Kigangwalla na wabunge wa wadesign yako someni kauli ya Deo (MB)- No Maslahi ya chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigangwalla na wabunge wa wadesign yako someni kauli ya Deo (MB)- No Maslahi ya chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bemg, Apr 29, 2012.

 1. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  FILIKUNJOMBE ANENA


  FILIKUNJOMBE ANENA
  Mbunge wa Ludewa (CCM) akizungumza katika mahojiano maalum ya NIPASHE Jumapili jijini Dar es Salaam juzi, Filikunjombe alisema tuhuma zinazowakabili mawaziri husika ni moja ya maeneo yanayoiathiri jamii pana ya Tanzania hivyo hakuna sababu ya kuweka mbele maslahi ya kisiasa.
  Alisema kama hoja ya kuwataka mawaziri kujiuzulu ingesimamiwa kidete na wabunge wa upinzani, isingekuwa na nguvu kama ilivyotokea kwa upande wa CCM.
  “Hoja hii ingesimamiwa na akina Zitto Kabwe isingekuwa na nguvu kwa maana watu wangesema ni kawaida ya upinzani, lakini wabunge wa CCM tuliposimama na kuzungumza, imeleta matokeo makubwa,” alisema.

  Filikunjombe alisema hali ya ustawi wa jamii imedumaa huku baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wakijilimbizia mali kinyume cha sheria.
  “Tunapokuwa majimboni kama kule kwangu Ludewa, wananchi wanahoji kuhusu ukosefu wa huduma bora za afya, elimu, miundombinu na maji safi na salama,” alisema.
  Aliongeza,“ kwa hali ilivyo sasa na hulka hii ya mawaziri wasiokuwa waaminifu kuhujumu rasilimali za nchi, si rahisi kuyafikia maisha bora kwa kila Mtanzania.”  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. Lawrence Luanda

  Lawrence Luanda JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Filikunjombe ni mkweli na jasili, tatizo sio maslahi ya chama bali ni nizamu ya uoga waliyonayo wabunge wengi kwa vyama vyao na kujua kwamba wako responsible to both vyama na wananchi hivyo ku balance majukumu yao.
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kigwangallah ni mchumia tumbo, ni mtu wa "hand to mouth politics".
   
 4. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  hahaha yaweza kuwa maneno yako
   
Loading...