwa kufanya kazi yoyote halali ili mradi mkono uende kinywani.

Kama ndivyo ina maana gani mwanafunzi kusota chuoni kwa miaka kadhaa kusomea taaluma fulani halafu mwisho wa siku anaambiwa asichague kazi? Hiyo taaluma yake haina umuhimu?

Sera ya Vijana Tanzania ya Mwaka 2007 inatambua vijana kuwa ni watu wote wenye umri wa miaka 15 hadi 35 na kulingana na Sensa ya Mwaka 2012, vijana ni asilimia 34.7 ya Watanzania wote.

Katika asilimia hiyo wamo wasomi na wengine wa kawaida ambao wamekuwa wakisota mitaani bila ajira au kujishughulisha na biashara ndogondogo ambazo kimsingi haziwezi kuwafikisha kokote.

Muungwana anaona basi kuwa ni vyema kundi hili la vijana likasaidiwa kadri inavyowezekana na mojawapo ya msaada mkubwa kwa kundi hili ni kuondoa kabisa kigezo cha uzoefu ili kulirahisishia kupata ajira.

Sidhani katika hali hii ya sasa kama vijana hawa wanaweza kwenda katika taasisi za fedha na kupata mkopo wa fedha bila kuwa waajiriwa au kuwa na dhamana inayokubalika ili kupata mitaji.

Hii ni kwa sababu taasisi za fedha hazikopeshi wasio na ajira au dhamana isiyohamishika kama nyumba, shamba au hati ya kiwanja.


Chanzo: Nipashe
 
Joseverest

Joseverest

Verified User
Joined
Sep 25, 2013
Messages
39,893
Likes
47,356
Points
280
Joseverest

Joseverest

Verified User
Joined Sep 25, 2013
39,893 47,356 280
Naunga mkono hoja
 
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Messages
26,589
Likes
59,165
Points
280
Age
21
Daby

Daby

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2014
26,589 59,165 280
Waanze wao seriklini kwenye aina zote za kazi.


Kumfundisha kijana kazi huku unahitaji ujuzi wake kampuni ipate faid ma nguvukazi yake kwa muda mwaafaka ni kitendawili kwa taasisi binafsi huku kuna wenye ujuzi waliyoifanya hiyo kazi kwa miaka kadha kiasi kwamba akija ni kuanza tu.
 
Nyabhakangala

Nyabhakangala

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2016
Messages
732
Likes
539
Points
180
Age
26
Nyabhakangala

Nyabhakangala

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2016
732 539 180
Kwakweli maana ukiomba jkt watataka uzoefu mortuary pia ukiomba wataitajiuzoefu sasa sjui hizi kazi tutazipataje.
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
21,861
Likes
46,768
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
21,861 46,768 280
Hilo ni jambo jema
 

Forum statistics

Threads 1,215,086
Members 463,007
Posts 28,535,109