Kigamboni: Askari Magereza wamuua Neema Dominic kwa risasi wakati wakimdhibiti raia aliyeachiwa huru na Mahakama

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,567
9,026
Leo askari wa magereza wameua msichana Neema Dominic , mkazi wa Tuamoyo aliyemaliza kidato cha nne mwaka juzi.

Kifo hicho kimetokana na Askari Magereza kumfyatulia risasi mfungwa aliyekuwa ameachiwa na Mahakama wakitaka kumkamata tena ndipo risasi walizomfyatulia zikampata Neema na kumuua papo hapo, nyingine zikimjeruhi mama yake mzazi.

_____
Maoni Yangu:

Hivi haya mauaji ya askari kwa RAIA mpaka lini?

========


Dar es Salaam. Neema Dominick mkazi wa Kigamboni Mtaa wa Tuamoyo jijini Dar es Salaam amefariki dunia baada ya kupigwa risasi katika eneo la paja na askari Magereza.

Baada ya risasi iliyomuua Neema kutokea upande wa pili pia ilimjeruhi mama yake mzazi, Rehema Ibrahimu katika eneo la paja.

Mauti hayo yalimpata Neema jana akiwa nyumbani kwao karibu na Mahakama ya Kigamboni wakati askari wa Magereza alipokuwa akijaribu kumzuia mtuhumiwa asitoroke mahakamani.

Akizungumzia tukio hilo, kaka wa marehemu, Juma Mwinjaku alisema kabla ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alitoroka kwa mara ya kwanza askari wakafanikiwa kumdhibiti kabla ya kutoroka tena na kuamua kutumia risasi kumzuia.

“Mara zote alipotoroka alikuwa akitumia upande ambao nyumba yetu ipo jambo ambalo lilifanya hata walipotumia risasi kuwa rahisi kutufikia.”

“Lakini kwa nini watumie risasi kumzuia mtuhumiwa ilhali wanajua eneo lile liko karibu na makazi ya watu pamoja na shule? Kwa nini hawaangalii madhara yanayoweza kutokea kwa watu,” alihoji.

“Binti huyo alimaliza kidato cha nne mwaka juzi kuna wakati alikuwa akitaka kwenda jeshini akakosa nafasi hivyo alikuwa yupo nyumbani tu akisubiri utaratibu mwingine,” alisema

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa aliyekuwa akizuiwa kwa risasi alikuwa tayari ameachiliwa na Mahakama.

Chanzo: Mwananchi
 
Na hiyo mpaka Mropokaji aje kumwamuru Katibu mkuu aunde kamati ya uchunguzi itachukua muda.

Hapa ndo weredi wa jeshi la Polisi huwa haueleweki. Wanamfungulia mtu mashtaka, mahakama inamwachia huru then wanatumia sheria vibaya kukamata tena.

Kibaya zaidi utakuta kesi yenyewe ni ya kipuuzi tu.

Halafu Kuna mpuuzi mmoja alisema polisi wa Tanzania wanamafunzo ya kulenga shabaha, wakilenga hawakosei. Sasa ajitokeze tena kujibu na hili maana hawachelewi kusema kuwa huyo aliyeua hajulikani.
 
Hawa askari wetu wana shida sana, Elimu ya darasani imewashinda tena ukienda huko magereza four zimejazana kwa idadi kubwa...

Bado wameenda depo na wamejifunza kulenga ( range ) ila bado wanashindwa kupata shabaha...

Apumzike kwa Amani binti mdogo...
 
Hivi ni kwa nini hii sheria ya mtu kuachiwa mahakamani halafu Kukamatwa tena isifutiliwe mbali?? Akisha futiwa mashtaka yake asiguswe tena wakitaka wamtafute upya... Halafu sikubaliani kabisa na mtu kukamatwa ilihali uchunguzi haujakamilika. Why wasikamilishe uchunguzi ndiyo mtu akamatwe na kesi kuanza right away?? How come askari aliyekwenda training anashindwa kulenga mtu miguuni? Anashindwa kufanya quick assessment kubaini anaweza kupiga risasi in public bila kuleta madhara? Ingekuwa wakiuwa kizembe wanafungwa hii kitu ingeisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo askari wa magereza wameua msichana Neema Dominic , mkazi wa Tuamoyo aliyemaliza kidato cha nne mwaka juzi.

Kifo hicho kimetokana na Askari Magereza kumfyatulia risasi mfungwa aliyekuwa ameachiwa na Mahakama wakitaka kumkamata tena ndipo risasi walizomfyatulia zikampata Neema na kumuua papo hapo, nyingine zikimjeruhi mama yake mzazi.

_____
Maoni Yangu:

Hivi haya mauaji ya askari kwa RAIA mpaka lini?
Rip Neema mbele yako nyuma yetu

Jr
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom