Kigali Rwanda

picha 2 ni Nairobi teleposta tower na iyo ya blue ni I&m building next to kenol kobil tower
 
Tumekuelewa. Na swali lako ni zuri sana. Asante.
Katiba ya Afrika ya Kusini inasema hivi "Afrika ya Kusini ni ya watu wote wanaoishi".

Ni kweli neno au maana "Uzawa" limekuwa likizungumziwa sana.
Makaburu wanasema kuwa wao ni Wazawa pia. Maana hawajapishana sana na Uhamiaji wa kabila la Wazulu ambao ndio wengi kuliko wote. Wazulu pia ni Wahamiaji.

Na tukisema "Mzawa" katika Bara hili ni Mbantu tuu, Basi tutakosea maana kuanzia Equator kwenda juu, tabaka la Wabantu ni Wachache sana.

Afrika ya Kusini imejengwa na watu wote.
Makaburu hao waliishi hapo Afrika ya Kusini kama nyumbani kwao na waliijenga nchi hiyo kwa Uzalendo mkubwa. Waliwaona Waingereza kama Wakoloni, na waliwapinga, walipigana nao na walipandisha bendera ya Uhuru. Hawakuweka mguu mmoja ndani, na mmoja nje. Na hata baada ya kuwapa Waafrika Uhuru wao, bado Makaburu wameendelea kuisaidiana Serikali kujenga nchi yao.
Saa nyingine Makaburu wanaonyesha Uzalendo wa hili bara zaidi ya wewe na mimi.
Makaburu hawakutorosha mali na kwenda kujenga Ulaya au sehemu nyingine duaniani.

Walichokosea ni Imani zao potofu kuwa Mwenyezi Mungu aliwapa Afrika kama zawadi, na Mwafrika amezaliwa kumtumikia Mtu mweupe mpaka siku ya Kiama. Ndio maana Makaburu walishirikiana na Israel ya Kizayuni kwa sababu wote wanatawala kwa misingi hiyo hiyo ya Ubaguzi.

Serikali ya Waafrika imejitahidi kurudisha Usawa katika Uchumi kwa kuwapa Waafrika au watu weusi nafasi na wao pia wafaidike. Na kwa kipindi cha miaka 22 sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye kipato cha Mwafrika.

Chama Tawala cha AnC walikuwa na uwezo wa kuwanyang'anya na kutaifisha mali zote kutoka kwenye mikono ya Wazungu wachache. Lakini walijiuliza, je Waafrika wana uwezo huo wa kuendeleza safari hiyo?

Walichukulia mifano katika nchi za Kiafrika waliorithi mazuri kutoka kwa Wakoloni na kuishia kwenye uharibifu tuu.
Uchumi haukuguswa bali ulipanuliwa, na Wazungu na kipaji chao pia walitunukiwa na waliombwa kuwaelimisha Waafrika ambao waliwekwa kwenye giza zaidi ya miaka 400.

Hospitali kubwa kuliko yote duniani, inasemekana iko huko Soweto inaitwa Chris Hani Hospital au Baragwana na ilijengwa na Serikali ya Makaburu na inayoa huduma sisi tunayoifuatia huko India.

Kuinua hadhi ya Mwafrika na kumkomboa kwenye Umasikini, Ubinaadamu ndio imekuwa dini ya Chama Tawala cha ANC.
Sheria za kazi Afrika ya Kusini lazima watu 7 wawe Waafrika, mmoja Mzungu, mmoja Mwindi na moja awe Chotara. Waafrika wamepewa kipa Umbele. Na Waafrika wanasukumwa kwenye nafasi za juu.

Na Mabenki kutoa mikopo, kuzadiwa Tenda za Serikali, kupewa nafasi za biashara, zinapewa kipaumbele kampuni zilizokuwa na Wafanyakazi wengi walio Watu Weusi.

Hatuangalii kwenye Google, tumeshafika Rwanda, na tumeshafika Sasolburg.

Kama wewe ni mtu wa Gugo, Naomba pia uangalie Mossey Bay. Hii ni miji midogo sana ambayo imeishinda miji au nchi nyingi za Afrika kwa maendeleo, na mifano ya kuiga lakini watu wamenyamza, wamefanya vitu vyao. Binaadamu ana uwezo mkubwa sana.
Mossey bay
 
Hizi hapa picha za Kigali
Czfyk4rXcAIbHq1.jpg
Czfyk4RWgAAEfZW.jpg
Czfyk4-W8AEpu0n.jpg
 
Kigali kuna visehemu viwili tuu ndio wanashinda wanaringisha mitandaoni, mbona bongo zimejaa sehemu kama hizo. Kigali ingekua na BRT ingekuaje? acheni kusifia chui kwa kuua mbu...
 
Back
Top Bottom