Kigamboni na mpango wa Bush

uzeebusara

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
657
513
Habari wadau. Naomba mwenye ufahamu wa kina juu ya mpango wa ujenzi wa kijiji cha mfano Kigamboni wa Bush anielezee kwa kina Kwn nina nyumba yangu nahamu sana ya kuimalizia maana hizi kodi ninazolipa ktk nyumba hii ya kupanga ni kufuru. Na kama mnavyojua kila mwaka mwenye nyumba anawaza kupandisha kodi tu. Hivyo basi naomba mtu au mamlaka inayofahamu vzr ielezee km huo mradi upo au laa na kama upo ishu za fidia zipo vp. Asanteni
 
Ngoja tusubiri wenye data zaidi ila nahs ramani na details zimeanza kuvuja maana inasemekana kuna watu walishaanza kulipwa Kibada.
 
Ngoja tusubiri wenye data zaidi ila nahs ramani na details zimeanza kuvuja maana inasemekana kuna watu walishaanza kulipwa Kibada.

hawajaanza kulipwa. wanahakiki ili kujua unastahili kulipwa laki 7,5 au 3.5 kwa sq. m.
 
Ukimwuliza ata mbunge wetu hana jibu,nilifuatilia tangu waziri muhusika alipokuwa chiligati mpaka leo Prof Tibaijuka lakini bado hakuna maelezo ya moja kwa moja,suala zito wanafanya la kisiasa,watu wanataka kujenga wanashindwa wengine wanataka kuuza wanashindwa maana ata hao wanunuzi hawajui ili suala la kigamboni linavyoendeshwa..wanasiasa wetu wana bahati sana hapa ni Tanzania lakini ingekuwa Nigeria,mambo yangekuwa yameshaeleweka
 
Mimi na uchungu sana na haya mambo inayotufanyia wananchi wake. Hv kweli inafikia hata makazi ya raia wako unauza halafu fidia inakuwa kama vl msaada. Hv nchi hii sera ya wazawa kwanza ipo kweli. Lkn naamini kabisa IPO cku kitanuka tu. Mtu kajibana hadi kasimamisha kabanda lake then kirahisi tu unakuja kusema ooooh eneo hili linachukuliwa na mwekezaji. Kw nn msiwape hao wawekezaji maeneo ya kwao kwenye mahekalu km Masaki?
 
Back
Top Bottom