Kigamboni: Mradi wa mji mpya Kigamboni wayeyuka kiaina

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,367
33,008
Sunday, 08 January 2012 13:12

Elias Msuya
KUKIWA na maandalizi kabambe ya ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni, uchunguzi umebainika kuwa mji huo sasa umeyeyuka kiaina na huenda usitekelezwe tena.

Mradi huo ulitangazwa kwenye gazeti la Serikali mwaka 2008 na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, Salome Sijaona ambaye kwa sasa ni Balozi nchini Japan.

Baada ya tangazo hilo, aliyekuwa Waziri katika wizara hiyo, John Chiligati alilitangazia Bunge kuhusu mpango huo na kuanza kufanya mikutano ya uhamasishaji kwa wananchi wa Kigamboni...............................

............................................Hata alipofuatwa ofisini, alimwelekeza mwandishi wa habari kumwona Katibu Mkuu, Patrick Rutabanzibwa ambaye licha ya kuwa ofisini alikataa kuzungumzia suala hilo akisema kuwa yuko likizo.

Badala yake alielekeza maswali hayo kwa Naibu Katibu mkuu wa Wizara… ambaye naye alitaka kwanza kuona maswali ya maandishi.

Licha ya kupewa maswali kwa maandishi hadi sasa imekuwa vigumu kupata majibu yake.
Hata hivyo akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake, ofisa mmoja katika wizara hiyo, alisema kuwa serikali ilikurupuka kutangaza mradi huo kwani haikuwa na fedha za kuutekeleza.

"Mradi huo utagharimu kiasi cha Sh13 trilioni ambazo ni sawa na bajeti ya mwaka mzima ya serikali. Fedha hizo hazipo, badala yake walitegemea kutafuta wawekezaji watakaokuja kuujenga mradi huo, ila hadi sasa hawajapatikana, ndiyo maana muda unakwenda na hakuna kinachoendelea" alisema Ofisa huyo.

Maneno hayo yanaungwa mkono na Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile akisema kuwa serikali haina uwezo wa kutekeleza mpango huo.

"Ukweli ni kwamba serikali haina uwezo wa kutekeleza huo mpango kwa sasa. Ikiwa bajeti ya serikali ya Sh13 trilioni inategemea wafadhili, fedha ya kutekeleza huo mradi itatoka wapi?" alihoji Ndugulile.

http://www.mwananchi.co.tz/mwananch...9-mradi-wa-mji-mpya-kigamboni-wayeyuka-kiaina

Wadanganyika mmeliwa tena...CCM Oyeeee!!!!!!
 
Back
Top Bottom