Kigamboni new city haimo kwenye bajeti hii vipi tena?

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,617
37,815
Wakuu,

Kama mnavyojua Serikali ya awamu na nne ina mpango wa kujenga Kigamboni new CITY ili kuleta sura mpya ya JIJI la Dar es salaam.
Nimesoma soma bajeti sijanusa ndani yake kama kuna mpango huu wa Kigamboni new CITY kwenye bajeti hii vipi? au pesa zake hazitapitia bungeni zitakuja moja kwa moja kuanza mradi? hata hili daraja nilisikia NSSF wanajenga ila bado hatujaona nondo wala mfuko wa siment ukipelewa site kulikoni.

Si chokochoko ila mwenye full info naomba anijulishe kwa faida ya wana kigamboni wenzangu. Tunausubiri mradi huu kwa hamu kubwa, ila njisi serikali inavyokuwa na usiri kuhusu mradi huu na ndivyo mradi huu unavyozidi kuwa na ugumu kuutekeleza ukizingatia wananchi wanazidi kuongezeka katika eneo husika na kuendelea kujenga makazi yasiyo rasmi.

nawakilisha.

Yote yawezekana kwa yeye atutiaye nguvu:
 
Tunaongelea utekelezaji wa mradi wa kigamboni, sasa huo upumbavu wako umetoka wapi tena?
Upumbafu wako ni kushindwa kujua mradi huo hautekelezwi na serikali kama miradi mingine ya maendeleo bali ni maeneo ya uwekezaji yatakayo fanywa na sekta binafsi, huwezi kuona pesa hiyo kwenye bajeti.
 
Huo mradi una umuhimu gani kwa taifa? Tusiige tembo kwenda haja, kama Dubai au Canada wanafanya sio na sisi tuige tu.
 
Upumbafu wako ni kushindwa kujua mradi huo hautekelezwi na serikali kama miradi mingine ya maendeleo bali ni maeneo ya uwekezaji yatakayo fanywa na sekta binafsi, huwezi kuona pesa hiyo kwenye bajeti.

pia ni upumbafu mkubwa kutojua kwamba habari kama hizi serikali imezikalia bila ufafanuzi kwa wananchi wadau wa mradi huu namna na utekelezaji wake. huu ndiyo udhaifu wa serikali yako ya magamba. Wananchi wa kigamboni wanaoishi kwenye ardhi hii ya mradi huu wanatakiwa kujua how and when ya mradi in details.

Hawa wananchi wanataka kuendeleza makazi yao hawawezi kuendelea kungoja mradi wenye usiri siri mkubwa ndani yake. ni sawa na mtu kuishi kwa matumaini.
 
Usidandie gari kwa nyuma.Wewe ndiye mwenye uelewa mdogo.Usikurupuke tu na kutusi watu.
Umekwisha uona wapi Sekta binafsi inafanya shughuli kama za barabarara kwa maana ya kulipia gharama na mambo mengine ya miundobinu kama si serikali kwa kutukamua sisi walipa kodi.
Mradi huu una mambo mengi yanayohitaji pesa na ambayo yanagusa jamii(hospitali,mashule(sekondari na Msingi),maji,umeme,barabara hasa kwa watakaoathirika na mradi.

Upumbafu wako ni kushindwa kujua mradi huo hautekelezwi na serikali kama miradi mingine ya maendeleo bali ni maeneo ya uwekezaji yatakayo fanywa na sekta binafsi, huwezi kuona pesa hiyo kwenye bajeti.
 
mipango ya serikali yetu ni mingi ila utekelezaji wake ndiyo tatizo - unahitaji kuwa na roho ngumu kama ya mwendawazimu kuisubiria hii mipango. Kwa mafano ukisoma mipango ya TANESCO inatia moyo lakini utashangaa tupo gizani mpaka leo why? Ukienda wizara ya ardhi kuna mipango miji mizuri lakini hebu angalia jiji lenyewe lilivyo - vijuma hovyo hovyo vinaota kama uyoga. usimamizi ni dhaifu.
 
mpaka wametuzuia kununua ardhi wala kujenga huko. Wananchi hawawezi hata kuendeleza nchi yao kwasababu ya mambo kama haya!!
 
Usidandie gari kwa nyuma.Wewe ndiye mwenye uelewa mdogo.Usikurupuke tu na kutusi watu.
Umekwisha uona wapi Sekta binafsi inafanya shughuli kama za barabarara kwa maana ya kulipia gharama na mambo mengine ya miundobinu kama si serikali kwa kutukamua sisi walipa kodi.
Mradi huu una mambo mengi yanayohitaji pesa na ambayo yanagusa jamii(hospitali,mashule(sekondari na Msingi),maji,umeme,barabara hasa kwa watakaoathirika na mradi.

Huna akili na siwezi kukushinda kwenye upumbavu kwa kuwa wewe mzoefu, sasa nenda katafute satelite city ya kigamboni kwenye bajeti mbadala utaikuta.
 
Back
Top Bottom