Kigeugeu cha serikali,Yanga Simba ruksa Kagame cup Darfur!!!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Ni kama aina fulani ya Kigeugeu.
Lakini ndio hali halisi.
Yanga na Simba sasa ruksa kushiriki kagame cup Darfur!!
 
Hacha utani wewe, timu zimeshavunja kambi! Makubwa sasa
Labda kama leo ni siku ya wajinga!
Ila ni kauli ya serikali kutoka bungeni leo,ila pia cecafa imeshaziondoa Simba na yanga kwenye michuano hiyo na kuzipa nafasi timu nyingine.
 
Confirmed!!
Kuna kikao kinaendelea usiku huu pale TFF ili kujua nini cha kufanya maana cecafa ilishaziondoa pia!
 
Dodoma/Dar es Salaam. Serikali imetoa ruksa kwa timu za Simba,Yanga na Falcon za Tanzania kushiriki Kombe la Kagame litakalofanyika nchini Sudan, huku viongozi wa timu hizo wakishangazwa na taarifa hizo.
Kabla ya kauli hiyo, Serikali ilitangaza kuzizuia timu hizo kwenda kushiriki kwenye mashindano hayo kwa sababu zakiusalama hasa katika jimbo la Darfur, moja ya kituo kilichopangwa kufanyika mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makala amewaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa Serikali ya Tanzania imewasilianana Serikali ya Sudan na kuhakikishiwa usalama wa wananchi wake katika michuano hiyo iliyopangwa kuanza Jumanne ijayo.
“Serikali ilikuwa na kigugumizi kuhusu ushiriki wa timu zetu za Simba Yanga na Falcon, lakini leo (jana) nimepokea Fax kutoka Serikali ya Sudan ikihakikishia usalama kwa wachezaji na Watanzania watakaosafiri na timu kwenda nchini humo,” alisema Makala.
Aliongeza: “Wametueleza mikakati yao ya jinsi watakavyotekeleza suala la ulinziwa timu kutoka uwanja wa ndege, hotelini na kwenda uwanjani bila shida yoyote.”
Makala alisema kutokana na uhakika wa usalama, wameamuakuziruhusu timu hizo kwenda Sudan.
Alisema awali walielezwa na Chama cha soka cha Sudan na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kuwa wachezaji watasafirishwa na helikopta toka Khartoum mpaka Darfur.“Walituambia hakuna wasiwasi wa usalama, kwamba timu zote zitapewa ulinzi wa kutosha kwenda uwanjani na kurudi hotelini,” alisema Makala.
Aliongeza: “Mbali na ulinzi na usafiri wa Helikopta, pia watatoamavazi kuzuia risasi kupenya (bullet proof), lakini sasa Serikali ya Sudan imeongeza kutuhakikishia ulinzi na usalama wa wananchi wetu, sisi tunatoa Baraka zetu zote, washiriki mashindano hayo na waje na Kombe” alisema.
Makala alisema Serikali imebeba dhamana ya Watanzania watakaoenda nchini Sudan kwenye mashindano hayo na kuzitaka timu husika kuendelea na mashindano na kuhakikisha vinakuja na kombe.
Hata hivyo wakati Serikali ikiziruhusu timu hizo kwenda kushiriki Kagame, tayari Cecafa ilishapanga upya ratiba na kuteua timu nyingine kuziba nafasi ya timu za Tanzania.
Timu hizo ni kutoka Uganda (URA), Rayon kutoka Rwanda ambazo ni timu mwanachama wa Cecafa, na timu mwalikwa kutoka nchini Chad ya Elite Sports.
Viongozi wa Simba na Yanga walipoulizwa kuhusu taarifa hizo, walisema hawana taarifa kama alivyosema Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Laurance Mwalusako, Katibu Mkuu wa Yanga alisema: “Klabu haina taarifa zozote kutoka Serikalini au TFF. .
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alisema: “Sina habari zozote, nipo na Waziri (Makala) Dodoma, mbona hajanijulisha lolote.”
Uwezekano wa timu hizo kwenda ni mdogo kutokana na ukweli kuwa taarifa hiyo imekujamuda mfupi kabla michuano kuanza.
Lakini pia kuna wasiwasi kama Cecafa wanaweza kuziruhusu timu hizo kwenda kwa vile tayariwalishaziteua timu nyingine kuchukua nafasi za timu za Tanzania.

Source: Mwananchi
 
Huu ni ubabaishaji uliokubuhu. Mtu anakurupuka na kutoa maamuzi mazito ya kuzuia timu zishiriki, baada ya muda mfupi mtu huyo huyo anakuja na maamuzi ya kuruhusu timu zishiriki. Huu ni ushahidi tosha kuwa Makala hakuwa makini katika maamuzi yake.
 
Back
Top Bottom