Kigamboni Blue Diamond of Tanzania project..

mtoto wa mama

Senior Member
Jan 11, 2011
188
18
Wana JF

Bado nashidwa kuelewa kuhusu mradi wa jiji jipya la Kigamboni maana nina kibanda changu huku nimeitwa mara ya pili kwa ajili ya uhakiki maana first time ilikuwa 2008 wakasema tusiendeleze chochote lakini miaka mitatu imepita bila lolote..

Sasa mwaka huu nimehakiki tena sasa sielewi maana ni kama huu mradi upo au ndio dana dana za magamba kwani kuna permit za ujenzi bado zinaendelea kutolewa tu..

Naomba mnijuze wenye info zaidi.
 
tafadhali soma ripoti hii tuliitayarisha baada ya miradi ya uendelezaji maeneo yaliyoko pembezoni mwa Jiji la Dsmikiwemo Kigamboni kuanza kutekelzwa utapata majibu.
 

Attachments

  • MRADI WA KUENDELEZA MAENEO YALIYOKO PEMBEZONI MWA DSM UNACHOCHEA UMASKINI MIONGONI MWA WAKAZI WA.pdf
    678.8 KB · Views: 236
  • Thanks
Reactions: Paw
usijenga huko kaka ...kama upo ndani ya eneo lao ..kwa sababu watakukaushia hadi nyumba yako iishe ..ukishahamia tu wanakuja kuipiga X then hulipwi kitu wala nini ..tafuta maeneo yapo kibao tu yaliyopimwa kama unapenda kuishi kigamboni nenda kakodishe nyumba kaka....
 
hapa nilipo nina video inayoonyesha jinsi mradi huo utakavyoanza, mji utakavyopangwa, nk....kwa mujibu wa waandaji wa video hii wanasema mradi huo utaanza mwaka huu 2011 na kuisha mwaka 2030....kama ntaweza ntaiweka hapa maana imezungumzia mradi huo kugawanywa katika maeneo makuu 5..international business center, industries, education center, tourism, residential areas na transport centers
 
ile project haiwezi tekelezeka ktk uongozi huu, kwan mpaka sasa wapo nyuma ya ratiba. Ni project nzuri bt isiyotekelezeka bongo! Ingekuwa inasimamiwa na Prince wa dubai yule aliyekuja na Mega structure ya Palm island ningekua na iman 100%
 
kuna yeyote mwenye info kuhusu maendeleo ya huu mradi na viwanja vinavyouzwa kwa mara ya pili Kibada?
 
kwa kuwa ni mpango wa freemason lazima utekelezeke uliza kilichomleta bush
 
hapa nilipo nina video inayoonyesha jinsi mradi huo utakavyoanza, mji utakavyopangwa, nk....kwa mujibu wa waandaji wa video hii wanasema mradi huo utaanza mwaka huu 2011 na kuisha mwaka 2030....kama ntaweza ntaiweka hapa maana imezungumzia mradi huo kugawanywa katika maeneo makuu 5..international business center, industries, education center, tourism, residential areas na transport centers
Bado masaa kadhaa tu mwaka uishe na mradi bado haujaanza.
 
Dr Ndungulile, tafuteni majibu ya ukweli. Lini hii project itaanza?????? Miezi mitatu iliyopita kulifanyika zoezi la kuweka X kuonyesha barabara mpya zitakapopita au zilizopo zitakavyoongezwa, sasa chakushangaza Jamaa hawajarudi tena kwa wananchi. Waziri Lukuvi naye aliahidi mwendo wa kasi kwenye project lkn yamekuwa yale yale ya Mhe Tibaijuka. Kulikoni? Sisi wananchi ndio tunaumia kwa kuwa ardhi haina thamani na huweza kuapply kupata title
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom